Katibu wa UWT Mbeya aliyefariki kwa ajali, maiti yake imepata ajali ikisafirishwa

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Gari iliyobeba mwili wa Marehemu aliyekuwa katibu wa UWT mkoa wa Mbeya, Lucy Sulle, kutokea mkoani Mbeya ukielekea mkoani Babati kwa ajili ya mazishi, nalo limepata ajali maeneo ya Chemba, saa 10 alfajiri huku watu kadhaa wakiwa wameumia na kupelekwa hospitali ya Chemba kwa ajili ya matibabu.

Baadhi ya Majeruhi kwenye ajali hiyo wamepelekwa Hospitali General iliyopo mkoani Dodoma huku wengine waliopata majeraha madogo wamehudumiwa na kuruhusiwa.
Aidha gari jingine lilipatikana na kubeba mwili huo na kuendelea na safari mkoani Babati kwa ajili ya mazishi.

Pia soma: Aliyekuwa Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake CCM Mbeya Lucia Sule afariki Dunia baada ya kukaa ICU siku 36

Siku zote alikuwa hajazikwa tu,habari ya lini hii?
 
View attachment 3292006
Alipata ajali kwenye msafara,akapata majeraha hatimae akafa. Amefariki anasafirishwa tena gari iliyombeba imepata ajali. Mh! Dunia hii Ina mambo kweli kweli
 
Ukiweza kufanya maboresho ya taarifa yako, Babati ni Wilaya iliyopo katika Mkoa wa Manyara, hatuna Mkoa wa Babati bali Mkoa wa Manyara.

Pole sana Kwa hao majeruhi, Mungu awape uponyaji wa haraka
 
Back
Top Bottom