Babarazack
Senior Member
- Sep 9, 2015
- 135
- 162
Habari wana jukwaa, mimi sio mwanasiasa wala sio mwanaharakati huru/wa kujitegemea lakini nimejikuta nikitamani kusema haya nikiwa kama raia ninaejali utu,usamala na uhai wa raia wote nchini ambao ndiyo msingi/mtaji wa mwanasiasa yeyote duniani,sasa niwakumbushe tu kuna kale ka msemo ka wahenga kanakosema,”Usifurahi kumnasa kware,shukuru na mtego uliokusaidia kumnasa”
Macho yangu
Kimsingi suala hili ni kubwa kiasi cha kuitikisa dunia katika Nyanja zote kuanzia uchumi,dini mpaka chini kabisa katika utamaduni upande wa mila na desturi.
Hivyo ni jambo ambalo kila aitwae binadamu mwenye akili zake timamu na anayejua thamani ya uhai kwa viumbe anapaswa kusimama katika nafasi yake kupambana kwa kadiri ya uwezo wake hadi sekunde ya mwisho kuhakikisha adui huyu wa wote COVID-19 anapotea kabisa katika uso wa dunia na kuruhusu shughuli zote za kawaida za mwanadamu hususani zile za kila siku kuendelea kama ilivyokuwa hapo awali.
Chanzo cha tatizo
Anza kwa kuangalia katika nchi ambazo ugonjwa huu umeanzia kisha jiulize maswali machache ili tuweze kujifunza kitu,
1.Suala la CORONA wamelipa uzito gani?
2.Wametumia mbinu gani kupambana na wamefanikiwa kwa kiasi gani?
3.Licha ya mbinu walizotumia wameathiriwa kwa kiasi gani? (hii ni ktk nyaja zote)
4.Mbinu walizotumia zilikuwa na ubora au udhaifu kiasi gani?
5.Ni changamoto zipi walikutana nazo?
Kisha maswali hayo hayo tuyarudishe katika nchi yetu,je kuna mfanano wa majibu?
Kuna watu watasema huwezi kuzifananisha China,Spain,Italy,Marekani,Uingereza na Tanzani.sawa basi tulinganishe na jirani zetu wa Uganda je sisi na wao ni sawa?
Je, BOBI WINE anaipinga serikali kuhusu CORONA?
Vita ni ya wote
Tatizo limeanza katika swali namba moja hapo juu, katika nchi yetu suala hili tumelipa uzito kwa kuwa ndiyo habari inayorindima kwa sasa duniani lakini shida kubwa ipo kwa wananchi mwitiko ni mdogo sana katika kuzingatia yale tunayoambiwa na wataalamu.Pili wanasiasa wetu wanalichukulia hili kama sehemu ya kujipatia faida za kisiasa, kwamba akisimama jukwaani,bungeni, kwenye chombo cha habari au katika mitandao ya kijamii anatumia nafasi hiyo kukosoa hatua zinazochukuliwa na serikali dhidi ya ugonjwa huu bila kutoa hatua stahiki zitakazoweza kutuvusha katika kipindi hiki kigumu,harakati zao ni kutaka kuitoa serikali katika target kwa kuanzisha mapambano mengine dhidi ya serikali wakati huu serikali inapopambana na CORONA bila kujali kuwa jitihada hizo zinalenga kuwanusuru mpaka wapiga kura wao ambao wamewaweka madarakani na ambao bado wanawahitaji wapiga kura hao hao ifikapo mwezi oktoba wawapigie kura ili waendelee kubaki katika nafasi hizo.
Serikali nayo licha ya kuwa imesimama vizuri sana katika mapambano haya lakini kwa kiasi Fulani kumekuwa na mkanganyiko wa kauli na miongozo inayotolewa mfano naibu waziri wa afya aliwahi kusema kuwa Barakoa za vitambaa hazisaidii kujikinga na virusi vya corona lakini baada ya siku chache kauli zilizotoka wenyewe mnazijua na mwisho jana waziri amesema barakoa za vitambaa zinazozalishwa nchini zinatakiwa zipewe kipaumbele. Kwa hiyo hapo kuna shida kidogo.
Wapinzani waiunge mkono serikali
Me nawashauri wapinzani wote nchi kuwa watafute faida za kisiasa katika kuunga mkono mapambano haya nafikiri kwao itakuwa na tija Zaidi kuliko wakibeza na kuanzisha migomo isiyokuwa na sababu ambayo mwisho wake ni kupoteza Imani kwa wapiga kura wao kwa sababu vitendo hivi tafsiri yake ni kuwasaliti wapiga kura wao katika kipindi kigumu. Badala yake wanapaswa kurudi na kushirikiana nao kwa nguvu zote,”nendeni kwa wahisani tafuteni pesa mje mtoe hata misaada ya barakoa,sanitizer,sabuni na vinginevyo.kwanini hamjifunzi kwa makampuni,wafanyabiashara na wasanii hawa wanaojitolea?
Au hamjui kua nyinyi mmewekwa na wananchi na mnalipwa kutokana na kodi za wananchi?
Nyinyi ndo mlipaswa kuwa na uchungu Zaidi kwa watu hawa na siyo kuwasaliti.Mpaka wanaona watu wa mbali kuwa kuna haja ya kutoa misaada wakati nyinyi ndiyo watu wenu hawa na mnanufaika kutokana na hawa”
Ona sasa spika amewashtaki kwa wapiga kura wenu…eti mmechukua pesa kisha mkakimbia
Serikali,”miluzi mingi humpoteza mbwa”
Ipo haja ya serikali yetu tukufu kuamini kuwa mipango na mikakati yake ni thabiti na kila uamuzi unaotolewa ni sahihi hivyo wasisikilize mwangwi unaojirudia baada ya wao kutamka wasonge mbele huku kupishana kauli sio poa.wananchi wote tunaunga mkono juhudi hizi.
Kama corona haichagui chama kwanini sisi tujigawe katika kupambana nayo?