Katika hili wanawake wanakosea

Katika hili wanawake wanakosea

mbona mie nilikuwa nampa 35 na alipata? na hapo ni nje ya kila kitu, malazi juu yangu,hata vitu vya kidada nilikuwa namnunulia pale ninapoweza....
Lakini tusi generalised kiivyo kwani mbona kuna watoto wetu kila kitu anapewa na mimba wanapata, shule nzuri, pesa za kutumia, na magari ya shule pia!! mi hapa nnachotaka kusema ni kweli H/G anakua amekosea ila tukiangalia na mazingira ya kwao kumrudisha bila kumsaidia chochote ili aweze kuendesha maisha yake ni kuongeza umaskini kwa ile familia aliotoka!!
 
Jamani mnaona ile rangi nyekundu, hapa ndipo kuna pointi ya maana, jadilini ktk hili,
 
Jamani huyu anamaanisha nyie akina mama mna roho mbaya binti wa watu amepata mimba nyumbani kwako hata roho ya huruma kumsaidia hakuna ndo kwanza unamsepesha haraka haraka hata kama ni mimba ya mmeo.
Waeleze hao, wagumu kuelewa
 
MI nafikiri hapo ni swala la kibinadam zaidi... ukiangalia kwa undani utakuta... dhamira ya kwanza ya huyo mama(mwanamke) kwenda kumchukua binti wa watu ni kwa ajlili ya yeye kufanyiwa kazi.. hapo inamaana swala la kumuangalia kama mtoto wake au mdogo wake halipo (haijalishi kama ana watu kwenye familia wnaolingana na huyo binti).. kwa hiyo lolote litakalotokea basi moja kwamoja hatataka kulifanya jukumu lake...

Hiyo ni changamoto kwa serikali na jamii kwa ujumla.. tunaposema ajira kwa watoto.. mija wapo ni kama haya.. ingawa ni vigumu kumbana mtu kwani wanajifanya ni kama wanasaidia familia maskini kwa kuchukua watoto... mi nafikiri kama serikali ingeweza kufanya tafiti na kuchukua njia mbadala mathalani kuunda chombo ambacho kitasimamia swalal zima la ajira na aina ya kazi zinazohusu majumbani wma watu.. na kuainisha baadhi ya vifungu vya kisheria kuwabana hawa watu... ili ikiwa analeta mtoto wa watu basi kwa mfano ajaze form na kufuata taratibu flani kwa usalama wa utu wa yeye na huyo binti/kijana.....

nafikiri itasaidia kiasi flani kwani kuna wengine hawaishii kumrudisha kwao bali humfukuza na kumuacha binti akitangatanga.. na wakati mwingine mimba ni za wahusika wa familia

NI hayo tu........................
******************************
kuishi Bongo ni kama kucheza draft ukiwa ndani asilimia ya kutambua nakurekebisha makosa ni ndogo... ukiwa nje unagundua makosa mengi na suluhisho kwa mda mfupi.. naona acha nikimbie nchi kidogo... ... i am simply bluffing lol
 
Lakini tusi generalised kiivyo kwani mbona kuna watoto wetu kila kitu anapewa na mimba wanapata, shule nzuri, pesa za kutumia, na magari ya shule pia!! mi hapa nnachotaka kusema ni kweli H/G anakua amekosea ila tukiangalia na mazingira ya kwao kumrudisha bila kumsaidia chochote ili aweze kuendesha maisha yake ni kuongeza umaskini kwa ile familia aliotoka!!

nadhani hututaelewana.......
 
wale wanaowatendea mabaya hawa mabinti, kamwe hatutaelewana nao

hv wewe unazungumzia ubaya gani,mimba nimempa mie?...hapo ni ubinadamu tu kama kumsaidia au laa baada ya tukio la mimba mana ckumtuma afanye hayo, sasa ijekuwa kec kwangu? jaribu kumshirikisha na mkeo nyumbani kwenye hili...kama umeoa lakini.
 
Kama ni ya mmeo, cha kufanya ni kuwaeleza wazazi wake kuwa amekuwa mke mwenzio na sio mfanyakazi tena, mmeo kama atakubali mwambie ampangishie chumba

Hiyo mishahara midogo ndiyo inayosababisha wapewe mimba na wauza mchicha magengeni au wapiga debe,

Msichana anayelipwa kuanzia 30,000/= kwa mwezi hawezi kupata mimba kienyeji hivyo.
No..siyo kweli wanapata tu hata kama ukimlipa zaidi ya 30,000/- mifano tunayo..ila hii mada inamafundisho sana..ni kero kubwa kwenye nyumba zetu "wasichana vs Wake zetu" big issue
Ukijidai ku-solve unaweza kuharibu ndoa...so (kimyaaa)..sijui solution yake kwakweli...
 
Hivi kuna nini kati ya hawa wawili, hakina mama wangekuwa wanaelewa kuwa H/G anaweza kukupikia chakula pamoja na uchafu wowote anaotaka kukuwekea, na ukaja unakula bila ya kujua, wangekuwa wanawaeshimu
 
Wewe unaona ukimrudisha kwao umemsaidia nini, kwa nini aliyempa mimba asipatikane akaozeshwa?

Kama ni baba mwenye mji (mme wa huyo mama) anahusika aozeshwe
..Kaitaba taratibu eh!? Hivi ukikuta aliyempa mimba ni mumeo (kama wewe kaitaba ni mwanamke) utakubali amuoe huyo binti na hatimaye kuwa mke mwenza mwenzio??
 
Unakwenda kijijini unakuta familia masikini sana, hawana hata uwezo wa kupata mlo mmoja kutwa, kuwaonea huruma unachukua binti yao hadi kwako mjini akufanyie kazi za ndani, apate pesa awasaidie wazazi wake

Binti akiwa kwako anapata ujauzito, bila kujali ameupata wapi, wewe unamludisha kwao,

-Je! huu ni uungwana?
-Hauoni kuwa unaiongezea familia umasikini na mzigo wa kulea mimba na hatimaye mjukuu?
-hakuna njia nyingine ya kumsaidia huyu binti zaidi ya kumrudisha kwao?
-Je ukikuta mimba hiyo ni ya mwanao wa kiume? na wakati huo umeisha mrudisha kwao!

kweli wabongo wengi hapa wanafuliaga sana! tubadilikeni!
 
hili sakata la kumrudisha ni sawa tu kwanini hajajitunza ? mie naboreka tu na kimshahara tunachowalipa wasichana wa kazi hiyo 15,000 au 20,000.00 hawawezi hata kujifanyia mahitaji yao binafsi
imagine mtu unaenda saloon unatumia more than 20,000.00 kwa siku moja harafu huyu binti kwa mwezi unampata 20,000.00

?
 
Sasa bibie kama unaboreka na hiyo hali umechukua hatua gani? umemwongezea au?
 
Unakwenda kijijini unakuta familia masikini sana, hawana hata uwezo wa kupata mlo mmoja kutwa, kuwaonea huruma unachukua binti yao hadi kwako mjini akufanyie kazi za ndani, apate pesa awasaidie wazazi wake

Binti akiwa kwako anapata ujauzito, bila kujali ameupata wapi, wewe unamludisha kwao,

-Je! huu ni uungwana?
-Hauoni kuwa unaiongezea familia umasikini na mzigo wa kulea mimba na hatimaye mjukuu?
-hakuna njia nyingine ya kumsaidia huyu binti zaidi ya kumrudisha kwao?
-Je ukikuta mimba hiyo ni ya mwanao wa kiume? na wakati huo umeisha mrudisha kwao!

ukarimu nao huponza. Kama kaitoa huko mashenzini analo. Hakushikwa miguu huyo, ila kama ni mwanangu sina jinsi
 
..Kaitaba taratibu eh!? Hivi ukikuta aliyempa mimba ni mumeo (kama wewe kaitaba ni mwanamke) utakubali amuoe huyo binti na hatimaye kuwa mke mwenza mwenzio??
Wewe una maoni gani?
 
Back
Top Bottom