Katika Picha: Maandamano ya wanahabari Leo

Status
Not open for further replies.
Hao walioko madarakani wanapaswa kutambua kuwa Watanzania wanaweza kuishi bila CHAMA CHA MAPINDUZI lakini hawawezi kuishi bila ya VYOMBO VYA HABARI! Ukweli unaouma kiasi gani huu????

BILA shaka alichokuwa akikizungumza mkuu ni kwamba kama Jukwaa la Wahariri lina viongozi ambao sio watu wa serikali .....yeye na serikali yake hawalikubali.

Mchezo huu wa kutaka kila taasisi ya kijamii kuanzia vijana, wanawake, wazee,walimu wanafunzi na wafanyakazi na kadhalika yaongozwe na watu wanaochaguliwa na serikali ndio umeifikisha nchi hii ambapo leo tuna GDP per capita ndogo kuliko Rwanda na Burundi!!!!

Hawakuishia tu hapo wameingilia mpaka kwenye dini ya Kiislamu lakini wakaogopa dini na madhehebu ya wenyewe wakiogopa Vatican, Ismailiya na Mabohora! Matokeo yake leo tunayaona kwa Waislamu kukosa uongozi wa kweli unaowezz kuunganisha waumini ili kuirahisishia serikali kazi ya utawala.

Na mjumbe wa waziri anatuambia kwamba hakuna ambacho Awamu ya Nne imejifunza toka nchi hii ipate uhuru miaka 47 iliyopita. Mtoto wa Uhuru hana alilojifunza toka makosa ya wale waliopigania uhuru. Tunakwenda wapi jamani? Nyuma au mbele?

Unajua ukiwa kwenye shirika au serikali kwa muda huwezi hata kujua kama ndio inakata roho au vipi!!! Lakini dalili zipo wewe kaa macho wazi, masikio zibua na pua zifanyie mazoezi ya kunusa harufu za jasho, ubabaishaji na uvundo wa kila aina na utagundua nini lijalo baada ya Wazee wa EAC, migomo ya walimu na wanafunzi kwa sababu dira imeharibika....... na chombo ...... pamoja na makidai yote kinakwenda ARIIIIIJOOOOOJOOOO!
 

Kaka FM

Nashukuru kwa kujibu yote even those post ambazo sijazikopy hapa,

Wakati mwingine ni vigumu kuelewa taaluma za watu wengine, hivyo waandishi wa habari wana kazi nzito ya kufilter, kupima na kuweka habari rahisi ambazo sisi wasomaji hatutapata wakati mgumu kuzielewa. This is not easy I guess. I asked one of my professor that, why research yake ni ngumu lakini ametumia lugha rahisi kiasi ambacho kila mtu anaweza akaelewa! akasema to write simplified things is not easy.

Kumbukeni tunaishi katika society ambayo wengi hawajaelimika bado, tusijidanganye DSM, still kuandika habari fulani ambayo mtu wa level fulani hataelewa lakini mwingine akaelewa ni kazi sana. So YES, challenge mnayo hasa katika eneo la habari gani iandikwe ipi isiandikwe. Narudia kwa mwanamapinduzi wetu Kubenea awe careful hata kama Mwanahalisi itafunguliwa kesho, maana anatafutwa. Any mistake or issue like this tunaumia sisi wasomaji-na uandikwaji wa habari za kifisadi unakoma!. Akiweka 'kitu' kiwe heavy kiasi ambacho, ikitokea maandamano kama haya wasiandamane wahariri tu BALI WANANCHI WOTE!


waberoya
 
QN: What is your take in this issue? Is Kibanda wrong saying Kubenea's news was not right/proper or whatever?

Thanks bro.

waberoya


Waberoya, Ngoja nitumie jibu langu kwako kuelezea mambo fulani ambayo yawezekana kwa watu wengine yanawachanganya kidogo. Kuna mambo karibu matatu ambayo yameingiliana kama nyuzi za mpira wa chandimu.

a. Haki ya Maoni na Habari
Katiba yetu inapozungumzia Uhuru wa Maoni inasema hivi



Kauli hiyo imetanguliwa na maneno "bila ya kuathiri sheria za nchi". Lakini ukiangalia utaona kuwa Katiba inatambua kuwa "kila Mtu" ina maana ya kuwa "Kubenea", "Mwanahalisi", mimi na wewe tunayo haki ya "kuwa na maoni yoyote" n.k n.k Lakini utaona kuwa Katiba haisemi kuwa haki hiyo ya kuwa na kutoa maoni inahusisha maoni ya kweli, ya uongo, yanayofurahisha au yanayochukiza. Inasema tu kuwa "maoni yoyote".

Lakini la pili ni kuwa kila rai naye ana haki ya kupwa "taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani" n.k Lakini kama haki ya kuwa na maoni Katiba haisema taarifa hizo ziwe za aina gani bali wananchi wana haki ya kupewa taarifa hizo.

Kwangu hilo ni la msingi mno kwa sababu ninayo haki ya kutoa maoni na wananchi wana haki ya kupata maoni yangu yawe mazuri, ya kuchekesha, ya kukera, ya kufurahisha or whatever have you.

b. Maoni yana Mipaka
Kisheria (ndipo kile cha "bila kuathiri sheria") kuna vitu ambavyo mtu hawezi kufanya akisingizia ni uhuru wa maoni au uhuru wa kutoa taarifa. Ndipo hapo sasa tunasheria zinazohusu Libel na defamation. Hili ni jambo la muhimu. Gazeti likiandika habari za mtu na kudai kuwa mtu fulani yuko hivi au vile na sifa au maelezo hayo kuonekana yanamchafua mtu mbele ya jamii au kumharibisa sifa na staha yake basi mtu yule anachofanya ni kwenda Mahakamani kwa kufuata sheria zetu na kufungua kesi ya Libel au defamation.

Hivyo ndivyo alivyofanya Dr. Salim Ahmed Salim dhidi ya gazeti la Nation la Kenya na kushinda mamilioni ya shilingi baada ya gazeti hilo kumzushia habari isiyokuwa ya kweli. Katika hili serikali haiingilii kati na kulifungia gazeti bali gazeti linaadhibiwa kisheria na linafanya masahihisho kama lazima n.k

c. Uwezo wa Kulifungia gazeti
Kitu ambacho watu hawaoni ni kiini hasa cha maandamano haya siyo habari iliyoandikwa kwani hiyo ingeweza kuamuliwa na mahakama na kama watu wamechukizwa au wanaona wamechafuliwa jina wanaenda mahakamani na kufungua kesi ya madai n.k Kiini cha mgogoro huu ni uwezo wa Waziri kulifungia gazeti lolote kwa sababu yeyote ile inayomridhisha yeye na uamuzi wake huo hauwezi kupitiwa na mahakama yoyote ile.

Kwa maneno mengine, kama Waziri akiona bosi wake (Rais) ameandikwa vibaya na ya kwamba "amedhalilishwa" au kwa namna yoyote ile au akiamini habari fulani ni ya kukera basi anaweza kulifungia gazeti bila hata ya kutoa sababu alimradi ametangaza kwenye gazeti la serikali. Watu wengi hawajui tu ni kuwa hadi hivi sasa kuna majarida na magazeti karibu 20 ambayo yamefungiwa kwa amri ya Waziri tu. Mengine yametoka mara moja na kufutwa.

Kiini cha hilo ni sheria ya magazeti ya 1976 na sheria ya Madaraka ya Rais wakati wa Hatari ya 1986. Sheria zote hizo mbili ndio tishio kubwa zaidi la uhuru wa habari nchini kuliko kitu kingine chochote. Hivyo waandishi na watu wengine wanapoandamana kupinga siyo wanaunga mkono kilichoandika kwani kama ni kizuri, kiibaya au cha kizushi kingeweza kuamuliwa kwa urahisi tu na mahakama bali ni ule uwezo wa Waziri kuwa mtawala wa Kiimla katika sekta ya habari na watu wote kufanya kazi kwa huruma yake.

Usichokijua ni kuwa baada ya makala ya Kubenea mimi niliandika ile makala ya "Usisomea makala hii inaweza kuwa ya Kichochezi" kwenye Tanzania Daima. Ofisi ya Maelezo waliwaita wahariri wa Tanzania Daima na kuwapa onyo kuwa makala yangu imerudia kile kilichoandikwa kwenye MwanaHalisi tena kwa maneno yale yale na kwanini gazeti hilo nalo lisichukuliwe hatua kali.

Uzuri ni kuwa makala yangu ilitoa onyo mapema kabisa kuwa kama mtu hataki kusoma habari za kichochezi asiendelee na pia iligawanywa mara mbili na hivyo kuwapa muda wa kufuatilia mtiririko wa hoja na hatimaye kuelewa kuwa hawakuwa na msingi wa kuliadhibu Tanzania Daima.

Hivyo waandishi wanachopinga ni kufungiwa kwa gazeti la MwanaHalisi kwa kutumia sheria za kidikteta kama hizo ambazo hazimpi mtu uwewzo wa kuzichallenge in courts. Ndio maana binafsi napenda njia ya defiance zaidi (kama wazee wetu leo) kuliko hii ya kuwabembeleza. Ningefurahi kuona MwanaHalisi wanachapisha gazeti hilo hilo tena na kukaidi agizo la Waziri. Mtu huru hatakiwi kutii sheria ya kidhalimu kwani kwa kufanya hivyo anakubali udhalimu huo.
 
...Ningefurahi kuona MwanaHalisi wanachapisha gazeti hilo hilo tena na kukaidi agizo la Waziri. Mtu huru hatakiwi kutii sheria ya kidhalimu kwani kwa kufanya hivyo anakubali udhalimu huo.
Weee! Labda lichapishwe na mhariri na Mkurugenzi wake watoweke Bongo, vinginevyo....!
 


Mkuu this is received,noted and understood by me.Thanks

Hiyo njia ya wazee is my best way, and is most recommended by me in TZ.


waberoya
 
Je kuna tamko lolote lililotolewa na Reginald Mengi?
 

Mama,

Una ujasiri mkubwa sana wakati kama huu kusema Waandishi na Kubenea wao wamechemka. Watu wote wamepanda kwenye bandwagon la Waandishi. Kisa, wanatetea waandishi kwa sababu magazeti yanaanika ufisadi. Kwa hiyo chochote watakachofanya waandishi basi lazima wasapotiwe hata wakivurunda. Mimi nina admire the galls ulizokuwa nazo kwenda kinyume na upepo kumbakumba wa hapa.

Waandishi wamechemka.

Hebu nambie. Jana walipoandamana, walisikika wakisema hawatetei kwamba habari ya Kubenea ni sahihi. Wanasema hata kama habari sio sahihi kufungia gazeti ni kuminya demokrasia. Wanasema hata kama habari sio sahihi ilibidi Ridhiwani ndio akashitaki, au Waziri akashitaki, sio ajiamulie. Sasa huku ni kutokuelewa hata kinachoendelea ni nini hapa.

Mkuchika kasema habari ni ya uongo, halafu ni ya kichochezi.

Tunaweza tukabishana nini ni uongo na tukadaiana vidhibiti. Lakini ku interpret nini ndio au sio uchochezi hiyo ni absolute discretion ya Waziri. Hivyo ndivyo lile li sheria la 1976 linavyosema. Mtukane Mkuchika, itukane sheria unavyotaka, lakini, Wamarekani wanasema, it is what it is!

Sasa, ukishakubali kwamba habari haikuwa sahihi, inabidi umwachie Mkuchika full and absolute discretion ya kuitafsiri na kuamua cha kufanya. Yeye kasema ule uongo una amount to uchochezi. Na ukishakubali huu ni uongo then sheria haisema Ridhiwani Kikwete na Mkuchika waende mahakamani kudai ukweli. Inasema Waziri atajiamulia kivyake. Mwenyewe. Kwamba ni uchochezi au la. As draconian and undemocratic such system may be, again, it is what it is.

Wanatakiwa waseme sheria ndio mbovu. Kusema Kikwete abadilishe Waziri ni kichekesho cha Abunuasi kwa sababu kesho akiondolewa Mkuchika akawekwa Mkuhani na sheria bado ni zile zile waandishi watakuwa mashakani bado. Mkuchika anatakiwa ku apply the law, kama alivyofanya hapa, kutafsiri kivyake. Sio kwenda mahakamani. Wao hilo hawalielewi masikini. Wao, wapasha habari, ndio ambao hawana habari ya nini kinaendelea. Inasikitisha!!

Na kuhusu kumgomea Waziri, huu ndio ukilaza mwingine. Magazeti yalivyo cover haya maandamano yanakwepa kusema "Mkuchika." Ni kituko kilioje. Hili lilikuwa ni tukio la kihistoria. Miaka 10, 20, 50 ijayo watu wa generation za wakati huo watakaposoma archives za gazeti la leo, October 29, 2008, ungetegemea waone - na wanastahili wapate - rekodi kamili ya nini kilijiri leo. Kwa nini Wahiriri waliandama ? Nani alifungia gazeti ? Kwa nini, aliyelifungia alisema nini ? What was his relation to the media prior to such development ? Na kabla hajawa Waziri background yake ni nini huyu Waziri ? Alipoulizwa na vyombo vya habari baada ya kufungia gazeti alisema ame intepret vipi kwamba huu ni uchochezi ? What was he thinking ? Rekodi yake ya uendeshaji wizara zaidi ya hili sakata ikoje, ana controversy nyingine ?

Huwezi uka cover hili tukio bila kuchambua baadhi ya masuala hayo. Hawa sio waandishi hawa. Ni lazima tuanze kujenga institutions za press Tanzania. Hata chache tu. Hata moja.
 



Supported., ila MKJJ hafurahii kuwasema waandishi wote, ni Kubenea tu kachemsha!

waberoya
 
Mwanahalisi kafanya makosa kwa kuandika habari zisizo na evidence halafu asiadhibiwe, waandishi cum wahariri wanakubali; to the contrary baadhi yao waandamane kupinga kwa nini gazeti lifungiwe!

Mwanahalisi hakufanya kosa lolote, kama vile ambavyo JF hatukufdanya kosa lolote tulipofungiwa, hapa mwenye makosa ni wewe ambaye huonekani kuielewa serikali yetu inavyo-operate, na huenda ukawa wala sio raia kama sisi maana haiwezekani ukashindwa kuielewa seirkali yetu kwamba ina tabia za kufungia anythingng bila sababu, Mwanahalis hana makosa mwenye maksoa hufungwa sio kufungiwa!

Yule muandishi mzee aliyecheza na Hosea alitoka jela majuzi hukumuona hapa JF, ukiikosea serikali inakufunga huwa haifungii, muulize Rage!


Hakuna excuse, ni kuwa waandishi walichemka over the boiling point pale walipoanza na kumfungia Mkuchika kwenye media coverage, na pili kuja kuandamana kisa eti mwanahalisi limefungiwa..tena kwa kosa ambalo liko dhahiri.

Off course hakuna excuse ya kutokuelewa kuwa anayexhemka ni wewe usiyeelewa unachosema, JF tulipofungiwa bila sababu ni hao hao kina Kubenea ndio waliotusimamia, sasa kama wewe umesahau sisi wengine hatujasahau, wao hawakuuliza tulkikosa nini walishambulia serikali kwa kuingilia uhuru wa habari, kwa hiyo taabu kujua anayechemka hapa ni nani kati yako na waandishi mashujaa walioandamana, na sisi baadhi yetu tuko nyuma yao!


Kwanza Tanzania hatuna Global Publishers ndio mana tunakuambia kua Tanzania sio USA liliko hilo gazeti, hapa anayetakiwa kuonywa ni wewe unakurupuka bila kujua unachosema, what are you saying kwamba wewe una akili sana kuliko wahariri wote waliandamana? Is that so? Then how come huna gazeti lako au angalau blog tu tukakuona how perfect you are?

Investigative journalism inafutana na evidence huko USA sio bongo, Muandishi Balinagwe alipoandika nyeti kuhusu serikali kule Mtwara wakati wa Mwinyi, serikali ilimuita na kumdai evidence alipowapa wakamfunga jela miezi sita, sasa inaonekana huna historia ya waandishi wa habari Tanzania, na wala hujui kwamba hata JF serikali iliwahi kutufungia bila sababu na haijaomba radhi mpaka leo, Mkuchika is a joke ndio maana hata magazeti hayamuandiki tena hiyo ni big step ya kumkosesha tembo usingizi, tunapigana na silaha tulizonazo tena kwa mazingara tuliyonayo, Tanzania sio USA mkuu ambako pia Dan Rather pamoja na ushahid wake bado alifukuzwa kazi kwa kuinyoohsea kidole serikali, sasa itakwua bongo? Hata records huna bro za waandishiw a habari na serikali?



Wewe unaonekana una lako jambo, unafikiri unamfool nani na maneno yasiyo kuwa na elimu wala ukweli, bali mapovu tu ya kutaka kuonekana unajua sana kumbe nothing, gazeti gani Tanzania linasomwa kuliko Mwanahalisi una maana wananchi wa bongo ni wajinga ila wewe tu ndiye mwenye akili sana ya kujua kua Mwanahalisi ni waongo? huna hata aibu Kubena hahitaji your approval kufanya kazi yake, kufungiwa kwa gazeti Mwnahalisi kwako ina maana serikali ya Tanzania inayoficha EPA na Richimonduli kuwa ndio wakweli?

Yaani unataka tuiamini serikali inayoficha habari za Dowans, na kwamba Meremeta ni kampuni ya jeshi ndio unataka tuwaamini over gazeti la Mwanahalisi? Unajua wananchi hapa JF mnahitaji kuwa macho sana na huyu ndugu na all his games humu, maana somehow anafikiri sisi wabongo humu ni wajinga kwamba yeye anaijua sana hii serikali kuliko sisi wote, mkuu ni serikali yako unayoiamini ndiyo ina sifa za ku-fool wananchi sio gazeti la Mwanhalisi, mabalozi wanane wa EU hawawezi kwenda kulitembelea gazeti ambalo wanalijua kuwa lina sifa za kuwadnagnaya wananchi, that is pthetic thinking!

Kubenea anazo evidence na kama ni kuzitoa ameshauriwa asirudie makosa ya Balinagwe ya kuwapa serikali evidence na hatimaye kuishia kufungwa jela,



Hapa JF tu panakutoa kamasi kila siku kuhangaika na michezo yaq kitoto toto, sasa hata ungekua mwandishi utamuuzia nani? Credibility utaitoa wapi kama hapa tu JF inakupa taabu? Ni nani hapa aliyekuomba uwe muandishi wahabari? Mbona unapenda kujipa power ambayo huna? And who cares about what you feel kuhusu waandishi wabongo? Na who cares kuhusu your so called fani yako? ni fani gani hiyo? Hujaombwa na mut hapa wala Tanzania, waandishi tulinao wanatosha, kama sio fani yako basi waachei wenye fani, lakini usitishe waandishi na maneno mengi ya hewa no body needs you huko kwenye uandishi, hatujaishiwa kiasi hicho! na no body cares kuhusu fani yako kwa sababu ingekwua fani kweli tungekusikia , usitutishe na maneno hewa bro! Tutawatetea waandihsi mpaka mwisho they are doing the best under very difficult circumstances.


Kukurupuka ni pamoja na kurukia ishu zisizokuhusu ambazo wala huna idea nazo, ni ukweli ulio wazi kua huna uhakika wala huelewi unachoskisema, Tanzania hatujawa USA wala UK, haiwezekani mabalozi wa EU wakapoteza muda wao siku nzima kulitembela gazeti la Mwanahalisi, knowing kwamba halina waandishi wanaojua kazi yao that is pure nonesense thinking,

Kuna critics wanazoweza kuzikubali lakini sio zako mtu ambaye huna clue yoyote na uandishi wa bongo wala uongo wa serikali yetu, labda uombe elimu hapa upewe kwamba serikali yetu haijawahi kusema ukweli on anything, licha tu ya kulisingizia Mwanahalisi, pia walishawahi hata kutusingizia JF pia.



Hapana unalipigania taifa vyema zaidi ukiwa raia wake, maana angalau unakuwa na idea of how linaendeshwa, sasa kama unaamini kuwa serikali yetu siku zote husema ukweli then huoni kuwa kuna tatizo hata na analysis zako kuhusu hili taifa licha ya waandishi tu!


Kutumia majina mengi, na maneno mengi ya hasira na maneno mengi yenye mapovu sio guarantee kwamba unajua unachokisema kwa watu tunaojua mambo mengi ya siasa, na kujua mambo mengi sijawahi kusikia kuwa ni dhambi, tatizo ni usipojua ukajifanya unajua, kwanza tuliambiwa credibility, baadaye tukambiwa dataz ni zauongo, sasa tunajua sana, what a turn of events and ideas yote haya kusudi tukubali tu hoja hewa, yote haya ili tukubali kwa nguvu hoja zisizo na mshiko kwamba serikali yetu inasema sana ukweli kuliko magazeti kama Mwanahlisi, what a joke?

Hatuwezi ku-apologize for what we know, hatukuumbwa sawa na hatukuzaliwa na mzazi mmoja humu JF, huhitaji kujua kila kitu duniani ili kujua kua serikali yetu ni bomu la kutupa, na huhitaji kujua kila kitu dunaini ili kujua kwamba serikali haijawahi kusema ukweli on anything, wivu huanzia kwenye rela life baadaye huhamia kwenye Forum ndio maana hatuna tatizo kuwaelewa na hoja uchwara za kujua dunia, ohh yes we know the world maana tumepita karibu kila nchi sasa tutakuwaje sawa na ambaye hujafika kila nchi dunaini? Eti tunahitaji ku-apologize kwa nini tumesaifri karibu kila nchi duniani? Sasa huo si ndio uswahili wenyewe,

Mnataka tuwaambie wivu na chuki vilipoanzia? Mlidhani hatujui?, tulikuwa tunajua ingawa mlikuwa mnaficha sana kwenye real life uliza wa karibu watawaambia kua tulikua tunajua na hata hapa hatushangai maana binadam hakuumbwa kuishi na wivu somehow ni lazima utatoka tu ama sivyo atakufa kiroho kabla ya siku zake ndo maana baada ya kupata hii nafasi ndio unatoka bila kificho wazii! Hatutishiki maana nyinyi sio wa kwanza kuwa na wivu na chuki, tunayoyajua tunajua kama hamjui ulizeni mtasaidiwa maana sisi tukiwa hatujui huwa tunauliza, lakini kujifanya unajua wakati hujui ,matokeo yake ndio haya kuchulkia watu kwa sababu wanajua usiyoyajua that is low, na kwamba usipojua wewe basi sio kweli what an arrogance, wewe ni nani?

Hvi kwa nini unafikiri kila mahali ni lazima uwe juu tu hata kama hakuna sababu? I mean hapa sio kile chama cha kabila letu hapa ni wabongo toka kila walk of life sasa unahitaji kua na hoja nzito kuwashauri wananchi kuwa una hoja, sio miguvu uchonganishi, hasira wivu, chuki, hakuna mjinga hapa kama wanachama wa kile chama cha kikabila, hapa wote tuna akili timamu, hata kwenye chama ndio maana wengine hukutuona maana tulikushitukia mapema, baada ya kujipa uongozi bila kuchaguliwa na wananchi, sasa mnataka kuhamishia na huku JF, hapana bro huku tumeamuka siku niyngi sana,

Na hatutishiki na mapovu, wala majina 100!
 
uzee unakujia vibaya, nisiandike mengi ya kumaliza kabisaa. Lakini FYI you're totally out of point, mambo ya wivu ni huko chumbani kwako. Tatizo una mambo ya kizamani zamani, kisisiemu sisiemu, kupenda umimi, much know na kuhusudu kuabudiwa. Wa design yako ndio mliotufikisha hapa tulipo kwa kuona akisema mtu ndio kasema. What the heck! To prove you wrong, I am not in the USA.

Hayo ya wivu wewe ndio unayajua kwa sababu ndio uliyeyaleta hapa. Yaelekea unayafanya sana ndio maana unajua details zake. Haya mambo ya kike kike sijui unayapendea nini mzee wewe!

Tena ukome kabisa kuniita bro..........au na wewe nianze kukuita mama au dada ndio maana unakua na mambo ya shakunaku shakunaku. Haya ndio tukuite 'mwanamke kusuta' sio 'mwanaume kujadili'.
 
Unapenda ligi sana wewe. Sio kila mtu mpenda ligi na upashikuna....kuita wenzio wana majina mia, uliwabatiza? au wewe ndio registra hapa unajua nani karegister na jina lipi na yuko wapi.
 
I know I know, Data data, hiyo ndio kazi unayofanya so its your right to have them and know them. That is not my responsibility......responsibility yangu hapa ni kutoa views zangu TAKE THEM OR LEAVE THEM. Kama wewe ndio referee au kocha humu sema ieleweke, sio kupelekapeleka kama unaendesha familia yako, mkeo na wanao if you have them. There might be something wrong with the fuses in your brain....
YOU ARE SO ARRONGANT.
 
yaelekea uizaliwa siku mvua ya radi inanyesha, basi unaona hakuna mwingine kama wewe........ni wewe tu na aendaye opposite na wewe ana chuki na wivu, you should take that out of your mind, blood and brain.

UTAKUWA ULILOGWA NA MCHAWI WAKO ALISHAKUFA.
 
habari ya dowans imetoka wapi hapa wakati inaongelewa SAED KUBENEA, MWANAHALISI NA HAO WAANDISHI WALIOGOMA KUCHEMSHA. Na ndio maana ikaamuliwa kuwe na threads zenye titles. I wonder mtihani wako ulifaulu vipi hasa maswali ya section B.

Kama sio UPASHIKUNA WA HABARI NI NINI, MWANAUME MZIMA .

Hii ni platform for critical analysis, kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake kwa jinsi anavyoona.
 

Kuchemka ni pamoja na kuandika na kujijibu mwenyewe, hapa hatujachemka ila tunakataa chuki na hasira dhidi ya waandihsi wasio na makosa na tunakataa kuburuzwa na mtu anayejigeuza rangi kama kinyonga, we are not fooled! na tutaendelea kuwa tetea waandishiw etu mpaka mwisho, maana si kweli kwamba kiola Mtnaznia ni mchemkaji unelss iwe rnagi yako tu, Dr.
Slaa hafai, Zitto hafai, Mbowe hafai, waandishi hawafai, ila wewe tu na rangi zako ndiye unafaa? as if wote hapa ni wajinga!



Waandishi wanasimamia principles wewe una tatizo binafsi that is the problem hapa, uchanganishi ni kawaida sana maana sasa unajaribu kuandika hata yasiyokuwepo, hoja ya vilaza imeshindwa sasa imegeuka kuwa blah! blah! na kulazimisha anyhting as if wote hapa tumelala, hapana waandishi wamesimamia ukweli na gazeti, la Mwanahalisi kufungiwa kimakosa na serikali isiyoaminika na ukweli hata siku moja!Bado tunasimama na Kubenea na waandishi wote walioandamana jana kuwa tupo nao ukurasa mmoja!

Mkuchika kasema habari ni ya uongo, halafu ni ya kichochezi.

Mkuchika angekua na ukweli CCM ingeshinda Tarime.


hiyo discretion ya waziri ndiyo inaypingwa na waandishi waziri hatakiwi kua na hiyo power, hata huko USA unakokusema ni FCC ambayo mtoto wa Colin Powell alikuwa mkurugenzi wake, ndio wenye power over media sio waziri, wala mkurugenzi. Katika nchi yenye demokrasia waziri hawezi kuwa na hayo madaraka peke yake, na hasa waziri wa CCM!


Wananchi wa Tanzania tumechoshwa na sheria za chama kimoja, maana kama yako ni hoja nzito basi hakuna sababu ya sisi kuwepo hapa JF, si kila kitu bongo kiina sheria na it what it is, sasa haoa tunafanya nini? hoja zingine ni vigumu kuamini mtu alikuwa anafikiri kwamba hapa kuna watu wenye akili kabla ya kuandika ndipo ninaosema hivi mlifikiri hapa tupo wajinga sana!


Waandishi hawana sababu ya kunegotiate na serikali kuhusu ukweli, sheria za chama kimoja ndio matokeo yake haya ya waziri kufanya madudu, ndio maana hata mabalozi wa EU wameshitushwa na kuiuliza seikali ijibu kwamba wamelifungia kwa makosa gani kwa sababu hata wao hawaoni sababu, mahakama tu ndio inatakiwa ku-tafsiri sheria sio waziri hizo ni sheria zilizopitwa na wakati, walipotufungia hapa JF ilikuwa sheria gani? Huko hakuna sheria ila kuna ufisadi ndio tunaoukataa, na tunajua kwua kwenye hii safari hatuko wote, lakini haina maana ya kukubali ufisadi mpaka kwenye magazeti!


Gazeti limefungiwa na serikali kupitia kwa Mkuchika, hata kama asingekwua waziri angekuwepo mwingine, jana waandishi walikuwa vilaza kwa sababu wangeandika kuhusu Mkuchika, hawakuandika sasa wamekuwa vilaza anyways kweli elimu ni mali, ninaonea huruma wasiokuwa nayo maana this is what unaweza kulishwa, gazeti limefungiwa na serikali, generation hiyo haitahitaji anything kutoka kweny kwani hii ya Obama inajali nini kuhusu miaka 45 iliyopita? Wangeajli Obama asingekwua mbele kwa polls, kwa hiyo hata generation ya kwetu ili kuleta mabadiliko hawahitaji archives za hiki kizazi maana wakizifutaa hawatabadili anything, waandishi wameweka msimamo na tunawaheshimu sana kwa hilo, maana angalau wana msimamo!

Huwezi uka cover hili tukio bila kuchambua baadhi ya masuala hayo. Hawa sio waandishi hawa. Ni lazima tuanze kujenga institutions za press Tanzania. Hata chache tu. Hata moja.

Waandishi Tanzania wapo, ila tatizo ni wananchi kuelewa na pia tatizo lingine kubwa kuliko ni wananchi wasioelewa lakini wanafikiri wanaelewa, tunasimama tena kuwapa pongezi waandishi wetu kwa msimamo mzito, huu ni mfano wa kuigwa!

Mabadiliko ni lazima na yanakuja mkuchika na serikali wanachofanya sasa ni delay tactic tu!
 

Mimi sina miaka 60 na akili ya kitoto, ya kuandika na kujijibu, uzee ndio huo mkuu, maneno ya wivu na chuki unayajua vizuri sana ndio maana umeyaanza mimi nimejibu tu, anayependa umimi hutumia majina 100 hapa, sisi ni jina moja tu maana tuna uhakika na tunachosema na tunajaribu siku zote kwua resonsibloe na maneno yetu, hapa mpenda CCM ya Mkuchika na mafisadi ni nani? Hpana wakuu wa majeshi wezi wa Kiwira na Mkapa, ndio waliotufikisha hapa

Hayo ya wivu wewe ndio unayajua kwa sababu ndio uliyeyaleta hapa. Yaelekea unayafanya sana ndio maana unajua details zake. Haya mambo ya kike kike sijui unayapendea nini mzee wewe!

Ya wivu umeyaleta mwenyewe, angalia maneno yako mwenyewe, ungekwua huyafanyi nisingekujua mapema sana, ndio maana nimekuomba uwaulize wa karibu watakuambia maana huwa ni kichekesho sana, mzee ni wewe mwenye miaka 60 mimi sina hata miaka 50 nitakwuaje mzee, mbona unkataa umeri wako na boirthday ulifanmya mwenyewe ukiwa na miaka 50, miaka 10 iliyopita au umesahau?

Tena ukome kabisa kuniita bro..........au na wewe nianze kukuita mama au dada ndio maana unakua na mambo ya shakunaku shakunaku. Haya ndio tukuite mwanamke kusuta sio mwanaume kujadili.

Na wewe ukome kuniita majina ya kizee ambayo ni yako mweyewe kikongwe wewe, meno yenyewe huna ya kubandika halafu unaita watu wazee hapa? Kujiita mama ili iwe nini ndio tukubali hoja hewa? Peleka ukongwe wako huko kizee wewe!
 
your arrogance and speculative behaviour ya kujua wenye majina mia, hebua taja la kwanza, la pili na la tatu...UMEKOSEA STEP, .............ndio siasa zenu za kifisadi kuepnda kujenga maadui na yeyote anayekuja na views against your views. Ndio nyie nyie mafisadi halafu unaleta za kuleta eti UNAPINGA UFISADI. MPINGA UFISADI GANI MNAFIKI unauma na kupuliza at the expense ya kuleta DATAZ! ukome kabisa kuniambia nina majina mengi humu.

Wazee wengine bwana, halafu utalia unafunjiwa heshima!
 


Wewe ndio jizee ...kuishi kwa dhana...dhana... karne ya ishirina na moja hii. Kama umezoea kuabudiwa ni huko nyumbani kwako...wewe kujiita Field Marshal ndio kuhodhi akili ya kila mtu, hodhi ya hao hao lakini si ya wote!

nina wasiwasi hilo ndilo linalokusumbua.
 
Unapenda ligi sana wewe. Sio kila mtu mpenda ligi na upashikuna....kuita wenzio wana majina mia, uliwabatiza? au wewe ndio registra hapa unajua nani karegister na jina lipi na yuko wapi.

Jana nilijua kua Mkandara na MMJ wamekupa kichwa na leo utaupanda mkenge mbona leo hutukani? Jaribu uone kizee wewe miaka 60 utafikiri umezaliwa jana, maneno ya nonesense tupu, hoja huna nimekuambia siku nyingi sana kwamba wewe as far as siasa ya bongo huna hoja nzito hata siku moja kujifnaya kiingereza maneno makubwa lakini ndani hewa tupu!

Ulipoanza ulifikiri nitakuacha? Umeanza mimi ninajibu tena kiroho mbaya jana nilikupa break ukadhani sasa kila siku, peleka ukikongwe wako huko, Tanzania tuachie sisi raia wake am,bao tuna nafasi ya kuiongoza wewe huwezi tena maana sio raia wetu, nenda huko mkongwe wa hedi wewe, peleka uzee wako mtu mzi a kujifanya mtoto, ili iwe nini? Mwanaume mzima mpaka kujifanya mwanamke ili? jitu zima hovyooooo!
 

Hayo dataz yamekushinda, ya credibility yamekushinda, sasa unalia kwua ninajua sana, views zako hakuna anyekukataza ila huwezi kutoa viwew za kunichokoza nitakujibu kama kawa, kama fuse inakua wrong mtumzima mwanaume miaka 60 mapengo kinywani anapojiita mwanamke, then something is very wrong sio uongo!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…