Katika hili la corona wapinzani wanapoteza credit

Katika hili la corona wapinzani wanapoteza credit

Wapinzani waunge vipi mkono juhudi za kupambana na Corona wakati ushauri wa wataalamu wa afya haufuatwi? mfano. kupima kujua walioambukizwa?

Wewe unataka wapinzani waungane na serikali kwenye nyungu, maombi, na kupeleka ndege madagascar kwenye dawa ya kienyeji ambayo haijafanyiwa majaribio popote, mbona unawafundisha ujinga hao wapinzani!.

Halafu suala la kuiunga mkono serikali kwenye haya mapambano eti ili wapate uungwaji mkono kisiasa, hapo ndio umevurugwa kabisa; watanzania wa leo sio wajinga, kumbe wewe unaitumia Corona kama mtaji wa kisiasa?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Umenielewa vzr ila umepindisha kidogo,sijasema waunge mkono nyungu au wazo la kufuata dawa madagascar hapana mimi niwashauri wasiwatenge wapiga kura wao watafute namna ya kuwa pamoja nao katika mapambano kama kipindi cha kampeni wanatoa kanga,tshirt na cap kwanini wasitafute barakoa wakagawa?

Alafu kufanya hivyo co dhambi na wala haimaanishi kuwa wanataka kura zao hapana,ni katika kushikana mkono kipindi cha matatizo.

Mbona ni juzi tu hapa wananchi walichangishwa ili kulipa faini za viongozi wao mbona viongozi hawa hatuwaoni tena kipindi hiki cha Corona?

Mwisho kama wanazo mbinu mbadala za kupambana na corona waseme basi ili zitusaidie wote.
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaweza kuwa sina akiri kama wewe lakini nikawa na akili kukuzidi.Kuna hekima ya haya mambo.Yesu alivyotaka kuuawa na Herode,alikimbilia Misri.je,Mungu mkuu alishindwa kumlinda?
Tunaposema bunge ni mkusanyiko usio na lazima tuna maanisha kulingana na mazingira ya sasa sio lazima kwenda bungeni.
Wewe mwenye akiri twambie hao wana waza nini kama upo kichwani mwao, la pili wamefanya nini kikubwa ambacho wewe umekuona kitasaidia?

Nimemsikia mwenyekiti wako anasema kwa yale maamuzi ya kujifungia wengi wapewe. Sasa yeye mbona kakimbia bungeni bila kusubili kula ya wengi wapewe?

Awaache walioamua kuingia bungeni kutumikia wananchi wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimsingi ni kwamba hauna akili iliyo huru.Hata kama unadai sio mwanasiasa wala mwanaharakati lakini una ukilaza fulani hivi.Try to think out of box.utaelewa maana ya wao kufanya waliyofanya.Lakin vilaza ambao wengi ni ccm basi hawawezi kujua mambo makubwa wao ni mambo ya ndio mzeendio mazee

Sent using Jamii Forums mobile app
msukule mwingine wa dj aikael.[emoji115][emoji115][emoji115]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ushauri gani wa WATAALAMU WA AFYA ambao serikali imeupeleka kwa wananchi kisha wapinzani wakaacha kuunga mkono ikiwa wapinzani walikamatwa tu kwa kugawa barakoa bure kwa wananchi? wananchi tuko macho hatujalala, tunaona na tunasikia kila kitu, endeleeni kutudharau hivyohivyo.
 
Yaweza kuwa sina akiri kama wewe lakini nikawa na akili kukuzidi.Kuna hekima ya haya mambo.Yesu alivyotaka kuuawa na Herode,alikimbilia Misri.je,Mungu mkuu alishindwa kumlinda?
Tunaposema bunge ni mkusanyiko usio na lazima tuna maanisha kulingana na mazingira ya sasa sio lazima kwenda bungeni.

Sent using Jamii Forums mobile app

Basi warudishe pesa, hakuna mtu atawafatafata. Kama mkusanyiko hauna haja.
 
Watanzania tunawaelewa Sana Cdm ,tuko pamoja yaani msirudi bungeni,yafe hayohayo ya ccm kwa njaa zao.
 
Ww ni ccm pure . Just declare your interest ili ueleweke vzr

DUMU KUBWA
 
Kwanza wewe ni member, ni either umetakatishwa kuwa mpiga porojo mpya au una ban umei gia kwa jina jipya humu.

Si mwanasiasa ila mpiga porojo wa CCM, Mbonak hoja zako haziko huru na ni pumba kama zilivyo pumba hoja za wapiga porojo wa CCM wengi?

Wapiga porojo wa CCM huwa mna tabia zinazo fanana, mosi huwa hamnaga references za mapitio mnapoleta hoja zenu, wengiwenu waropokaji tuu, kiufupi mna hoja za nguvu na si nguvu za hoja, ref, kuzima TV bunge live, maana mnajijua ni pumba kwenda mbele.

Hivi kama wewe una akili utafuata chochote mtu anasema hata kama ni wehu? Hamjifunzi, hivi tume ya kina Osoro si ingekuwa rejea nzuri saana? Maana Noah zetu zimepeperuka, na mind you muongo akiwa amakudanganya kilasiku na wewe kama zoba unakubari uongo kirahisi hukuona fala! Hebu jipime kundi linalokuhusu kwa sasa
 
Upinzani umekosa uongozi Tangu Slaa aondoke, umebaki utoto na kutafuta sympathy toka Magharibi. Octoba 2020 CDM itafikia Mwisho kuwa chama kikuu cha Upizani na Mbowe atakuwa kama Mrema.
Kama huna cha kuandika bora usome ya wenzako alafu akae kimya,hivi uongozi wa Mboe utaufananisha na hao wapuuzi wapiga makofi,hivi kuwaaambia watu jamani tuchukue taadhari na kuwaambia watu tujiweke karantiini ili tusiendeelee kuambukizana ni kutafuta symphath,au hujui maana ya sympathy,acha pumba bwege wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana jukwaa, mimi sio mwanasiasa wala sio mwanaharakati huru/wa kujitegemea lakini nimejikuta nikitamani kusema haya nikiwa kama raia ninaejali utu,usamala na uhai wa raia wote nchini ambao ndiyo msingi/mtaji wa mwanasiasa yeyote duniani,sasa niwakumbushe tu kuna kale ka msemo ka wahenga kanakosema,”Usifurahi kumnasa kware,shukuru na mtego uliokusaidia kumnasa”

Macho yangu

Kimsingi suala hili ni kubwa kiasi cha kuitikisa dunia katika Nyanja zote kuanzia uchumi,dini mpaka chini kabisa katika utamaduni upande wa mila na desturi.

Hivyo ni jambo ambalo kila aitwae binadamu mwenye akili zake timamu na anayejua thamani ya uhai kwa viumbe anapaswa kusimama katika nafasi yake kupambana kwa kadiri ya uwezo wake hadi sekunde ya mwisho kuhakikisha adui huyu wa wote COVID-19 anapotea kabisa katika uso wa dunia na kuruhusu shughuli zote za kawaida za mwanadamu hususani zile za kila siku kuendelea kama ilivyokuwa hapo awali.

Chanzo cha tatizo

Anza kwa kuangalia katika nchi ambazo ugonjwa huu umeanzia kisha jiulize maswali machache ili tuweze kujifunza kitu,

1.Suala la CORONA wamelipa uzito gani?

2.Wametumia mbinu gani kupambana na wamefanikiwa kwa kiasi gani?

3.Licha ya mbinu walizotumia wameathiriwa kwa kiasi gani? (hii ni ktk nyaja zote)

4.Mbinu walizotumia zilikuwa na ubora au udhaifu kiasi gani?

5.Ni changamoto zipi walikutana nazo?

Kisha maswali hayo hayo tuyarudishe katika nchi yetu,je kuna mfanano wa majibu?

Kuna watu watasema huwezi kuzifananisha China,Spain,Italy,Marekani,Uingereza na Tanzani.sawa basi tulinganishe na jirani zetu wa Uganda je sisi na wao ni sawa?

Je, BOBI WINE anaipinga serikali kuhusu CORONA?

Vita ni ya wote

Tatizo limeanza katika swali namba moja hapo juu, katika nchi yetu suala hili tumelipa uzito kwa kuwa ndiyo habari inayorindima kwa sasa duniani lakini shida kubwa ipo kwa wananchi mwitiko ni mdogo sana katika kuzingatia yale tunayoambiwa na wataalamu.Pili wanasiasa wetu wanalichukulia hili kama sehemu ya kujipatia faida za kisiasa, kwamba akisimama jukwaani,bungeni, kwenye chombo cha habari au katika mitandao ya kijamii anatumia nafasi hiyo kukosoa hatua zinazochukuliwa na serikali dhidi ya ugonjwa huu bila kutoa hatua stahiki zitakazoweza kutuvusha katika kipindi hiki kigumu,harakati zao ni kutaka kuitoa serikali katika target kwa kuanzisha mapambano mengine dhidi ya serikali wakati huu serikali inapopambana na CORONA bila kujali kuwa jitihada hizo zinalenga kuwanusuru mpaka wapiga kura wao ambao wamewaweka madarakani na ambao bado wanawahitaji wapiga kura hao hao ifikapo mwezi oktoba wawapigie kura ili waendelee kubaki katika nafasi hizo.

Serikali nayo licha ya kuwa imesimama vizuri sana katika mapambano haya lakini kwa kiasi Fulani kumekuwa na mkanganyiko wa kauli na miongozo inayotolewa mfano naibu waziri wa afya aliwahi kusema kuwa Barakoa za vitambaa hazisaidii kujikinga na virusi vya corona lakini baada ya siku chache kauli zilizotoka wenyewe mnazijua na mwisho jana waziri amesema barakoa za vitambaa zinazozalishwa nchini zinatakiwa zipewe kipaumbele. Kwa hiyo hapo kuna shida kidogo.

Wapinzani waiunge mkono serikali

Me nawashauri wapinzani wote nchi kuwa watafute faida za kisiasa katika kuunga mkono mapambano haya nafikiri kwao itakuwa na tija Zaidi kuliko wakibeza na kuanzisha migomo isiyokuwa na sababu ambayo mwisho wake ni kupoteza Imani kwa wapiga kura wao kwa sababu vitendo hivi tafsiri yake ni kuwasaliti wapiga kura wao katika kipindi kigumu. Badala yake wanapaswa kurudi na kushirikiana nao kwa nguvu zote,”nendeni kwa wahisani tafuteni pesa mje mtoe hata misaada ya barakoa,sanitizer,sabuni na vinginevyo.kwanini hamjifunzi kwa makampuni,wafanyabiashara na wasanii hawa wanaojitolea?

Au hamjui kua nyinyi mmewekwa na wananchi na mnalipwa kutokana na kodi za wananchi?

Nyinyi ndo mlipaswa kuwa na uchungu Zaidi kwa watu hawa na siyo kuwasaliti.Mpaka wanaona watu wa mbali kuwa kuna haja ya kutoa misaada wakati nyinyi ndiyo watu wenu hawa na mnanufaika kutokana na hawa”

Ona sasa spika amewashtaki kwa wapiga kura wenu…eti mmechukua pesa kisha mkakimbia

Serikali,”miluzi mingi humpoteza mbwa”


Ipo haja ya serikali yetu tukufu kuamini kuwa mipango na mikakati yake ni thabiti na kila uamuzi unaotolewa ni sahihi hivyo wasisikilize mwangwi unaojirudia baada ya wao kutamka wasonge mbele huku kupishana kauli sio poa.wananchi wote tunaunga mkono juhudi hizi.

Kama corona haichagui chama kwanini sisi tujigawe katika kupambana nayo?

Hili gazeti nilidhani lina cha maana, kumbe upuuzi mtupu.
 
Umenielewa vzr ila umepindisha kidogo,sijasema waunge mkono nyungu au wazo la kufuata dawa madagascar hapana mimi niwashauri wasiwatenge wapiga kura wao watafute namna ya kuwa pamoja nao katika mapambano kama kipindi cha kampeni wanatoa kanga,tshirt na cap kwanini wasitafute barakoa wakagawa?

Alafu kufanya hivyo co dhambi na wala haimaanishi kuwa wanataka kura zao hapana,ni katika kushikana mkono kipindi cha matatizo.

Mbona ni juzi tu hapa wananchi walichangishwa ili kulipa faini za viongozi wao mbona viongozi hawa hatuwaoni tena kipindi hiki cha Corona?

Mwisho kama wanazo mbinu mbadala za kupambana na corona waseme basi ili zitusaidie wote.
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanashauri mara ngapi na hakuna anaefatilia ushauri wao,ni mara Mdee na Msigwa wamesema uletwe msaaada wa dharura tujadili korona nani alifata,zaidi ya wapiga makofi kupinga tu,na pia wabunge walikuwa wanagawa Barakoa matokeo yake mbunge anakamatwa na polisi na kuambia haruhusiwi ampe mkuu wa mkoa,aĺafu unakuja na pumba zako,huruhusiwi kusema bila kufanya utafiti,ungekuwa umaesikiliza tokea mwanzo usingewalaumu Chadema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiulize hii..

1. "Baba Tupime watoto wako woteeeeee ukiwepo na ww" mtu wa kwanza

2. "Jamani Baba yetu kwanini usitupime ili tujue Afya zetu Baba tutakuwa na usalama zaidi tukipimwa wotee" wa pili

3. "Jamani Baba huko Nje watu wanapatwa na shida sasa sis tupime tujue tupo vzr maana tayari wapo wenzetu walishasikika kuwa wamejifungia ndan sabab ya huu ugonjwa baba naomba tupime" wa tatu, nne, tano-kumi.

4. "Sasa nasemaje mm nashauri turudini katka tamaduni zetuu tupigee Nyun... maana hakuna dawa kwahyo tujifukkz"

5."Mara paaaaap mwanafamilia wa kwanza anafariki,wa pili anaenda, wa tatu anaondoka"

Unategemea watoto wenye akili wasikuache hapo ili wao wakatafakari tunawaokoaje ndugu zetu hawa kuilko kukubali kuendelea kuumueleza mtu anayekupuuzaaaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni uhuru wao kugomea na kukubali kile wanachoona kinafaa na kukataa kile wanachoona hakifai,kama wameamua kuangalia uhai wao kwanza ni wajinbu wetu kuwaacha kwani wao siyo wanasiasa,nje ya siasa wana majina mengine wanaitwa,wanaitwa baba,wanaitwa mama,wanaitwa mume,wanaitwa mke,wanaitwa mwanangu.
Kama wameamua kutoipa kipaumbele siasa kwa sasa tuiwaache,kama wameamua kutoka bungeni tuwaache,kwani ni lazima washiriki,mangapi yanmepita bila wao kuwepo na mangapi waliyapinga na yakapitishwa wao wakiwepo au ni kipi wanaweza kukizua kisioite wakiwepo.
Jukumu lao kubwa ni kuikumbusha serikali.
 
Back
Top Bottom