Katika hili waziri wa michezo (Ndumbaru) amekosea, ni hatari, mamlaka zirekebishe mapema

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Waziri mwenye dhamana ya michezo wa Tanzania, Ndumbaru, siku ya leo amesikika akipiga marufuku watanzania wenye ushabiki (watakao vaa jezi) wa vilabu vya nje vinavyokuja kushindana na timu za Tanzania (Simba na Yanga) kuonekana uwanjani.

Kwa hakika hii sio kauli ya kiungwana kwenye soka, na ina mlengo wa kupandikiza chuki, ubaguzi na fujo michezoni, kitu ambacho kinapigwa vita mnoo na FIFA.

Mamlaka za juu za nchi (waziri mkuu, makamu wa Rais na Rais) tunawaomba sana mjitokeze haraka mnoo kufuta kauli ya Ndumbaru ili kulinda Amani na mshikamano michezoni.
 
Vaa jezi ya timu yako ya hapa nchini. Hutaki nenda na hati ya kusafiria uliyokuja nayo kutoka kwenye nchi timu yako ilipo toka.
 
Ingekua Taifa Stars sawa,ila Waziri kutoa kauli kama hizo kwa klabu za Simba na Yanga ni kuingilia kwanza utani wa jadi wa Simba na Yanga, ipo hivyo tangu mwanzo.

Yanga iliungana na wapigania uhuru kudai uhuru na hata kutetea haki za watu weusi,Simba iliungana na wakoloni kugandamiza haki za watu weusi ikiwemo kwenye siasa na hata kwenye mfumo wa ligi enzi hizo.

Utani wa Simba na Yanga kutoafikiana kwa jambo la kila mwenzie ndio umezaa Derby kubwa Afrika Mashariki,kati na ukanda wa Maziwa.

Uhasama/ utani wa Simba na Yanga ndio unaifanya Kariakoo Derby kua kwenye top 5 derby barani Afrika. Mashabiki waache wakashangilie wanachokitaka,ni haki yao,hawavunji katiba/ sheria.

Yanga wakienda uwanjani na wakaishangilia Al Ahly dhidi ya Simba ni sawa ni sahihi.

Simba wakija uwanjani wamevaa jezi za Mamelod na kuwashangilia Mamelod Sundowns ni sawa,hawavunji sheria Kamsikilize vizuri Waziri.

Hakuna Ulimwengu wowote klabu zikacheza haalfu kukatolewa matamko kua wasio klabu hiyo wanalazimishwa waiunge mkono klabu wasiyoipenda.

Haiwezekani ukakuta Madrid wakalazmishwa wawaunge mkono Barcelona, Arsenal wakalazimishwa dhidi ya Chelsea, Ac Milan dhidi ya Inter Milan.

Mawazo ya Waziri ni ya kipuuzi, mpira usiingiliwe na siasa, wao watangaze hamasa ya kununua magoli inatosha!

Kiukweli kauli yake kimichezo ni fedhehea na upumbavu tu kimataifa!

Waziri Ndumbaro akemewe!!

Maybe wengi wamemsahau Ndumbaro kiasi, akiwa waziri wa sheria na Katiba alitoa tamko kua Watanzania kwa sasa hapana kupewa katiba mpya, bali serikali itafanya mpango katiba iliyopo ifundishwe kwa Watanzania wote kwa miaka mitatu mfululizo kwa kila mtanzania ili waielewe!!

Sijui alitaka kila mtanzania awe na degree ya Katiba ya zamani, stupid as stupid does
 
Watanzania ni kichwa cha mwendawazimu, watu wakifanya hayo mnaongea ikichukuliwa hatua mnaongea, hamjui nini mnataka.
 
Hii ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwani Polisi wa huko Barcelona wanang'oa plate number za 3D?

kwani huko timu zao zilishiriki kuleta uhuru ?

Hapa hawataki jezi za huko na ukijichanganya shauri yako
 
hajui kuna raia wa nchi hizo wapo hapa nchini kwa shughuli mbalimbali wanapenda kuona timu zao zikija huku wazishangilie, wanakiuka HAKI ZA KIBINADAMU. Haki ya faragha.....kumchagulia mtu mzima cha kufanya...uzalendo haulazimishwi...mtu mzima hushauriwa tu...uamuzi anao mwenyewe
 
Watanzania ni kichwa cha mwendawazimu, watu wakifanya hayo mnaongea ikichukuliwa hatua mnaongea, hamjui nini mnataka.
Rekebisha kauli yako.
Watanzania sio kichwa cha mwendawazimu, bali timu ya soka ya taifa la Tanzania ndio kichwa cha mwendawazimu.
 
Back
Top Bottom