round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 345
- 1,145
Ni mchezo uliojaa wachezaji wengi Wamarekani weusi na waafrika waliobadili maisha yao kwa mishahara inayoenda mpaka bilioni 3 kwa wiki
Huwa ni vijana warefu wenye miili ya mazoezi, wanatupia pamba za bei, mkwanja upo wa kutosha, Ni ngumu kuambiwa NO wakitupa ndoano
Lakini kuna mchezo mchafu unaendelea kwa wanawake wanaoolewa kuzifanya ndoa ziwe kitega uchumi cha kuja kutumia jasho la wachezaji hao kuwatajirisha,
Wachezaji wengi wanapokuwa bado wanacheza wake zao wanapata umaarufu, tunaweza kusema wanajitengenezea Brand, wachezaji wakistaafu media haziwapi attention vile vile kwa wake zao, kinachofuata ni wanawake kuanza kutengeneza visingizio vyovyote ili ndoa ivunjike.
Mahakamani mabilioni ya mchezaji waliyovujia jasho yanaganwanywa, Maisha ya wanawake wengi sana yanabadilika kwa mtindo huu wa kitapeli