Katika hili, waafrika tunakosea sana.

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Inasikitisha sana kuona kwamba bado waafrika tunaendelea na tabia ya kulalamika hovyo, na kutaka kujifanya tunaonewa katika mambo Mengi hata kama sisi ndio tuliofanya kosa.

Tabia yetu ya kutopenda kuwajibika, au tabia yetu ya ubinafsi uliokithiri na kujawa na kiburi cha madaraka, vinatufanya tujione ni watu tusiopaswa kuguswa, tunajiona sisi ndio wenye haki ya kutenda tu, ila hatupaswi kutendwa.

Bado wimbo wa mabeberu wanatuonea wivu, hawataki kutuona tunaendelea, umekua ukitumika kama sindano ya ganzi ili kuzilaza bongo zetu zisifikirie nje ya "box". Hii ni hatari sana kwa Afrika na sisi waafrika kwa ujumla.

Serikali hizi za Afrika, zimekua zikiwatesa sana raia wake, zimekua mstari wa mbele katika kuvunja haki za raia zao, lakini pale dunia inapojaribu kupaza sauti, viongozi huanza kuimba wimbo wa " Mabeberu wanatuonea wivu", wivu katika kutesa na kuua raia wenu?.

Wananchi wengi wanaofanya biashara na serikali, hawalipwi pesa zao kwa wakati, wengi wamefuatilia malipo yao kwa miaka mingi sana, wengi wanefilisika na wengine wamejiua kutokana na Madeni yabayowakabili, lakini serikali hazijali kuwalipa bila hata kutoa sababu za msingi. Wananchi hawa hawana la kufanya zaidi ya kuzipigia magoti serikali husika kuomba ziwalipe.

Jambo la kusikitisha zaidi na kushangaza, ni pale ambapo serikali ambayo ndio msimamizi mkuu wa utii wa sheria za nchi, ndio inayoongoza kuzivunja sheria hizo hizo, kwasababu tu wakijua kwamba hakuna wa kuwalazima kutii sheria hizo, wao ndio wenye vyombo vya dola, kwamba serikali inaweza kutii au kutotii amri ya MAHAKAMA.

Anapotokea mtu, nchi au shirika lolote likatumia mbinu yoyote yenye nguvu zaidi ya serikali, ili kuilazimisha serikali kutii AMRI halali za MAHAKAMA, au kutokiuka haki za raia wake, viongozi wa serikali hizi huanza kuanzisha wimbo wa " Mabeberu hawatutakii mema", siku hizi umeongezewa utamu kidogo " wanatuonea wivu", na sisi wananchi tunaanza kuitikia bila hata kujua muktadha mzima wa wimbo kwa wakati ule.

Maamuzi ya kulipwa huyu Mzungu aliyesababishwa kuzuiliwa kwa ndege, yalitolewa na MAHAKAMA za Tanzania, na hata baada ya serikali kukata rufaa, bado mahakama ya rufaa ilimpa haki huyu mzungu, lakini bado serikali ya Tanzania iliendeleza kiburi cha kutomlipa, kama ambavyo inafanya kwa " Government suppliers", kulipa pale inapojisikia. Alipoamua kwenda kuiomba MAHAKAMA ya Africa kusini ili kumsaidia apate haki yake, viongozi wameanzisha wimbo wao wa kawaida "Mabeberu wanatuonea wivu".

Katika hili, tunakosea sana.
 
Hakuna cha maana wanafundishwa kusoma na kuandika majina yao ili waweze kuipigia kura ccm
usikae ndani 2 kwenye tv nenda shuleni kamuulize mkuu wa shule je pesa zinazoletwa na serikali zinatosheleza uendeshaji? Uje usifie tena
 
Kwahivyo wewe pia umeamua kuendeleza utamaduni wa kulialia? Tukiwaambia viongozi wenu, na hicho chama chenu cha mafisi, ni watu ambao hawana muelekeo huwa mnasema kwamba tunawaonea wivu. Pambana na hali yako wewe 'kijana' wa lumumba, buku saba saba huwa unazitafuna pekee yako.
 
Biggie,Waafrica hatuko hivyo hao ni ccm ambao wanataka kutufanya watu weusi tuonekane hatuna maana!
 
Kwa kuongezea, tunataka kuwafungulia mashtaka ya uhujumi uchumi wale wote waliyomsaidia huyu mkulima mpaka kupelekea ndege yetu kushikiliwa...

Ina maana kwamba, hata wale waliyompa ushindi wa kwamba alipwe fidia nao wapo ndani ya msafara...


Cc: mahondaw
 
Hivi mahakama ya Kenya ilipoagiza "servers" za kumpyuta za tume ya uchaguzi zifunguliwe, mlitekeleza?, au ilipoamuru Miguna Miguna arudishwe nchini na kurudishiwa passport yake, Jubilee ilitekekeza?.
Usijaribu kufananisha mahakama za Kenya na huo upuuzi wenu. Server zilifunguliwa na zikakaguliwa na wataalamu wa pande zote mbili pamoja na tume huru ya uchaguzi. Kwenye kesi ya Miguna, mahakama ilifatilia hukumu yake kwa kumuagiza IGP aje ajieleze mbele ya mahakama. Mahakama zenu zina ubavu wa kufanya vitu vya kueleweka kama hivyo au kazi ni kungoja tu maagizo kutoka juu? Kama hii hukumu hapa ya 'senior magistrate'(kada wa chama) kwenye ile kesi dhidi ya Sugu. Yaani ni aibu kubwa kutoka kwa wasomi wenu. Kiingereza kibovu, hukumu yenyewe ni ovyo na ya kishabik, ambayo hainukuu kifungu chochote cha sheria. Hii lazima iliandika na katarist mwenyewe akinywa juisi na pipi pale ikulu.
 

Kafieni mbele huko na mabeberu yenu, hayo mabeberu yalivyosikia kuhusu reports za unyonyaji wa madini yetu walitia neno, wala haina haja ya kusingizia viongozi, sie wananchi wazalendo tutawanyoosha 😏😏😏
 
Na nyie acheni kisebesebu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ eti tukiwaambia, ninyi Mavi kunuka mmwambie nani kitu? Pambaneni na njaa zenu kwanza, CCM ni zaidi ya Kenya yote na Africa
 
Wanapaswa kunyongwa hadharani wala sio kubembelezwa huko mahakamani, kitendo cha wao kuside na beberu kwa nia ovu ya kuihujumu Tanzania ni out of patriotism, hata kama tunadaiwa hatujakataa lakini kitendo cha Watanzania kushiriki kuandaa reinforcement kule South ni kitendo kisicho cha kizalendo kwa taifa lako,

Marekani yenyewe haiwezi kufanya huo upumbavu, tatizo ninyi nyumbu upinzani wenu unaextend mipaka, hii multipartism iliwakuta bila manual descriptions. 😏😏
 
Hivi kuhusu Miguna Miguna umejibu nini?, mahakama zenu ni hovyo zaidi, zimejaa rushwa na hata zikitoa amri Jubilee hawatimizi wanadharau tu.
1) Server za tume ya uchaguzi hadi Leo hazijafunguliwa, ndio Sababu kubwa iliyosababisha NASA kususua uchaguzi wa marudio, hata mambo yanayohusu nchi yako huyajui vizuri, hovyo kabisa wewe.

2) Kuhusu Miguna Miguna, hadi Leo serikali ya Jubilee imegoma kutii amri ya mahakama kumruhusu arudi NYUMBANI, mahakama zenu ni hovyo zaidi, kwanza zimejaa rushwa, pili Jubilee wanadharau sana MAHAKAMA zenu
 

Kafieni mbele huko na mabeberu yenu, hayo mabeberu yalivyosikia kuhusu reports za unyonyaji wa madini yetu walitia neno, wala haina haja ya kusingizia viongozi, sie wananchi wazalendo tutawanyoosha [emoji57][emoji57][emoji57]
Rudi kwenye forum za udaku, huku hakukufai umekosea njia, tunakushukuru kwa mchango wako
 
Biggie,Waafrica hatuko hivyo hao ni ccm ambao wanataka kutufanya watu weusi tuonekane hatuna maana!
Ninyi watu weusi wapumbavu msio na akili ndio mnatuaibisha Pan-Africanists, ninyi ni Vibaraka wa mabeberu msio na akili, trump ni Rais wa marekani lakini anawasemea boers, do you even know them? They are not US citizens bali ni weupe wenzake, ni Waafrika wangapi walikuwa wakiuzwa Libya? Kuna kiongozi hata mmoja wa ulaya Alikemea hilo? Waafrika wangapi wanauwawa cold-blooded na US police?

Lakini kuna litaahira mahali lisilokua na mbele wala nyuma linabwatuka sababu kuna kaburu aliekuwa akishiriki kuwanyonya Waafrika wenzetu kimabavu amefukuzwa Tanzania, huyu mkulima alikua akifadhili apartheid rule, Nyerere alimfurusha sababu alikua ni Pan-Africanist

Ninyi mngekua ndio mmeshika nchi mngegawa mpaka tigo kwa wazungu wawagonge
 
 
Hivi unajua kwamba aliyesema alipwe ni MAHAKAMA kuu ya Tanzania?, kwahiyo hata makama kuu ya Tanzania inashirikiana na mabeberu?. Nilikuomba kwa heshima urudi katika forum za udaku, huku hakukufai.
 
Hivi unajua kwamba aliyesema alipwe ni MAHAKAMA kuu ya Tanzania?, kwahiyo hata makama kuu ya Tanzania inashirikiana na mabeberu?. Nilikuomba kwa heshima urudi katika forum za udaku, huku hakukufai.
Hehehe kupatwa kwa akili kisoda leo

Kwa hiyo unafikiri kila kitu mahakama ikipitisha ni sawa? Ndio maana kuna cort of appeals, suala kama huyo beberu alikua akifadhili apartheid rule haliwezi kuwa justified easy kwenye mchakato wa kimahakama sababu ya sababu fulani fulani

Kama alikuja Tanzania kama investors wengine anahaki ya kulindwa na sheria za Tanzania kama muwekezaji na vile vile International arbitration, hizo sheria hazitambui beberu wala mambo ya apartheid policy so kisa sheria na lawsuits zilizotumika kuendesha case hazitambui hayo mambo haimaanishi kwamba hayo mambo ni mema na huyo mtu hana hatia.

Akili yako nshakuambia ni kisoda, hata kule guantanamo wapo wanaoteswa miaka na miaka lakini mahakamani hawapelekwi kamwe, ni kutokana na kwamba kuna maslahi ya watu fulani waliyaingilia ambayo sio judicial tangible


Akili kisoda wewe kichwa nazi 😏😏😏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…