KERO Katika kijiji cha Bonye tarafa ya Bwakila chini, Duthumi Morogoro vijijini wakulima tunasumbuliwa sana na mfugaji aitwae Lembile Sangara a.k.a DC

KERO Katika kijiji cha Bonye tarafa ya Bwakila chini, Duthumi Morogoro vijijini wakulima tunasumbuliwa sana na mfugaji aitwae Lembile Sangara a.k.a DC

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Hapa kijijini kuna mfugaji yupo juu ya sheria na kijiji kinaonekana kimeshindwa kumdhibiti, sheria ya kijiji cha bonye inamtaka kila mmiliki wa ng’ombe asizidishe ng’ombe zaidi ya 10 , jambo la kushangaza huyu Lembile anaweka hadi ngombe zaidi ya 200 kwa msukuma mmoja.

Na kijiji hakimchukulii hatua yeyote, hata askari wa kituo wanamwita huyu Lembile Boss, bwana shamba wa kijiji pia ni rafiki mkubwa wa Lembile kiasi hawezi kufanya tathmini bila ya kupata ho ahead kutoka kwa Lembile, jambo hili linapelekea kuandikwa kwa tathmini za chini ya makadirio.

Tunaomba serikali iingilie kati swala hili kwakuwa chanzo kikubwa cha mihogoro hapa kijijini ni huyu Masai Lembile na mifugo yake.
 
Mkuuay pole Kwa kuwa na roho mbaya ya kwanini,yaani nyie ndiyo hasara ya taifa kwahiyo unatakaje
 
Back
Top Bottom