joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Inasikitisha sana kuona kwamba bado waafrika tunaendelea na tabia ya kulalamika hovyo, na kutaka kujifanya tunaonewa katika mambo Mengi hata kama sisi ndio tuliofanya kosa.
Tabia yetu ya kutopenda kuwajibika, au tabia yetu ya ubinafsi uliokithiri na kujawa na kiburi cha madaraka, vinatufanya tujione ni watu tusiopaswa kuguswa, tunajiona sisi ndio wenye haki ya kutenda tu, ila hatupaswi kutendwa.
Bado wimbo wa mabeberu wanatuonea wivu, hawataki kutuona tunaendelea, umekua ukitumika kama sindano ya ganzi ili kuzilaza bongo zetu zisifikirie nje ya "box". Hii ni hatari sana kwa Afrika na sisi waafrika kwa ujumla.
Serikali hizi za Afrika, zimekua zikiwatesa sana raia wake, zimekua mstari wa mbele katika kuvunja haki za raia zao, lakini pale dunia inapojaribu kupaza sauti, viongozi huanza kuimba wimbo wa " Mabeberu wanatuonea wivu", wivu katika kutesa na kuua raia wenu?.
Wananchi wengi wanaofanya biashara na serikali, hawalipwi pesa zao kwa wakati, wengi wamefuatilia malipo yao kwa miaka mingi sana, wengi wanefilisika na wengine wamejiua kutokana na Madeni yabayowakabili, lakini serikali hazijali kuwalipa bila hata kutoa sababu za msingi. Wananchi hawa hawana la kufanya zaidi ya kuzipigia magoti serikali husika kuomba ziwalipe.
Jambo la kusikitisha zaidi na kushangaza, ni pale ambapo serikali ambayo ndio msimamizi mkuu wa utii wa sheria za nchi, ndio inayoongoza kuzivunja sheria hizo hizo, kwasababu tu wakijua kwamba hakuna wa kuwalazima kutii sheria hizo, wao ndio wenye vyombo vya dola, kwamba serikali inaweza kutii au kutotii amri ya MAHAKAMA.
Anapotokea mtu, nchi au shirika lolote likatumia mbinu yoyote yenye nguvu zaidi ya serikali, ili kuilazimisha serikali kutii AMRI halali za MAHAKAMA, au kutokiuka haki za raia wake, viongozi wa serikali hizi huanza kuanzisha wimbo wa " Mabeberu hawatutakii mema", siku hizi umeongezewa utamu kidogo " wanatuonea wivu", na sisi wananchi tunaanza kuitikia bila hata kujua muktadha mzima wa wimbo kwa wakati ule.
Maamuzi ya kulipwa huyu Mzungu aliyesababishwa kuzuiliwa kwa ndege, yalitolewa na MAHAKAMA za Tanzania, na hata baada ya serikali kukata rufaa, bado mahakama ya rufaa ilimpa haki huyu mzungu, lakini bado serikali ya Tanzania iliendeleza kiburi cha kutomlipa, kama ambavyo inafanya kwa " Government suppliers", kulipa pale inapojisikia. Alipoamua kwenda kuiomba MAHAKAMA ya Africa kusini ili kumsaidia apate haki yake, viongozi wameanzisha wimbo wao wa kawaida "Mabeberu wanatuonea wivu".
Katika hili, tunakosea sana.