homeland12
Member
- Aug 17, 2022
- 58
- 97
Either.... Or
Akifa si anakufa tu mkuu, utamzuia mtu kufa?Akifa?
BL mbna unaanza kuogopesha jamani Dear, LolMimi kwenye urafiki ukishaingiza mambo ya pesa, nakupotezea. Maana ya urafiki si lazima akusaidie kipesa. Hata mawazo, kukushauri pale anapoona huendi sawa. Mambo ya pesa ndiyo maana kuna Taasisi za kukopesha. Acheni kubebesha watu mizigo isiyo yao.
HahahaDuh ww inabid usupport no reform no election kwa nguvu zote.
Sahihi kbsa mkuuKwa upande wangu na zama tulizopo marafiki wawepo ila ikitokea shida hasa ya kipesa ni bora uwe na ndugu wa karibu mliyeshibana ambaye anaweza akakusaidia na huyo anaweza akakufichia siri kuliko hao marafiki ambao wengi tumejaa unafiki.
Bantu Lady wewe unakuwaga serious kwa kila kitu😅Mimi kwenye urafiki ukishaingiza mambo ya pesa, nakupotezea. Maana ya urafiki si lazima akusaidie kipesa. Hata mawazo, kukushauri pale anapoona huendi sawa. Mambo ya pesa ndiyo maana kuna Taasisi za kukopesha. Acheni kubebesha watu mizigo isiyo yao.
Una roho nzuri Sana we jamaa,mi ningemtimua siku hiyo hiyo baada ya kuona risitiKujenga urafiki inahitaji akili sana siyo kila urafiki unaingia kichwa kichwa. Hoja ya msingi tupambane tuwe na uchumi imara. Huwezi kuwa na mtu wa kukupa hiyo 10k kama uchumi wako hakuna siku na ww utatakiwa umsaidie na usiweze kumpa. Maisha ni give and take au two way traffick. Lakini pia lazima ujue, kuna kipindi uko vizuri utapata marafiki wengi na hata ukashindwa kujua rafiki wa kweli kwa sababu wanahitaji kupokea toka kwako. Ila meza ikipinduka ukawa huna kitu hao hao uliokuwa unawahangaikia ndio wa kwanza kukukimbia. Imeshawahi kunitokea kuna watu walikuwa close friends lakini by that time wao ndo walikuwa wanafaidika na urafiki. Baadaye Pakatokea changamoto kwa miaka michache, nilihitaji sana msaada wao wote walisepa wakabaki wachache sana. Nikamshukuru Mungu kujua kwamba hao wawili au watatu waliobaki ndio marafiki zangu. Tunapeana support mtu anajitoa hata laki 5 na hadai, mwingine hata milioni. Ila na wao wanajua mm nikiwa poa huwa nawatoa
Kuna mwamba wakati flani hakuwa na geto la kupanga, vile mimi nina space nikamkaribisha. Akawa anaishi bure simdai hata mia. simdai hela ya umeme wala maji. na ni mwajiriwa anapokea mshahara, alikaa kwa takriban mwaka. Kipindi hicho mrs wangu yupo masomoni mkoa mwingine pamoja na watoto. siku moja mrs akaniambia amekwama hana kitu kabisa. na mm nikijiangalia sina kitu. nikamwomba jamaa anisevu 50k nimtumie wife, jamaa kachomoa akasema yeye hana kitu kabisa. Nikasema poa, nikatafuta msaada pengine. Siku hiyo hiyo mwamba akatoka kwangu, akaenda kwenye appointment na demu wake mchepuko (maana mrs wa jamaa naye yupo mkoa mwingine). Akaenda benk akatoa laki wakaenda kuspend. akarudi usiku sana nikamfungulia. asubuhi akawahi kutoka kwenda job. akasahau funguo wa ofisi. Nikiwa najiandaa kutoka akanipigia amesahau funguo zake nimchukulie. Nikazama room kwake kucheeki kwenye mfuko wa suruali nakuta risiti ya atm,kuicheki inaonyesha jana yake alitoa laki moja, salio 3m. niliumia sana. Nikasema huyu lazima nimfanyie research. Jioni tulivyorudi kuna mida akaacha simu chaji akaenda kununua vocha gengeni. nikazama fasta kwenye simu yake kucheki sms inbox. nikakuta za jana yake wanapangana appointment na huyo mchepuko. Nikachukua namba ya huyo mchepuko kutaka kumfahamu tuu nikaja kumjua. Nilinyamaza na hilo jambo nikaja kumlipua baadaye sana ameshaondoka kwangu baada ya yeye kunilalamikia kwamba siku hizi simjai. Pumbafu zake hadi leo tunaishi kinafiki tuu.
Jamani 😅😅😅😅 hujanikuta tu kwenye anga zangu, nakuwa cool tu Raymanu KEBantu Lady wewe unakuwaga serious kwa kila kitu😅
Basi mimi ndgu ndio nina mazoea nao kwenye hela.Mimi sitaki kabisa kusikia kuhusu ndugu, ndugu ni nyoka.
Mimi marafiki ndy nimefanya ni ndugu zangu.
Marafiki haô nao ninaishi nao makini sana kwa mipaka ya haki ya juu.
Na mpaka mojawapo ni mazoea kwenye HELA sitaki.
Kwanini kila siku kuwaza kusaidiwana hao marafiki tuu? Wewe hao marafiki wakikwama unauwezo wa kuwasaidia hizo hela? Kama wewe huna huo uwezo na wewe hufai kuwa rafiki yao.Kama Hawa ndio washikaji zako , Kama ndio Hawa ndo marafiki zako ,
Ikitokea umekwama una shida unahitaji either buku tano au kumi either ni urgently au sio urgently sasa katika marafiki zako wa karibu ukakosa wa kukupiga tafu ..
Aisee jitafakari sana uhusiano wako na marafiki wanaokuzunguka
Hapa ULIFANYA jambo la maana kama yupo bongo huu ni mtaji kabisa japo mambo Huwa yanafeli.Jana kuna dogo kalia hali nimempiga na milioni.
Hapo kwenye buku 5 au 10 ondoa buku weka milioni.
Hela ya bongo haina thamani.
Na hayo hayo ndo yamefanya aombeKwanini uombe buku 5 buku 10? Huoni kama wewe ndo una matatizo?
Ukiwa na huu ukauzu utagombana na watu wengi sana hapa Tanzania cha msingi km huna tumia maneno ya busara kumuaminisha kuwa huna hela vinginevyo utaonekana mbaya sanaNiligombana na mwalimu mwenzangu kisa ni kuwa yeye alikuwa na ukaribu na Mimi, lakini hoja yake ni kuwa siku akikwama nimsaidie,nilimwambia ni aibu kwa mwanamume mwenye mke na watoto kuishi kwa kutegemea fadhiri za mwanamume mwenzie.
Siwezi fanya ujinga huo, matatizo yangu ya kifedha nitayatatua mwenyewe na mshahara wangu,full stop.