Katika hili la Rais Samia kuwaamini Wapinzani Freeman Mbowe ana mchango mkubwa, apongezwe

Katika hili la Rais Samia kuwaamini Wapinzani Freeman Mbowe ana mchango mkubwa, apongezwe

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wote tunajua serikali ya Rais Samia ina waziri mmoja na manaibu waziri watano waliopitia kwenye mikono ya Mbowe kimalezi pale Chadema.

Tunaye waziri Kitila Mkumbo na tunao manaibu waziri Mwita Waitara David Silinde, Gekui, Dr Mollel na Patrobas Katambi wote wakiwa wamelelewa na Mbowe.

Pia tunaye mkuu wa mkoa anayeheshimika sana Dkt. Anna Mghwira ambaye alipitia CHADEMA.

Na tunaye naibu waziri mstaafu Juliana Shonza ambaye amelelewa sana na Mbowe pale Chadema.

Hivyo mchango wa mawaziri hawa waliotengenezwa Chadema ni wazi umechangia kwa kiwango fulani mkuu wa nchi kutamani kufanya kazi na wachapa kazi wa upinzani bila ya wao kuhama vyama vyao.

Hongera Freeman Mbowe, hongereni Chadema, hongereni Upinzani.

Kazi Iendelee!
 
Kuna "juice" za aina nyingi sana wapinzani huwa wanadanganywa nazo kuanzia enzi za Kikwete, mwambie Rais Mbowe anataka Katiba Mpya au akishindwa hiyo basi Tume Huru ya uchaguzi, hivyo vyeo vyenu kaeni navyo.
 
Mbowe ndio walewale wapinzani uchwara mbele mlungula anawasaliti huku mnajiona
 
Tanzania hii ni ya watanzania wote regardless tofauti za kiitikadi,welldone President Samia so far ur doing very well na Mwenyezi Mungu akupe nguvu na ujasiri wa kuyafanya yote uliyopangia kuifanyia nchi yetu,viva president viva!!
 
Back
Top Bottom