mwalimu Jr.
Member
- Aug 20, 2008
- 51
- 4
Hao walioko madarakani wanapaswa kutambua kuwa Watanzania wanaweza kuishi bila CHAMA CHA MAPINDUZI lakini hawawezi kuishi bila ya VYOMBO VYA HABARI! Ukweli unaouma kiasi gani huu????
BILA shaka alichokuwa akikizungumza mkuu ni kwamba kama Jukwaa la Wahariri lina viongozi ambao sio watu wa serikali .....yeye na serikali yake hawalikubali.
Mchezo huu wa kutaka kila taasisi ya kijamii kuanzia vijana, wanawake, wazee,walimu wanafunzi na wafanyakazi na kadhalika yaongozwe na watu wanaochaguliwa na serikali ndio umeifikisha nchi hii ambapo leo tuna GDP per capita ndogo kuliko Rwanda na Burundi!!!!
Hawakuishia tu hapo wameingilia mpaka kwenye dini ya Kiislamu lakini wakaogopa dini na madhehebu ya wenyewe wakiogopa Vatican, Ismailiya na Mabohora! Matokeo yake leo tunayaona kwa Waislamu kukosa uongozi wa kweli unaowezz kuunganisha waumini ili kuirahisishia serikali kazi ya utawala.
Na mjumbe wa waziri anatuambia kwamba hakuna ambacho Awamu ya Nne imejifunza toka nchi hii ipate uhuru miaka 47 iliyopita. Mtoto wa Uhuru hana alilojifunza toka makosa ya wale waliopigania uhuru. Tunakwenda wapi jamani? Nyuma au mbele?
Unajua ukiwa kwenye shirika au serikali kwa muda huwezi hata kujua kama ndio inakata roho au vipi!!! Lakini dalili zipo wewe kaa macho wazi, masikio zibua na pua zifanyie mazoezi ya kunusa harufu za jasho, ubabaishaji na uvundo wa kila aina na utagundua nini lijalo baada ya Wazee wa EAC, migomo ya walimu na wanafunzi kwa sababu dira imeharibika....... na chombo ...... pamoja na makidai yote kinakwenda ARIIIIIJOOOOOJOOOO!