Katika ardhi ya Palestina nini kinawapa kipato raia wake?

Kila anaembariki Mpalestina amebarikiwa na anaemlaani,amelaaniwa
Haya maneno we umeyapata wapi?? Hivi wagala mnajua mlivyokuwa mazuzu nyie ndo na wenzenu wote 😃,, mnavyowashobokea hao waisrael ambao hawataki hata kuwasikie nyie na ukristo wenu,, kwa hiyo na wagala wenzenu wanayoiunga mkono Palestina nao vp mana wapo pia..
 
Siku ukiandika hoja,nitaijibu ila Kwa sasa bado.
 
Niko hapa Lebanon tangu 2008 Tangarian nilipotoka Zanzibar. Najua nacho kiandika. Wengi huko nyumbani wanaambiwa au kuhadithiwa mengi ya uongo. Media mnazoangalia nyingi zinarubuni hususan mfumo wa maisha ya Gaza
 
Niko hapa Lebanon tangu 2008 Tangarian nilipotoka Zanzibar. Najua nacho kiandika. Wengi huko nyumbani wanaambiwa au kuhadithiwa mengi ya uongo. Media mnazoangalia nyingi zinarubuni hususan mfumo wa maisha ya Gaza
Kazi zipo ila hapo kuna uwekezaji wa mataifa mengi ,vita ya pale nyuma ya pazia ni mikono ya watu nje ya Gaza
 


Hayo maghorofa walijengewa na Serikali ya Israel baada ya makubaliano ya 1990. Pia walikuwa wanapewa umeme na maji bure. Na wanaitegemea aisrael kwa ajira, isipokuwa wale wafanyakazi wa mamlaka ya ndani ya Palestine. Hata hiyo Serikali ya Palestine ilikuwa ikipewa pesa za kuendeshea Serikali yao, na Israel.

Maghorofa yote yalikuwa ni ya msaada. Na sahizi kuna offer ua msaada tena ya kujengewa maghorofa na Jumuia ya nchi za kiarabu, na offer nyingine ni ya Marekani ya kuwahamisha na kwebda kuwajengea huko watakakohamishiwa.
 
Wengi wapo displaced kwa hio wanatumiwa pesa na ndugu zao
 
Wanaishi Kwa misaada na pia Wana ndugu wengi nchi za ulaya na uarabuni.
 
Wapalestina wanafahamika kama Most educated Refugees in the world, wana vyuo na scientist wakubwa wakubwa Duniani, pamoja na kwamba wanaonewa kila siku, ukiangalia data za Stanford kuna Vyuo Palestine vinatoa hadi scientist 17 ambao wapo kwenye top 2% ya best scientist.

https://www.najah.edu/en/research/n...-of-world-scientists-in-2024-stanford-ranking.

Kutokana na population yao kuwa educated wanatengeneza vitu vyao wenyewe kujikimu, wakipewa misaada wanatumia effectively etc.

Kwenye industries zao wanatengeneza wenyewe Textiles, leather, vitu vya mawe kama limestone, cement etc, Matunda, mafuta kama ya olive etc.
Baadhi ya video zikionesha viwanda vyao

Hapa kefiyah

View: https://m.youtube.com/watch?v=srKwguAYRT4&pp=ygUUUGFsZXN0aW5lIEluZHVzdHJpZXM%3D
Hapa leather


View: https://m.youtube.com/watch?v=S4E465h9CAc&pp=ygUcUGFsZXN0aW5lIEluZHVzdHJpZXMgbGVhdGhlcg%3D%3D
Hapa sabuni

View: https://m.youtube.com/watch?v=yPsYOnGPOZk&pp=ygUeUGFsZXN0aW5lIEluZHVzdHJpZXMgbGltZXN0b25l
Wana viwanda vya kisasa pia ila na kuonesha hivyo local ili uone akili za hao jamaa, wanaweza tumia crude tools na kutengeneza viwanda vyenye output kama hizo,

Wana Export karibia $700M ambayo per capita wapo Vizuri kushinda hata sisi.

So soon utaanza kuona hapo Gaza maghorofa yanasimama tena, Mtu ambaye anatengeneza bunduki ama sniper kutoka Bomba la maji kujenga kwake sio Tatizo.
 
Boss Palestina wana Madokta 210 kila watu 100,000 Tanzania una Madokta 2 kila watu 100,000 wamekuzidi kama mara 100 hivi,

Unahisi Madokta ni msaada? Unaenda shule kusoma, unapiga Moyo konde badala ya kuzamia nchi nyengine na kula Mshahara wa maana unarudi kwenu kwenye Vita kusaidia wenzako.
 
Kunamahali nimesema palestina hakuna madoctor au. Hawana wasomi? Bas tufaanye sna nachojua wewe unajua zaid👐
 
Hamas wao zaidi ya VITA wana jishughulisha na nini?
Hamas wana wings mbili, upande wa Jeshi na upande wa siasa, Hamas kama Chama cha siasa ndio Serikali ya Gaza,

1. Wanatoa Elimu, tena bora literacy rate Gaza ni asilimia 97, for comparison hakuna Nchi yoyote Sub Sahara Africa inayoipita Palestina kwa karibu inalingana na shelisheli ambayo ni asilimia 96.

2. Huduma za Afya, kama huko juu nilivyoandika kila wapalestina 100,000 kuna madaktari 210, for comparison Tanzania Ina madaktari wawili kila watu 100,000, kwa sub Sahara Africa ni Mauritius na shelisheli pekee ndio wamewapita Palestina nchi zote zilizobakia zimepitwa.

3. Kumaintain security na order. Nitakupa mfano wakati wa Covid 19 Maimamu walikuwa replaced na Madokta misikitini, Ukienda kuswali daktari anasimama kutoa hotuba namna ya kujilinda na Covid na hatua za kuchukua.

4. Foreign relations, Hamas wanategemea support toka Nchi mbalimbali kama Iran, Qatar, Uturuki, China, North Korea, Urusi etc kote huko inabidi kuwe na watu Kumaintain relationship.
 
Wengi wao wana elimu nzuri wengi Wahandisi, Madaktari bingwa, wasanifu majengo, pamoja nahayo wasio na ajira wanalima sana Zabibu,mboga wanafuga, wana fukwe nzuri hasa Gaza kwaajili ya utalii waisrael walikua wanalipa pesa ndefu mapumziko beach, waliobahatika katika ajira wameajiriwa na wanafanya kazi ndani ya Israel wanalipwa
vizuri sana lakini wanatakiwa wawe nje ya geti la kuingilia israel saa kumi na mbili jioni watoke wote
 
Kipato chao ni Manna na Salwa
 
West bank na Gaza zile zinaitwa mamlaka ya Palestine. Kumbuka sio nchi. Wamepewa mamlaka madogo na Israel kuokota kodi ndani ya ya west bank na gaza, kwa ajili ya huduma ndogondogo kama afya na elimu.
Wengi wa wapalestina wana vishughuli vya kujipatia kipato. Wanapata pia msaada toka nje haswa kwenye nchi za kiarabu.
 
Kwanini hujauliza zile siraha nzito nzito wanatoa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…