LGE2024 Katika shindano la stories of change 2024 nilieleza wazi udhaifu wa sheria zetu za uchaguzi

LGE2024 Katika shindano la stories of change 2024 nilieleza wazi udhaifu wa sheria zetu za uchaguzi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Genius Man

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2024
Posts
1,012
Reaction score
2,317
Katika shindano la "stories of change" ambalo lilikuwa likilenga maboresho ya msingi yanayopaswa kufanyika ndani ya taifa ili kuipata Tanzania tuitakayo katika nyanja mbali mbali ikiwemo masuala ya sheria.

Niliezea wazi udhaifu wa sheria zetu za uchaguzi kwamba zipo kama mapambo na Haziwezi kufanya kazi zinapaswa kujengewa uwezo na utaratibu mzuri ili ziweze kufanya kazi kama tulivyo kusudia kuziweka, Kwasababu udhaifu wowote wa sheria hizi za uchaguzi unaweza kupelekea uchaguzi usiwe wa haki.

Nilieleza kuwa sheria hizi zilipaswa kuboreshwa kwa kuzijengea uwezo na utaratibu mzuri wa kufanya kazi kama tulivyo kusudia kuziweka.

Mfano unakuta sheria zetu za uchaguzi zinataka mtu anayepaswa kuandikishwa kupiga kura anapaswa awe na umri sio chini ya miaka 18 na awe mtanzania, lakini utaratibu wetu wa uandikishaji wa wapiga kura unaweza kumuandikisha mtu yoyote yule hata asiyekuwa mtanzania Kwasababu kwanza uandikishaji wetu hakuna utaratibu wa uhakiki wa taarifa za mtu, katika mazingira kama haya ni wazi sheria zetu bado ni dhaifu na mapambo.

Nilishauri sheria hizi zinapaswa ziboreshwe kwa kujengewa uwezo na utaratibu mzuri ili ziweze kufanya kazi kama tulivyo kusudia, kwa kurekebisha utaratibu wetu wa uandikishaji wa wapiga kura, mtu asiende kuandikishwa mkono mitupu bali kuwe na utaratibu wa kuhakiki taarifa zake kama amekidhi sifa zote kisheria, kinyume na hapo ni wazi kuwa sheria zetu haziwezi kufanya kazi ni dhaifu.


Soma andiko langu hapa katika jukwaa la stories of change 2024
👇

 
Back
Top Bottom