Ingekua Taifa Stars sawa,ila Waziri kutoa kauli kama hizo kwa klabu za Simba na Yanga ni kuingilia kwanza utani wa jadi wa Simba na Yanga, ipo hivyo tangu mwanzo.
Yanga iliungana na wapigania uhuru kudai uhuru na hata kutetea haki za watu weusi,Simba iliungana na wakoloni kugandamiza haki za watu weusi ikiwemo kwenye siasa na hata kwenye mfumo wa ligi enzi hizo.
Utani wa Simba na Yanga kutoafikiana kwa jambo la kila mwenzie ndio umezaa Derby kubwa Afrika Mashariki,kati na ukanda wa Maziwa.
Uhasama/ utani wa Simba na Yanga ndio unaifanya Kariakoo Derby kua kwenye top 5 derby barani Afrika. Mashabiki waache wakashangilie wanachokitaka,ni haki yao,hawavunji katiba/ sheria.
Yanga wakienda uwanjani na wakaishangilia Al Ahly dhidi ya Simba ni sawa ni sahihi.
Simba wakija uwanjani wamevaa jezi za Mamelod na kuwashangilia Mamelod Sundowns ni sawa,hawavunji sheria Kamsikilize vizuri Waziri.
Hakuna Ulimwengu wowote klabu zikacheza haalfu kukatolewa matamko kua wasio klabu hiyo wanalazimishwa waiunge mkono klabu wasiyoipenda.
Haiwezekani ukakuta Madrid wakalazmishwa wawaunge mkono Barcelona, Arsenal wakalazimishwa dhidi ya Chelsea, Ac Milan dhidi ya Inter Milan.
Mawazo ya Waziri ni ya kipuuzi, mpira usiingiliwe na siasa, wao watangaze hamasa ya kununua magoli inatosha!
Kiukweli kauli yake kimichezo ni fedhehea na upumbavu tu kimataifa!
Waziri Ndumbaro akemewe!!
Maybe wengi wamemsahau Ndumbaro kiasi, akiwa waziri wa sheria na Katiba alitoa tamko kua Watanzania kwa sasa hapana kupewa katiba mpya, bali serikali itafanya mpango katiba iliyopo ifundishwe kwa Watanzania wote kwa miaka mitatu mfululizo kwa kila mtanzania ili waielewe!!
Sijui alitaka kila mtanzania awe na degree ya Katiba ya zamani, stupid as stupid does