Katika Dunia ya Kidijitali, kwanini Mwananchi abebeshwe mzigo wa vitambulisho?

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
379
Reaction score
1,412
Ni jambo la kusikitisha kuona mwananchi wa kawaida analazimika kubeba kadi takribani 10 kila siku ili kupata huduma mbalimbali.

Kuanzia Kitambulisho cha Taifa (NIDA), kadi ya mpiga kura, kadi ya benki, ya ajira, ya bima ya afya, hadi kadi za usafiri au zile za klabu zaa michezo, mzigo huu wa vitambulisho umekuwa kero kubwa.

Jambo la kushangaza zaidi, taasisi hizi zote hufanya kazi kana kwamba zipo katika Dunia tofautitofauti, kila moja ikihitaji kitambulisho chake, hata pale ambapo kuna uwezekano mkubwa wa kushirikiana kwa taarifa kupitia mifumo ya pamoja.

Hali hii inaonyesha ukosefu mkubwa wa ushirikiano wa kimfumo miongoni mwa taasisi za umma na binafsi.

Mbaya zaidi, hali hii inaweka hatarini Usalama wa Taarifa Binafsi pale Mwananchi anapopoteza mojawapo ya vitambulisho hivyo.

Zama hizi za maendeleo ya teknolojia ya Kidigitali, haileti picha nzuri tena kwa Taifa lenye wasomi kutokuwa na mfumo wa pamoja wa utambuzi wa mtu mmoja (Integrated National Digital Identity System).

Tuna wataalamu wa TEHAMA nchini, na pia tuna mifano mingi mambo makubwa ya kimfumo za zaidi ya hilo ambayo tumeweza kufanya vizuri, tunaweza kutumia uzoefu huu kufakisha hili pia kwa maslahi mapana.

Kitambulisho kimoja cha Taifa chenye uwezo wa kuhifadhi taarifa za msingi za mtu mmoja ikiwa ni pamoja na taarifa za afya, ajira, bima, huduma za kifedha, na nyinginezo kinaweza kutumika kama kitovu cha utambuzi wa huduma zote.

Iwapo kutakuwa na sababu za kiusalama au kiutendaji, basi si vibaya kuwa na vitambulisho viwili vya msingi, kimoja kwa huduma za kijamii na kingine kwa huduma za kifedha.

Mfumo huu jumuishi unaweza kusaidia zaidi kupunguza gharama kwa Wananchi na taasisi, kuongeza ufanisi na kurahisisha upatikanaji wa huduma,kutoa ulinzi madhubuti kwa taarifa binafsi pia kusaidia katika kutoa takwimu sahihi kwa ajili ya kupanga maendeleo.

Wito wangu kwa Serikali na Mamlaka husika
Kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wakala ya Serikali Mtandao (eGA), Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), na taasisi zote zinazohusika, kuanzisha mchakato wa kuunganisha mifumo ya utambuzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Iwapo kuna changamoto za kisera au kiutekelezaji, wadau wa sekta husika wakae pamoja kutoa maoni na mapendekezo ya pamoja.

Ni wakati wa kuondoa urasimu wa vitambulisho vingi na kuanza safari ya kuwa na mfumo mmoja jumuishi wa utambulisho wa kidigitali ili kutupunguzia wananchi usumbufu iliyopo sasa.
 
Ni wakati wa kuondoa urasimu wa vitambulisho vingi na kuanza safari ya kuwa na mfumo mmoja jumuishi wa utambulisho wa kidigitali ili kutupunguzia wananchi usumbufu iliyopo sasa.📌🔨
 
Bank zote wangekuwa na CPU moja.. Kama wameweza hivyo kwa wafanyakazi nina hakika kwa wateja haishindikani
Serikali nayo ingekuwa na CPU moja kwenye vitqmbulisho vyake (NIDA, LESENI, KURA)
Hivyo mtu unajikuta una kadi mbili tu zenye kila huduma na katika zote NIDA ndiyo ingekuwa kadi kuu
 
Upo sahihi, ujumbe huu ufike kwa mamlaka husika.
 
mkuu, situliambiwa kuna shida ya mifumo kusomana, tunaweka mambo sawa tatizo litatatuliwa hivi punde pale uwezo wa mifedha utakaporuhusu na changamoto za kiutendaji kurekebishwa kwa sasa kipaumbele ni uchaguzi ukamilishaji wa sgr na kuhakikisha tunapata umeme wa uhakika.
 
Umeongea jambo zuri Mkuu .

Uzi Kama huu aliandika Mshindi wa story of change mwaka 2022.

Kuwa tunabidi kuunganisha Vitambulisho na taasisi kusomana .

Tungekuwa na I'd moja inakuwa Kama Account unaweka Vyeti Vyako kuanzia kuzaliwa Vya vifo kitaaluma na I'd zako zote umo.

Hii inaongeza usalama na pia inatuhamisha katika dunia ya kubeba makaratasi mengi yasiyokuwa na Msingi.

Mfano MTU kamaliza Chuo sio lazima akachukue cheti unamuingizia katika ID yake .

Hard copy zinakuepo Ila zisiwe Kama ilivyo sasa hivi.
 
Nimechungulia wallet yang u ninazo sita
NIDA
LESENI
BANK 4(NMB2, CRDB 1, SC1)
YA KIVUKO
Ni mzigo mzito kwakweli na ikitokea wallet imeenda na wahunj hapo ndio kilio cha kuanza kuripoti na Ku renew kila mojawapo
Hapo ongezea kadi ya mabasi ya mwendokasi. Nao wametoa kadi zao usiponunua hupandi izo basi.
 
Bank zote wangekuwa na CPU moja.. Kama wameweza hivyo kwa wafanyakazi nina hakika kwa wateja haishindikani
Serikali nayo ingekuwa na CPU moja kwenye vitqmbulisho vyake (NIDA, LESENI, KURA)
Hivyo mtu unajikuta una kadi mbili tu zenye kila huduma na katika zote NIDA ndiyo ingekuwa kadi kuu
Kadi ni moja tuu.

Ilitakiwa mtu unapozaliwa unapewa namba. Hiyo namba yako ndio unatengenezewa kitambulisho kimoja (smart card) na taarifa zako zote zinawekwa humo. Ukimaliza shule, wana update, ukipata leseni wana update, ukipata kazi sijui nssf nini wana update humo, ukifungua account wana update. Kila kitu unafanya kwa kutumia kadi yako hiyo.

Na kwa karne hii ni aibu kusema eti mifumo haisomani. Seriously?
 
Naona tayari nhif wameungana na Nida.wanatumia namba ya nida.
Unaambiwa huna haja ya kitambulisho.namba yako hiyohiyo ya nida ukienda nayo hospital taarifa zako zipo unapata huduma
Ni hatua nzuri sana.. Sasa huduma zote za serikali ziunganishwe hapo
 
Kadi ni moja tuu.

Ilitakiwa mtu unapozaliwa unapewa namba. Hiyo namba yako ndio unatengenezewa kitambulisho kimoja (smart card) na taarifa zako zote zinawekwa humo. Ukimaliza shule, wana update, ukipata leseni wana update, ukipata kazi sijui nssf nini wana update humo, ukifungua account wana update. Kila kitu unafanya kwa kutumia kadi yako hiyo.

Na kwa karne hii ni aibu kusema eti mifumo haisomani. Seriously?
Sitaki kuingiza siasa hapa lakini naamini tukiweza kuwa na "SIASA MPYA"kabisa hili jambo linawezekans kabisa.. Ni kitu cha mwaka mmoja tuu
 
Umeongea jambo zuri Mkuu .

Uzi Kama huu aliandika Mshindi wa story of change mwaka 2022.

Kuwa tunabidi kuunganisha Vitambulisho na taasisi kusomana .

Tungekuwa na I'd moja inakuwa Kama Account unaweka Vyeti Vyako kuanzia kuzaliwa Vya vifo kitaaluma na I'd zako zote umo.

Hii inaongeza usalama na pia inatuhamisha katika dunia ya kubeba makaratasi mengi yasiyokuwa na Msingi.

Mfano MTU kamaliza Chuo sio lazima akachukue cheti unamuingizia katika ID yake .

Hard copy zinakuepo Ila zisiwe Kama ilivyo sasa hivi.
Online account yenye taarifa zako zote ambazo ziko connected na database ya nchi.. China wameweza kupitia wechat
 
Ni jambo la kusikitisha kuona mwananchi wa kawaida analazimika kubeba kadi takribani 10 kila siku ili kupata huduma mbalimbali.

Kuanzia Kitambulisho cha Taifa (NIDA), kadi ya mpiga kura, kadi ya benki, ya ajira, ya bima ya afya, hadi kadi za usafiri au zile za klabu zaa michezo, mzigo huu wa vitambulisho umekuwa kero kubwa.

Jambo la kushangaza zaidi, taasisi hizi zote hufanya kazi kana kwamba zipo katika Dunia tofautitofauti, kila moja ikihitaji kitambulisho chake, hata pale ambapo kuna uwezekano mkubwa wa kushirikiana kwa taarifa kupitia mifumo ya pamoja.

Hali hii inaonyesha ukosefu mkubwa wa ushirikiano wa kimfumo miongoni mwa taasisi za umma na binafsi.

Mbaya zaidi, hali hii inaweka hatarini Usalama wa Taarifa Binafsi pale Mwananchi anapopoteza mojawapo ya vitambulisho hivyo.

Zama hizi za maendeleo ya teknolojia ya Kidigitali, haileti picha nzuri tena kwa Taifa lenye wasomi kutokuwa na mfumo wa pamoja wa utambuzi wa mtu mmoja (Integrated National Digital Identity System).

Tuna wataalamu wa TEHAMA nchini, na pia tuna mifano mingi mambo makubwa ya kimfumo za zaidi ya hilo ambayo tumeweza kufanya vizuri, tunaweza kutumia uzoefu huu kufakisha hili pia kwa maslahi mapana.

Kitambulisho kimoja cha Taifa chenye uwezo wa kuhifadhi taarifa za msingi za mtu mmoja ikiwa ni pamoja na taarifa za afya, ajira, bima, huduma za kifedha, na nyinginezo kinaweza kutumika kama kitovu cha utambuzi wa huduma zote.

Iwapo kutakuwa na sababu za kiusalama au kiutendaji, basi si vibaya kuwa na vitambulisho viwili vya msingi, kimoja kwa huduma za kijamii na kingine kwa huduma za kifedha.

Mfumo huu jumuishi unaweza kusaidia zaidi kupunguza gharama kwa Wananchi na taasisi, kuongeza ufanisi na kurahisisha upatikanaji wa huduma,kutoa ulinzi madhubuti kwa taarifa binafsi pia kusaidia katika kutoa takwimu sahihi kwa ajili ya kupanga maendeleo.

Wito wangu kwa Serikali na Mamlaka husika
Kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wakala ya Serikali Mtandao (eGA), Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), na taasisi zote zinazohusika, kuanzisha mchakato wa kuunganisha mifumo ya utambuzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Iwapo kuna changamoto za kisera au kiutekelezaji, wadau wa sekta husika wakae pamoja kutoa maoni na mapendekezo ya pamoja.

Ni wakati wa kuondoa urasimu wa vitambulisho vingi na kuanza safari ya kuwa na mfumo mmoja jumuishi wa utambulisho wa kidigitali ili kutupunguzia wananchi usumbufu iliyopo sasa.
Dah nimeshapoteza kimoja cha NIDA hapa na mawazo balaa
 
sema shida nyingi za TZ ni zipo makusudi kwa ajili ya ulaji wa viongozi sio kwamba hawafahamu iyo issue ni wanatambua sema wakitatua iyo shida watakosa ulaji,
 
Ni wakati wa kuondoa urasimu wa vitambulisho vingi na kuanza safari ya kuwa na mfumo mmoja jumuishi wa utambulisho wa kidigitali ili kutupunguzia wananchi usumbufu iliyopo sasa...
Mdogo mdogo tutafika tu kwenye (bbb).... REVELATION 13..
 
Back
Top Bottom