Columbus
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 2,002
- 651
Mwaka jana mwezi August-September nilikuwa nahitaji fundi wa kupaua nyumba yangu, kwa bahati nzuri jirani yangu alikuwa anamfahamu fundi fulani nikachukua namba yake ya simu nikamuita.
Baada ya kuitathmini kazi yangu alisema anaiweza na baada ya muda mfupi aliianza ikiwa vifaa vyote pamoja na mbao, misumari na mabati aina ya IT trough vilikuwa juu yangu. Baada ya wiki moja alinikabidhi kazi na mimi nikamkabidhi pesa zake kama ujira.
Sasa mvua zilipoanza mwezi ule wa February nikagundua nyumba aliyopaua yule fundi inavuja isivyo kawaida kiasi kwamba kuna sehemu zingine ukisimama kwa robo saa wakati mvua inanyesha unakamua shati.
Nilipoona hivyo nilimpigia simu na kumjulisha tatizo hilo ili aje aone aweze kurekebisha lakini kwa mshangao hakuja na nilivyokuwa nikiendelea kumpigia simu alikuwa anakata simu zangu na nikitumia namba nyingine anapokea na kunikatia simu baada ya kusikia sauti yangu.
Wiki iliyopita nilienda Polisi, akaitwa kituoni, alipoulizwa alitoa sababu nyingi zisizo na msingi lakini polisi alishauri tuongee kama tunaweza kulimaliza jambo hili kiungwana ambapo tulikubaliana atakuja kuangalia. Kesho yake kweli alikuja lakini hakuweza kuona lile tatizo la nyumba kuvuja kwa sababu msimu wa mvua umeisha.
Siku hiyo aliyekuja aliahidi kuja tena ili aanze hiyo kazi ya marekebisho ikiwa ni kupandisha paa lote juu lakini kitu cha kushangaza fundi hajatokea na nikimpigia ananijibu kihuni kama vile hawajibiki kwa lolote, nikimpigia Polisi naye hapokei simu yangu.
Hapa JamiiForums nina imani nitapata ushauri. Je, ndugu zangu nichukue hatua gani? nitaufanyia kazi ushauri wenu.
Gharama zote za vifaa ni shiling million 10.
CC: Mtambuzi