Wyatt Mathewson
JF-Expert Member
- Dec 22, 2017
- 10,770
- 25,419
unalia wakati ndio opportunity ya wewe kutoa solution na kua bilionea?Ni jambo la kusikitisha kuona mwananchi wa kawaida analazimika kubeba kadi takribani 10 kila siku ili kupata huduma mbalimbali.
Kuanzia Kitambulisho cha Taifa (NIDA), kadi ya mpiga kura, kadi ya benki, ya ajira, ya bima ya afya, hadi kadi za usafiri au zile za klabu zaa michezo, mzigo huu wa vitambulisho umekuwa kero kubwa.
Jambo la kushangaza zaidi, taasisi hizi zote hufanya kazi kana kwamba zipo katika Dunia tofautitofauti, kila moja ikihitaji kitambulisho chake, hata pale ambapo kuna uwezekano mkubwa wa kushirikiana kwa taarifa kupitia mifumo ya pamoja.
Hali hii inaonyesha ukosefu mkubwa wa ushirikiano wa kimfumo miongoni mwa taasisi za umma na binafsi.
Mbaya zaidi, hali hii inaweka hatarini Usalama wa Taarifa Binafsi pale Mwananchi anapopoteza mojawapo ya vitambulisho hivyo.
Zama hizi za maendeleo ya teknolojia ya Kidigitali, haileti picha nzuri tena kwa Taifa lenye wasomi kutokuwa na mfumo wa pamoja wa utambuzi wa mtu mmoja (Integrated National Digital Identity System).
Tuna wataalamu wa TEHAMA nchini, na pia tuna mifano mingi mambo makubwa ya kimfumo za zaidi ya hilo ambayo tumeweza kufanya vizuri, tunaweza kutumia uzoefu huu kufakisha hili pia kwa maslahi mapana.
Kitambulisho kimoja cha Taifa chenye uwezo wa kuhifadhi taarifa za msingi za mtu mmoja ikiwa ni pamoja na taarifa za afya, ajira, bima, huduma za kifedha, na nyinginezo kinaweza kutumika kama kitovu cha utambuzi wa huduma zote.
Iwapo kutakuwa na sababu za kiusalama au kiutendaji, basi si vibaya kuwa na vitambulisho viwili vya msingi, kimoja kwa huduma za kijamii na kingine kwa huduma za kifedha.
Mfumo huu jumuishi unaweza kusaidia zaidi kupunguza gharama kwa Wananchi na taasisi, kuongeza ufanisi na kurahisisha upatikanaji wa huduma,kutoa ulinzi madhubuti kwa taarifa binafsi pia kusaidia katika kutoa takwimu sahihi kwa ajili ya kupanga maendeleo.
Wito wangu kwa Serikali na Mamlaka husika
Kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wakala ya Serikali Mtandao (eGA), Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), na taasisi zote zinazohusika, kuanzisha mchakato wa kuunganisha mifumo ya utambuzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Iwapo kuna changamoto za kisera au kiutekelezaji, wadau wa sekta husika wakae pamoja kutoa maoni na mapendekezo ya pamoja.
Ni wakati wa kuondoa urasimu wa vitambulisho vingi na kuanza safari ya kuwa na mfumo mmoja jumuishi wa utambulisho wa kidigitali ili kutupunguzia wananchi usumbufu iliyopo sasa.
wewe unataka matatizo yote yatatuliwe halafu nyie mtakua mabilionea lini?
sipeendagi mambo ya malalamiko wakati ndio fursa hizi