Katika hili Sheria inasemaje ?

Katika hili Sheria inasemaje ?

Columbus

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
2,002
Reaction score
651
Mwaka jana mwezi August-September nilikuwa nahitaji fundi wa kupaua nyumba yangu, kwa bahati nzuri jirani yangu alikuwa anamfahamu fundi fulani nikachukua namba yake ya simu nikamuita.

Baada ya kuitathmini kazi yangu alisema anaiweza na baada ya muda mfupi aliianza ikiwa vifaa vyote pamoja na mbao, misumari na mabati aina ya IT trough vilikuwa juu yangu. Baada ya wiki moja alinikabidhi kazi na mimi nikamkabidhi pesa zake kama ujira.

Sasa mvua zilipoanza mwezi ule wa February nikagundua nyumba aliyopaua yule fundi inavuja isivyo kawaida kiasi kwamba kuna sehemu zingine ukisimama kwa robo saa wakati mvua inanyesha unakamua shati.

Nilipoona hivyo nilimpigia simu na kumjulisha tatizo hilo ili aje aone aweze kurekebisha lakini kwa mshangao hakuja na nilivyokuwa nikiendelea kumpigia simu alikuwa anakata simu zangu na nikitumia namba nyingine anapokea na kunikatia simu baada ya kusikia sauti yangu.

Wiki iliyopita nilienda Polisi, akaitwa kituoni, alipoulizwa alitoa sababu nyingi zisizo na msingi lakini polisi alishauri tuongee kama tunaweza kulimaliza jambo hili kiungwana ambapo tulikubaliana atakuja kuangalia. Kesho yake kweli alikuja lakini hakuweza kuona lile tatizo la nyumba kuvuja kwa sababu msimu wa mvua umeisha.

Siku hiyo aliyekuja aliahidi kuja tena ili aanze hiyo kazi ya marekebisho ikiwa ni kupandisha paa lote juu lakini kitu cha kushangaza fundi hajatokea na nikimpigia ananijibu kihuni kama vile hawajibiki kwa lolote, nikimpigia Polisi naye hapokei simu yangu.

Hapa JamiiForums nina imani nitapata ushauri. Je, ndugu zangu nichukue hatua gani? nitaufanyia kazi ushauri wenu.

Gharama zote za vifaa ni shiling million 10.

CC: Mtambuzi
 
  1. Huyo aliyekuunganisha hahusiki tena
  2. ulimthibitisha kwamba ni fundi kisheria?
  3. ulkua na mshauri elekezi/
  4. ulifuata ramani?
  5. Je mlikubaliana bati za gage ngapi na yeye ameweka ngapi?
  6. Gharama ya kurekebisha hapo panapovuja ni shilingi ngapi?
Kisheria

  1. ulipeleka suala polisi kimadai au kijinai? (utapeli etc)
  2. ulitoa statement polisi?
  3. una kusudio la kwenda mahakamani?
Tafuta wanasheria hapo karibu
 
  1. Huyo aliyekuunganisha hahusiki tena

    Hahusiki
  2. ulimthibitisha kwamba ni fundi kisheria?

    Hapana
  3. ulkua na mshauri elekezi/

    Hapana
  4. ulifuata ramani?

    Ramani ilibadilika sio iliyopo ktk ramani
  5. Je mlikubaliana bati za gage ngapi na yeye
    ameweka ngapi?

    Bati nilinunua mimi kwa ushauri wa wataalam wa ALAF
  6. Gharama ya kurekebisha hapo panapovuja ni shilingi ngapi?

    Upande mmoja unatakiwa kupandishwa juu kwa futi 3 zaidi ili kupata slope
Kisheria

  1. ulipeleka suala polisi kimadai au kijinai? (utapeli etc)
    Nilienda kimaridhiano isipokuwa ss nataka kufungua kesi kabisa jinai
  2. ulitoa statement polisi?

    Hapana
  3. una kusudio la kwenda mahakamani?

    Ikibidi niko tayari
Tafuta wanasheria hapo karibu

Msaada wa kisheria utafaa hapo?
 
  1. Huyo aliyekuunganisha hahusiki tena
  2. ulimthibitisha kwamba ni fundi kisheria?
  3. ulkua na mshauri elekezi/
  4. ulifuata ramani?
  5. Je mlikubaliana bati za gage ngapi na yeye ameweka ngapi?
  6. Gharama ya kurekebisha hapo panapovuja ni shilingi ngapi?
Kisheria

  1. ulipeleka suala polisi kimadai au kijinai? (utapeli etc)
  2. ulitoa statement polisi?
  3. una kusudio la kwenda mahakamani?
Tafuta wanasheria hapo karibu

Kama fundi mwenyewe ni muhuni kutafuta mwanasheria ni kutaka kupoteza fedha zaidi, huyo ku deal naye kihuni, wape polisi chao kisha muweke ndani halafu mambao mengine utayajua akishafika hapo.
Kuna mafundi wakorofi mpaka akiwekwa ndani ndiyo akili inafanya kazi, maana atawakusanya ndugu zake wote hapo polisi na hapo wewe utakomaa upewe chako na usumbufu pia.

Unaweka mwanasheria halafu fundi mwenyewe anakimbilia Malinyi kujichimbia.....
 
ndio maana nimemuuliza swali la gharama za hapo panapovuja ili asijikute anatumia laki moja okuokoa elfu hamsini,

lakn mtambuzi unanifukuzia pia kitumbua changu (joke)
 
Kama fundi mwenyewe ni muhuni kutafuta mwanasheria ni kutaka kupoteza fedha zaidi, huyo ku deal naye kihuni, wape polisi chao kisha muweke ndani halafu mambao mengine utayajua akishafika hapo.
Kuna mafundi wakorofi mpaka akiwekwa ndani ndiyo akili inafanya kazi, maana atawakusanya ndugu zake wote hapo polisi na hapo wewe utakomaa upewe chako na usumbufu pia.

Unaweka mwanasheria halafu fundi mwenyewe anakimbilia Malinyi kujichimbia.....

Nilirudi polisi wamenishauri niende mahakamani ili aitwe na baada ya kufika mahakamani wamesema nikaanzie ofisi ya kata ktk baraza la usuluhishi.
 
Ulienda kisiasa weye, Hebu tangaza cha juu halafu uone kama kuna polisi atalaza damu.
Au labda ulikutana na Polisi mlokole, nakushauri ubadilishe kituo, fanya kila mbinu wamsweke ndani kwanza, kule lazima ujinga umtoke na atakurudishia fedha zako
 
yaani babangina umenichefua hapo kwenye bold
Ulienda kisiasa weye, Hebu tangaza cha juu halafu uone kama kuna polisi atalaza damu.
Au labda ulikutana na Polisi mlokole, nakushauri ubadilishe kituo, fanya kila mbinu wamsweke ndani kwanza, kule lazima ujinga umtoke na atakurudishia fedha zako
 
Hapo tayari kulikuwa na mkataba. Alichokifanya huyo fundi ni bleach of contract. Anatakiwa awajibike kwa hilo.
 
Sijui kama mahakama ipi inaruhusu kutumia wakili,nina safari nje ya nchi ufuatiliaji inakuwaje!
 
Ulienda kisiasa weye, Hebu tangaza cha juu halafu uone kama kuna polisi atalaza damu.
Au labda ulikutana na Polisi mlokole, nakushauri ubadilishe kituo, fanya kila mbinu wamsweke ndani kwanza, kule lazima ujinga umtoke na atakurudishia fedha zako
Kuna watu wamezoea kuwekwa lupango mpaka wamezoea na wamekuwa ma-bush lawyer, unamweka leo ndani anasubiri masaa 24 yapite alianzishe na ndugu zake anawaambia hakuna kutoa kitu mpaka mahakamani, fundi anaweza kuja akakuambia mbao mbichi msumari ulikuwa unadunda wakati wa kupiga bati
 
kuna watu wamezoea kuwekwa lupango mpaka wamezoea na wamekuwa ma-bush lawyer, unamweka leo ndani anasubiri masaa 24 yapite alianzishe na ndugu zake anawaambia hakuna kutoa kitu mpaka mahakamani, fundi anaweza kuja akakuambia mbao mbichi msumari ulikuwa unadunda wakati wa kupiga bati

hapo atakua na shift legal burden
 
ulienda kisiasa weye, hebu tangaza cha juu halafu uone kama kuna polisi atalaza damu.
Au labda ulikutana na polisi mlokole, nakushauri ubadilishe kituo, fanya kila mbinu wamsweke ndani kwanza, kule lazima ujinga umtoke na atakurudishia fedha zako

hiyo si kisiasa ni kufuata dispute settlement procedures

  1. negotiation
  2. mediation
  3. reconciliation
  4. arbitration
 
Hapo tayari kulikuwa na mkataba. Alichokifanya huyo fundi ni bleach of contract. Anatakiwa awajibike kwa hilo.
Mkataba wa maandishi au wa mdomo?hata kama ungekuwa ni wa maandishi lakini mkataba wao ni kuezeka bati na kweli bati ameezeka na mwenye nyumba akaridhika akampa chake ila amekuja kugundua kwamba bati linavuja baada ya mvua kuanza kunyesha. kinachotakiwa ni kwanza ni kuonana na huyo aliemkutanisha na fundi (jirani) kuangalia kama kweli ni fundi au alisikia na kupitia huyo jirani aongee nae fundi wake ili aje arekebishe maana huwezi kumpa mtu reference kama kazi yake hujaiona na mafundi wengi mjini ni wa uzoefu wa kazini hata elimu ya kawaida ya darasani walimaliza kwa shida na hata ukimpeleka polisi au mahakamani mwisho wa siku utaulizwa ulijuaje competency yake kama fundi.

Kuna maeneo naungana na Mtambuzi ile ya kumwendea kihuni lakini kuna maeneo pia inabidi mazungumzo pia yaendelee maana kumtia hatiani ni ngumu
 
Last edited by a moderator:
hapo atakua na shift legal burden
Wanambwembwe hao kama hujui unaweza ukaambiwa misumari uliyonunua sio ungeleta ile ya Arusha, ndio maana mie nilitumia fundi mmoja kujenga kutoka msingi mpaka kuezeka, kama fundi aliekujengea mlienda nae vizuri mpka kumaliza boma lote ikitokea hana utaalamu wa kuezeka ni vyema ukamtumia huyo kukutafutia fundi wa kuezeka lakini lazima uhakikishe sehemu ambazo amefanya kazi angalau sehemu hata mbili maana show ya nyumba ni roofing na hawa mafundi huwa wana network nzuri kuanzia sehemu ya kununua mbao na vifaa vingine na wakati mwingine hata ukipungukiwa kama umekaa nae vizuri anaweza akawa refaree na ukachukua vitu dukani unalipa baadae
 
kwenye mikataba ya ujenzi huwa kuna window period ambayoi ni miezi 6..basically kuangali ubora wa kazi ambapo mjenzi anawajibika kwa iwango cha lami, KAMA HIYO ILIPITA HAPO SASA NI KESI NYINGINE NA MKATABA HUO PIA UNAWEZA KUWA BY IMPLICATIONS APART FROM whether was by expression or written
Mkataba wa maandishi au wa mdomo?hata kama ungekuwa ni wa maandishi lakini mkataba wao ni kuezeka bati na kweli bati ameezeka na mwenye nyumba akaridhika akampa chake ila amekuja kugundua kwamba bati linavuja baada ya mvua kuanza kunyesha. kinachotakiwa ni kwanza ni kuonana na huyo aliemkutanisha na fundi (jirani) kuangalia kama kweli ni fundi au alisikia na kupitia huyo jirani aongee nae fundi wake ili aje arekebishe maana huwezi kumpa mtu reference kama kazi yake hujaiona na mafundi wengi mjini ni wa uzoefu wa kazini hata elimu ya kawaida ya darasani walimaliza kwa shida na hata ukimpeleka polisi au mahakamani mwisho wa siku utaulizwa ulijuaje competency yake kama fundi.

Kuna maeneo naungana na Mtambuzi ile ya kumwendea kihuni lakini kuna maeneo pia inabidi mazungumzo pia yaendelee maana kumtia hatiani ni ngumu
 
kwenye mikataba ya ujenzi huwa kuna window period ambayoi ni miezi 6..basically kuangali ubora wa kazi ambapo mjenzi anawajibika kwa iwango cha lami, KAMA HIYO ILIPITA HAPO SASA NI KESI NYINGINE NA MKATABA HUO PIA UNAWEZA KUWA BY IMPLICATIONS APART FROM whether was by expression or written
Amavumbi unaangalia fundi kwenye level ya juu, huyo ni fundi wa mtaani hata ofisi hana (hata approach zake ni za kimtaanimtaani kama alivyofanya mleta uzi maana kama angekuwa wa level hiyo nadhani wala asingekuja hapa). Maana fundi unaemsema wewe ni yule anaekuja na quatation kabisa (BOQ) unazipitia tena wanakuja hata watatu kisha unaangalia yupi kati ya hao unampa kazi kisha mnaandikiana mkataba, mafundi unaowasema wewe lazima kwenye hela yake 5% unakaa nayo just in case kuna sehemu amevurunda aje arekebishe kwenye grace period.
 
Last edited by a moderator:
kama ni wa mtaani sawa, ujenzi wetu huu wa kimasikini nauelewa sana na costs zake ndio hizi sasa
Amavumbi unaangalia fundi kwenye level ya juu, huyo ni fundi wa mtaani hata ofisi hana (hata approach zake ni za kimtaanimtaani kama alivyofanya mleta uzi maana kama angekuwa wa level hiyo nadhani wala asingekuja hapa). Maana fundi unaemsema wewe ni yule anaekuja na quatation kabisa (BOQ) unazipitia tena wanakuja hata watatu kisha unaangalia yupi kati ya hao unampa kazi kisha mnaandikiana mkataba, mafundi unaowasema wewe lazima kwenye hela yake 5% unakaa nayo just in case kuna sehemu amevurunda aje arekebishe kwenye grace period.
 
Aisee watu wengine wanaishi kiupole sana. Yaani huyo fundi unatakiwa kumfanyia umafia tu, ndiyo dawa yake. Kama vipi tafuta watoto wa kihuni umuharibu reception kwanza. Yaani mimi mtu hawezi kuniletea uhuni kama huo halafu nikamuacha tu hivi hivi. Hususani kama anajifanya kichwa ngumu kama huyo.
 
Back
Top Bottom