The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Moja ya vitu ninajivunia hapa duniani ni watu. Nina marafiki kadhaa ambao kwakweli tunarahisishiana maisha kwa kiasi kikubwa. Ni marafiki tuliojuana kwa miaka kadhaa na tunapigana tafu. Si urafiki wa kubembeleza au kutafuta. Ni urafiki uliopaliliwa na haiba zetu pamoja na mitazamo yetu. Hatukuwahi kuombana urafiki. Urafiki ulitutafuta ukatuleta pamoja. Tunatoka kwenye backgrounds tofauti kabisa kiuchumi, na huenda kiutamaduni, ila tupo pamoja kwenye shida na raha, kwa hali na mali.
Nimewahi kukutana na watu wanaosema kuwa hawahitaji watu kwenye maisha yao, yaani hawataki ndugu wala marafiki. Ni sawa kabisa. Kila mtu anaweza kuchagua atakalo kutokana na uzoefu wake na akawa na furaha. Kila mtu ana njia yake na hiyo ni sawa kabisa.
Tukirudi kwangu, mimi nina marafiki, tena wazuri na sijutii kuwa nao. Imetokea tu kuwa nina watu wanaotegemeka kwenye maisha yangu. Wale washikaji ambao wakinicheki nikiwa na shida hata kama sina mia basi nitatafuta namna ya kusaidia, labda tu ishindikane. Huwa nabeba shida zao kama zangu na wao wanabeba zangu kama zao.
Ingawa mimi siishi mbali sana na Nyagi, miongoni mwa marafiki zangu wapo kama mimi na wengine hawajawahi hata tu kupasikia Serengeti. Ingawa Uzinzini sipatembelei sana, ila nina marafiki zangu wenye makazi ya kudumu huko. Tofauti hizi haziathiri mahusiano yetu hata kidogo. Tunaishi freshi na kwa codes fulani.
Umeshawahi kuwa na mshikaji ambaye ukimpigia simu ukasema: “Mwenyekiti, heb’ chakata mia chap,” kisha akakusaidia bila hata kuuliza maswali? Una mshikaji ambaye ukimmwambia una ‘kisanga’ anahakikisha haujinyongi? Basi mimi ninao watu kadhaa wa hivyo. Na watu kadhaa naamini wanajivunia mimi kwa namna kama hiyo.
Mimi naamini ukiwa na washikaji wazuri basi maisha unakuwa umeyapatia kwa namna fulani. Tukiwa nao tunajihisi salama kucheua nyongo zetu kuhusu kazi, maisha, mahusiano na kila kitu. Na uzuri ni kuwa haya mambo yanaweza kuwa ni magumu sana kuyaeleza lakini ukiwa na marafiki sahihi yanaweza kuwa ni sehemu tu ya utani. Kwa mfano, nina jamaa yangu mmoja hata nimwambie shida nzito kiasi gani, ana uwezo wa kuidogosha mpaka nikajiuliza kwanini nilikuwa najipa stress. Ana kipawa, au unaweza kuiita talanta, ya kulainisha maisha. Ni gwiji kwenye hilo eneo. Nguli kabisa.
Kumradhi kwa kuongea vitu vingi visivyo na maana, ila ujumbe wangu ni kuwa kwenye maisha tunahitaji watu tunaoweza ku-share nao maisha kwa kupeana motisha, kusaidiana, kukosoana, kusherehekeana n.k. Hii inawezekana kama urafiki huo utakuwa umejengwa kwenye misingi imara. Usimuombe mtu awe rafiki yako, inabidi urafiki utokee tu. Usiogope kumwambia rafiki yako kuwa uzinzi holela au sigara zitamuua. Usisite pia kumueleza ni namna gani yeye ni mtu safi. Ndiyo maisha. Usisubiri amekufa ndiyo uwaambie ndugu zake kuwa alikuwa mtu safi. Watu wanahitaji kujua haya mambo wakiwa hai.
Ulimwengu upo kasi sana. Kadiri maisha yanavyokwenda chuki na maruhani mengine yanaibuka kati yetu wanadamu. Kuna watu wamepitia changamoto fulani zinazowafanya wazungumze vibaya kuhusu ndugu au marafiki. Ni sawa tu kwa wao kushika hizo hisia za kujihami, ila kama wewe binafsi hauna sababu ya kushikilia msimamo huo, basi usiokote tu narratives na ukazinywa kwa fujo.
Katika ulimwengu wa “fu*k friends”, mimi nimechagua kuwa na marafiki na kila tukipata wasaa tunaishi kwelikweli.
Ukute aliyeimba 'Sihitaji Marafiki' naye ana marafiki. 😀
Nakuacha na hili. Je, una marafiki wa kutegemeka? Je, wewe ni rafiki wa kutegemeka?
Well, hili bandiko lilinijia kichwani baada ya kukutana na posti kadhaa mtandaoni zinazo-discourage urafiki na undugu. Mimi naona tofauti. Ahsante.