Katika Afrika ni Watanzania tu ndo tuna kifungua kinywa (Breakfast)

Katika Afrika ni Watanzania tu ndo tuna kifungua kinywa (Breakfast)

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,583
Reaction score
27,838
Nimebahatika kutembelea nchi mbalimbali Afrika (Kusini mwa Sahara); nilichokiona ni kwamba wengi hawana utamaduni wa kifungua kinywa asubuhi (Mzungu huita breakfast).

Najua hata Tanzania yetu pia sio wote wanapata kifungua kinywa, lakini ni jambo la kawaida hasa mijini, asubuhi kupata kikombe cha chai au wengine hata kahawa na chapati/andazi/kitumbua/mkate.
 
Hakika ukitafuta chai asubuhi nchi hizo utapata tabu sana na wala supu hakuna. Udinya ugali tu muda ukifika.
 
nchi gani hizo?maana kenya,Uganda,zambia Malawi na hata DRC breakfast ipo kama kawa.
 
Bila kutaja mbadala wa breakfast , Bado hujakamilisha uzi
 
Mozambique hamna chakula cha mchana

Asubuhi ni mnakula msosi mzitoooo Yan heavy[emoji123][emoji123] mchana deshi hadi jioni/usiku tena hapo vitu vilaini na matunda pembeni

Mtanzania ukifika huko lazima upate shida kidogo maana wengi tumezoea asubuhi chai na vitafunwa kidogo mchana msosi wa maana na usiku pia
 
Nimebahatika kutembelea nchi mbalimbali Afrika (Kusini mwa Sahara); nilichokiona ni kwamba wengi hawana utamaduni wa kifungua kinywa asubuhi (Mzungu huita breakfast)

Najua hata Tanzania yetu pia siyo wote wanapata kifungua kinywa, lakini ni jambo la kawaida hasa mijini, asubuhi kupata kikombe cha chai au wengine hata Kahawa na chapati/andazi/kitumbua/mkate.
Wengine hawafungui kinywa wanafanyaje ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom