Inasikitisha sana
Katika miaka ya 1990, kulikuwa na picha iliyosambaa sana ya tai aliyekuwa akisubiri msichana mdogo aliyekuwa na njaa kufa ili aweze kula maiti yake. Picha hiyo ilipigwa wakati wa njaa ya mwaka 1993/94 nchini Sudan, na mpiga picha kutoka Afrika Kusini aitwaye Kevin Carter, ambaye baadaye alishinda Tuzo ya Pulitzer kwa ‘picha hiyo ya kuhuzunisha 😓.
Hata hivyo, wakati Kevin Carter alikuwa anafurahia mafanikio yake na kusherehekewa kwenye vyombo vikubwa vya habari duniani kwa ‘uwezo wake wa kipekee wa upigaji picha’, aliishi kwa miezi michache tu baada ya hapo kabla ya kuangukia kwenye msongo wa mawazo na hatimaye kujiua!
Msongo wake wa mawazo ulianza wakati wa mahojiano na moja ya chombo cha habari (kupitia simu), mtangazaji mmoja alipompigia na kumuuliza nini kilimtokea yule msichana mdogo, Kevin alijibu tu, “Sikusubiri kujua kilichompata baada ya kupiga picha, nilikuwa nawahi ndege…” Kisha yule mpigaji simu akasema, “Nakwambia ukweli kwamba kulikuwa na tai wawili siku hiyo, mmoja alikuwa na kamera.
Kauli hiyo ilimsumbua sana Kevin Carter, na mawazo hayo yakampelekea msongo wa kudumu hadi akajiua. Kevin Carter angeweza kuwa hai leo na hata maarufu zaidi, kama tu angemchukua yule msichana na kumpeleka katika Kituo cha Chakula cha Umoja wa Mataifa, ambacho ndicho msichana huyo alikuwa akijaribu kufikia au hata kumpeleka tu mahali salama.
Leo hii, kwa masikitiko makubwa, mambo haya yanaendelea kote duniani. Dunia inasherehekea upumbavu na vitendo visivyo vya kibinadamu kwa gharama ya mateso ya wengine.
Kevin Carter alipaswa kumchukua yule msichana kutoka pale, jambo ambalo halingemgharimu chochote lakini hakufanya hivyo, alikuwa na muda wa kutosha kupiga picha, lakini hakuwa na muda wa kuokoa maisha ya mtoto huyo.
Hivyo basi, tunapaswa kuelewa kuwa lengo la maisha pia ni kugusa maisha ya wengine.
Katika kila jambo tunalofanya, utu na ubinadamu viwe mbele kabla ya kile tunachotaka kufaidika nacho. Katika kila tendo letu, tuwafikirie wengine na namna tunavyoweza kuwa msaada kwao, huo ndio ubinadamu wa kweli.
C&p