Katika hili Wakristo tumepotoka

Katika hili Wakristo tumepotoka

Jokajeusi

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2018
Posts
6,323
Reaction score
10,813
Habari wakuu!!

Mimi ni Mkristo. Tena si yule Mkristo wa kufuata miujiza au wa kufuata mkumbo. Ni mkristo ninayefuata misingi ya maandiko matakatifu kama yanavyosema bila kujali ni nini naamini au nani anaamini. maandiko matakatifu ndio msingi wa maisha ya binadamu wawapo hapa duniani. Kufuata maoni ya watu ni moja ya ukengeufu wa watu wengi hasa sisi Wakristo.

"YESU SIO MUNGU NA HAJAWAHI KUWA MUNGU, NA HATAWAHI KUWA MUNGU"

Wakristo wamejikuta wakivunja moja ya sheria za Mungu bila ya wao kujijua. Moja ya sheria za Mungu ni kutokuiabudu miungu mbinguni bila kujali inaishi wapi na inauwezo kiasi gani. Ngoja ninukuu:
Kutoka 20:
3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

Maandiko hayo yanatutaka tusiabudu miungu mingine. Wakristo tumejikuta tukiingia katika mtego bila kujijua. Wengi wanamhusisha Yesu na Mungu. Wengi wanamuabudu na kumtumikia iwe kwa kujua au la. Lakini ukweli ni kuwa wanavunja sheria hii kubwa ya Mungu. Sababu kubwa ya wao kumuita Yesu ni Mungu bado haipo dhahiri zaidi ya mahaba na imani iliyokosa akili na elimu ya dini. Yesu hawezi kuwa Mungu eti kwa sababu alikufa akafufuka, Alizaliwa bila mbegu ya baba, eti kisa alifufua wafua, kisa alitembea juu ya maji. Nasema hakuna kigezo kinachomfanya Yesu kuwa Mungu.

Yesu ni kiumbe kama walivyoviumbe wengine. Uwezo wake haumfanyi kuwa Mungu. Hata Musa kutenganisha bahari haikumfanya aitwe Mungu. Uwezo wa mtu, akili ya mtu na sifa zinginezo alizonazo mtu hazimfanyi kuwa Mungu. Bali zinamfanya awe mkuu kwa watu au viumbe husika.

Jukumu alilopewa Yesu ni kuitiisha Dunia kwa kurejesha utawala wa Mungu Duniani. Hata hivyo jukumu alilopewa Yesu kama kiumbe chenye heshima katika falme za kiroho ni kuiangusha mamlaka ya Shetani, kumkabili adui Mauti ambaye ndiye adui wa mwisho baada ya lucifa kuwekwa chini ya ulinzi. Na hilo ndilo jukumu la Yesu kuja kuukomboa ulimwengu kutoka katika maadui wawili yaani Shetani ambaye humtumikia Mauti. Hivyo ni kusema Mauti ndiye adui Mkuu ambaye shetani humtumikia.

Zingatia maneno niliyoyakoleza
Soma 1Wakorintho 15:
24 Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.
26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.
27 Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.
28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.

Ndugu zangu Wakristo tuache kuabudu Miungu bila kujijua. Yesu ni kama viumbe wengine. Tunachopaswa ni kumheshimu tuu kama viumbe wengine watakatifu. Hatupaswi kumtumikia Yesu wala kumuabudu isipokuwa Mungu pekee kama Amri za Mungu zisemavyo.

Kama kuna mwenye hoja tafadhali aje na maandiko sio maneno matupu tuu.

Nawasilisha
 
Naweza nikasema ni uchanga wa kiimani au kutokuelewa maandiko kwa ufasaha,
Hata ungekuwa Mkristo wa mizizi ya mbuyu bado huwezi ukalijua Neno for 100%, Najaribu kusema nini?

Umesoma kasehemu kadogo mno kuhusu Yesu sio Mungu, na Ukaweka kuwa kama hiyo mistari yako kidogo iliyoletwa ndio proof kuwa Yesu sio Mungu.

Kuna mambo Kidogo ya Msingi unapaswa kuyajua na kuyatambua kabla haujafikia kuongea jambop fulani.
Kwa mfanoUnaposoma ili uje kuwa tabibu hautaanza kusoma moja kwa moja kuwa tababu la hasha, Jambo la kwanza na La Msingi utatakiwa kwanza Ujifunze kusoma pasipo kujali hamu ayako yakuwa tabibu,

Uatapaswa uanze elimu ya awali kisha ya msingi na kuendelea, Ndio maana hata madereva sio kila mwenye leseni ya gari ataruhusiwa kuendesha basi kama hajakidhi kigezo cha umri.

Niliposoma post yako i mtu unaelewa vizuri sana na nakuona unauelewa mzuri sana ila kuna shida ndogo mno ambayo naona ndi inakusumbua.
Shida kubwa nikwamba umejipa ukomo wa mawazo na kifikra na kufanya watu wote waishie pale ulipoishia wewe, Jammbo Zuri ulipaswa ujiulize mambo kama haya
Je wengine wanajua nini juu ya utata nilio nao?
Je kwanini watu wafuate na kusimamia jambo lisilo sahihi miaka yote hiii?
Nakupa kama mfano tu ambao ungekusaidia kukujengea hoja za msingi na kuanza kujifunza kwanza kupitia makosa ya wengine.

Mbaya zaidi umeleta kujua mbele ya kadamnasi ingekuwa ni vyema ungeleta jambo lako kwa upole na kutaka kujua zaidi ila hoja yako umeileta kibabe Mno.
Kumbuka endapo utatambua na kujua kile umefanya leo nilazima kitakufanya ujutie yale uliyoandika, ila usijari japo hoja yako haitaki wewe kujifunza zaidi ila nitajaribu kukueleza kwa ufupi kwa namna ile namimi ninajua
 
Kabla sijazungumza haya wacha nikufungue kitu kimoja cha muhimu sana
Mimi ni Mlutheli sasa nilikuwa na shida moja sana juu ya ubatizo jambo ambalo lilinisumbua kwa miaka mingi mno,
Mtu sahihi ni yupi anayebatiza kwa kuzamisha ndani ya maji au ambaye hazamishwi?

Lakini pale watu wa madhehebu mengine waliposema sisi Walutheli tunakosea nilichowaza ni hiki?
Kwanini Mungu ajifunue na kujidhihirisha kwa mambo mengine lakini kwanini asitufundishe yakuwa suala la ubatizo tunakosea?
Kwanini Mungu atufunulie jambo fulani lakini asituambie hili la Ubatizo?

Nilipojiuliza maswali hayo nikajua ahaa kumbe kuna jambo laziada mbali na ubatizo ambali watu tunaliacha na kusimamai atu hoja ya ubatizo kama madhehebu Mengine wanakosea.

Maana Mungu hatakuwa Mungu kama akufundishe Mambo mengine na lakini jambo ovu unalofanya kila siku akuache nalo!
Nikama mtoto wako kila siku anaiba unauacha lakini akizini unamwambia haya ni makosa.
Sijui unaipata vyema logic yangu?

Sileti mada ya ubatizo ila najaribu kukupa mfumo ambao unakuwa nimzuri zaidi katika kufuatilia jambo unalotaka kujifunza pasipo kukwazana na wengine lakini pia huenda ukawasaidia kwasababu pia wokovu unapitia kwa mtu yeyote tu.

Sasa nitaenda moja kwa moja katika kukueleza Kwamba Yesu Kuwa Yesu NI Mungu Hatujakosea Wala Hatujakosea kamwe
 
Mkuu ulitafa vifungu tuanze na hivi

Yohana 14.

1:Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia.

2 Katika nyumba ya baba yangu mna nafasi nyingi. Kama sivyo, nisingeliwaambia kwamba nakwenda kuwaandalia makao.

3 Na nikishawaandalia, nitarudi kuwachukua mkae pamoja nami; ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. 4 Ninyi mnajua njia ya kufikia ninakokwenda.”

5 Tomaso akamwuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda; tutaijuaje njia?”

6 Yesu akawaam bia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu.

7 Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.”

8 Filipo akamwambia Yesu, “Bwana, tuonyeshe Baba yako nasi tutaridhika.”

9 Yesu akamjibu, “Filipo, imekuwaje hunifahamu baada ya mimi kuwa pamoja nanyi muda wote huu? Mtu ye yote ambaye ameniona mimi, amemwona Baba. Sasa inakuwaje unasema, ‘Tuonyeshe Baba’?

10 Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu, na Baba yangu yuko ndani yangu? Mambo ninayowaambia siyasemi kwa mamlaka yangu mwenyewe, bali yanatoka kwa Baba yangu ambaye anaishi ndani yangu, na ndiye anayetenda haya yote.

11 Niaminini ninapowaambia ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu na Baba yangu yu ndani yangu. La sivyo, niaminini kwa sababu ya haya mambo ninayotenda.

12 Ninawaambia hakika, mtu ye yote akiniamini ataweza kufanya miujiza kama hii na hata zaidi, kwa kuwa mimi ninakwenda kwa Baba yangu.

13 Kitu cho chote mtakachoomba kwa jina langu, nitawafanyia, ili Baba yangu apate kutukuzwa kwa yale ambayo mimi Mwanae nitawafanyia. 14 Mkiniomba
 
Pia Labda Kabla sijaleta Somo Halisi Naomba Unisaidie Hili Jambo Unalielewa Vipi
Kwanza Ni Ukweli kuwa hakuna mtu ambaye anakuwa na mamlaka sawa Na Mungu, kama yupo mtu anayesema anamamlaka sawa na Mungu basi jua huyo anakufuru na ni dhambi kubwa kujifanya Mungu.

Mfano katika Mamlaka ambazo Mungu anazo ni kama Hizi
1.Kusamehe dhambi
Hakuna mwenye mamlaka ya kusamehe dhambi isipokuwa Mungu pekee, Kwanini Yesu alisamehe dhambi wakati yeye sio Mungu?Kama alisamehe dhambi wakati sio Mungu maana yake alikufuru? Kwanini aliyekufuru awe njia ya kweli na uzima? Mbona Musa alikufuru na aliadhibiwa?
Labda nijibu wkanza hapa kabla sijaendelea
 
Mkuu ulitafa vifungu tuanze na hivi

Yohana 14.

1:Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia.

2 Katika nyumba ya baba yangu mna nafasi nyingi. Kama sivyo, nisingeliwaambia kwamba nakwenda kuwaandalia makao.

3 Na nikishawaandalia, nitarudi kuwachukua mkae pamoja nami; ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. 4 Ninyi mnajua njia ya kufikia ninakokwenda.”

5 Tomaso akamwuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda; tutaijuaje njia?”

6 Yesu akawaam bia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu.

7 Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.”

8 Filipo akamwambia Yesu, “Bwana, tuonyeshe Baba yako nasi tutaridhika.”

9 Yesu akamjibu, “Filipo, imekuwaje hunifahamu baada ya mimi kuwa pamoja nanyi muda wote huu? Mtu ye yote ambaye ameniona mimi, amemwona Baba. Sasa inakuwaje unasema, ‘Tuonyeshe Baba’?

10 Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu, na Baba yangu yuko ndani yangu? Mambo ninayowaambia siyasemi kwa mamlaka yangu mwenyewe, bali yanatoka kwa Baba yangu ambaye anaishi ndani yangu, na ndiye anayetenda haya yote.

11 Niaminini ninapowaambia ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu na Baba yangu yu ndani yangu. La sivyo, niaminini kwa sababu ya haya mambo ninayotenda.

12 Ninawaambia hakika, mtu ye yote akiniamini ataweza kufanya miujiza kama hii na hata zaidi, kwa kuwa mimi ninakwenda kwa Baba yangu.

13 Kitu cho chote mtakachoomba kwa jina langu, nitawafanyia, ili Baba yangu apate kutukuzwa kwa yale ambayo mimi Mwanae nitawafanyia. 14 Mkiniomba

17 Yesu akawaambia, “Baba yangu anafanya mema siku zote. Mimi pia sina budi kufanya mema.” 18 Maneno haya yaliwaudhi sana viongozi wa Wayahudi. Wakajaribu kila njia wapate kumwua, kwa sababu, zaidi ya kuvunja sheria za sabato, alikuwa akijifanya sawa na Mungu kwa kujiita Mwana wa Mungu.

Naona kama dozi kubwa hii kwake maana hatujajua kwanza uelewa wake ni upi, sijajua nini kinamsumbua huyu jamaa
 
Yesu ni Mungu fuatilia maandiko haya...kama huelewi kizungu tafuta Biblia ya Kiswahili:-

1.Thomas answered him, “My Lord and my God!” Jesus said to him, “Do you believe because you see me? How happy are those who believe without seeing me!” (John 20:28-29) .

2. Suddenly Jesus met them and said, “Peace be with you.” They came up to him, took hold of his feet, and worshipped him. (Matthew 28:9) walimuabudu kwa sababu anastahili kuabudiwa kama alivyosema 'Mimi na Baba tu wamoja'

3. John 10:30 I and the Father are one. Mimi na Baba tu wamoja/shirika.

4. John 20:28 Thomas answered him, “My Lord and my God!”

5. Colossians 1:19 For in him all the fulness of God was pleased to dwell,

6. Colossians 2:9 For in him the whole fulness of deity dwells bodily,

7. 2 Peter 1:1 . . . our God and Savior Jesus Christ:

8. Hebrews 1:8 But of the Son he says, “Thy throne, O God, is for ever and ever, the righteous scepter is the scepter of thy kingdom.”

9. In Hebrews 1:6, God the Father also says that all the angels should worship God the Son.

10. The Bible teaches that “God” is judge (1 Sam 2:10; Ps 50:6; Ecc 12:14; many others). But so is Jesus (Jn 5:22, 27; 9:39; Acts 10:42; 2 Tim 4:1). Therefore He is God.

11. God the Father sits on His throne in heaven (1 Ki 22:19; Ps 11:4; 47:8). Jesus is on the same throne, too (Rev 7:17; 22:1, 3).

12. Jesus is God the Son. He is the eternal, all-powerful, all-loving, self-existent Creator God.

Jesus is omnipotent (possesses all power):

Philippians 3:20-21 . . . the Lord Jesus Christ, [21] who will change our lowly body to be like his glorious body, by the power which enables him even to subject all things to himself.

He's omniscient (all-knowing):

Colossians 2:2-3 . . . Christ, [3] in whom are hid all the treasures of wisdom and knowledge.

He's omnipresent (present everywhere):

Ephesians 1:22-23 the church, [23] which is his body, the fulness of him who fills all in all. (cf. Col 3:11)

Sasa wewe joka acha kudanganya watu humu kasome hivyo vifungu vyote vinathibitisha Uungu wa Yesu. YESU NI MUNGU MWANA AMEN
 
Mwanzo1:26 Utatu wa Mungu.Tumfanye mtu kwa mfano wetu.
 
Watunzi wa hivi vitabu walitulia kwa kweli.
 
Maandiko hayo hayo nabii tito amenakiri
Kumbukumbu la Torati 5 : 21 kuna kipengere kinasema usimtamani mjakazi wa mwenzio/jirani yako. Yeye akapata tafsiri kwamba kumbe mjakazi/housegirl wa ndani ni ruhusa kumtamani na kumwingilia sababu mke kamleta amsaidie kazii mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujamiana nae. Labda kama umeongea na Yesu mwenyewe akakwambia yeye sio Mungu. Vinginevyo wewe na nabii tito mko kundi moja. Tunawasiliza wote.
 
Mkuu ulitafa vifungu tuanze na hivi

Yohana 14.

1:Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia.

2 Katika nyumba ya baba yangu mna nafasi nyingi. Kama sivyo, nisingeliwaambia kwamba nakwenda kuwaandalia makao.

3 Na nikishawaandalia, nitarudi kuwachukua mkae pamoja nami; ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. 4 Ninyi mnajua njia ya kufikia ninakokwenda.”

5 Tomaso akamwuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda; tutaijuaje njia?”

6 Yesu akawaam bia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu.

7 Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.”

8 Filipo akamwambia Yesu, “Bwana, tuonyeshe Baba yako nasi tutaridhika.”

9 Yesu akamjibu, “Filipo, imekuwaje hunifahamu baada ya mimi kuwa pamoja nanyi muda wote huu? Mtu ye yote ambaye ameniona mimi, amemwona Baba. Sasa inakuwaje unasema, ‘Tuonyeshe Baba’?

10 Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu, na Baba yangu yuko ndani yangu? Mambo ninayowaambia siyasemi kwa mamlaka yangu mwenyewe, bali yanatoka kwa Baba yangu ambaye anaishi ndani yangu, na ndiye anayetenda haya yote.

11 Niaminini ninapowaambia ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu na Baba yangu yu ndani yangu. La sivyo, niaminini kwa sababu ya haya mambo ninayotenda.

12 Ninawaambia hakika, mtu ye yote akiniamini ataweza kufanya miujiza kama hii na hata zaidi, kwa kuwa mimi ninakwenda kwa Baba yangu.

13 Kitu cho chote mtakachoomba kwa jina langu, nitawafanyia, ili Baba yangu apate kutukuzwa kwa yale ambayo mimi Mwanae nitawafanyia. 14 Mkiniomba
Nilitaka nimtumie hiki vizuri umeanza nakuja nyuma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Isaya 9:6-7
[6]Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele, Mfalme wa amani.
[7]Maongeo ya enzi yake na amani
Hayatakuwa na mwisho kamwe,
Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake;
Kuuthibitisha na kuutegemeza
Kwa hukumu na kwa haki,
Tangu sasa na hata milele.
Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilichotokea kwa yesu ni kwmba
Hakukuwa na mtu mwenye dam safi isiyo na dhambi ambae angeweza kuwaokoa wenye dhambi.
Ikabidi yule mungu mkuu.
Yehova afanyike mwili aje katika umbile la kibinadam aishi na watu kisha damu yake imwagike kama ya mwanadam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yesu alisema kunijua mimi ni uzima
Sehem nyingine akasema je huamini mimi ni ndani ya baba na baba yu ndani yangu na mimi ni ndani yenu. Ni mungu mmoja si mwenye nafsi tatu.
Ila mungu mmoja akifanya kazi mara tatu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NI MUNGU YULE YULE MMOJA AKIFANYA KAZI IWA JINSI AU NAMNA TATU.
WALA MUNGU HANA NAFSI TATU. NDO MANA MYAHUDI HUWEZI KUMPELEKEA MUNGU ULIEMGAWAGAWA AKAKUAMINI.
HAKUNA MAHALI WAMEANDIKA MUNGU ANANAFSI TATU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tito 2:13
[13]tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ukirudi kwa mchangiaji wa kwanza alituma yohana 14
.
Pale yesu anajitambulisha kuwa yeye ndie baba yeye ndie roho mtakatifu.
Maana filipo alimuuliza tuonyeshe baba yatutosha, yeye akajibu akamwambia nikuonyeshe baba! Wewe nimekuwa pamoja nanyi siku izi zote wewe usinijue mimi ni nani.

Mbele anasemaje anasema nitamwomba baba nae atawaletea msaidizi ndie roho wa kweli ulimwengu haumuoni ila nyinyi mnamuona kwa sababu anakaa nanyi sasa.
Alaf anasema siwaachi yatima naja kwenu nikija ulimwengu hautaniona ila nyinyi mtaniona kwa sababu mimi nitakaa ndani yenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binadamu amegawanyika sehem tatu.
MWILI +ROHO+NAFSI.

MWILI wa yesu ulikuwa ni kristo.
ROHO YAKE alikuwa mungu mwenyewe Yehova.
Nafsi ni uhai ama tabia za roho yake ilikuwa ni mungu mwenyewe

Ndio mana imeandikwa amelaaniwa alieangikwa mtini.
Na mungu asingeweza kuipokea laana huo.
Wakati mungu sasa anauacha mwili ambao ndio sadaka.
MWILI UNASEMA BABA BABA MBONA UMENIACHAA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom