Katika usajiri huu wa dirisha dogo, chama langu Simba naomba muwasajiri hawa wachezaji 3 kuimarisha kikosi

Katika usajiri huu wa dirisha dogo, chama langu Simba naomba muwasajiri hawa wachezaji 3 kuimarisha kikosi

Thailand

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2019
Posts
275
Reaction score
795
Kwanza niwe muwazi mimi ni shabiki wa Simba SC haswa. Sasa hatari ninayoiona kwa musimu huu wa ligi kuu, ni ubora alionao mtani wetu Yanga SC, bila unafiki na ushabiki hakika Yanga wanakikosi cha kutisha mpaka na hofu nani wa kuweza kumzuia hasichukue ubingwa.
Kibaya zaidi ninachokiona mbele yetu ni Kichapo tutapewa na Yanga na ubingwa watachukua.
Hilo litakuwa jambo baya sana sisi mashabiki wa Simbab SC kupigwa na mtani na uingwa kunyang'anywa.

Lakini ninaona bado wanasimba tuna muda wa kuzuia mojawapo au yote yasitokee.

Udhaifu wa Simba upo sana sehemu ya katikati hasa baada ya Thadeo Luanga kuumia.
Mkude ni mzuri sana ila anaitaji viungo wenye nguvu sawa na yeye wasiochoka ili kupambana mwanzo mwisho.
Pendekezo la Kwanza ni:
1. TONOMBE MUKOKO
HUyu jamaa ni bonge la kiungo ambaye kule utupoloni hapewi tena nafasi baada ya majukumu yake kuwa covered na wachezaji wengi tu. Simba muwekeeni mzigo huyu jamaa ahamie msimbazi. Itakuwa partnership nzuri endapo MUKOKO, MKUDE NA LUANGA AU KANOUTE wanaanza kwenye game.

2. AMBROS wa Biashara United
Viongozi wa Simba mtafuteni huyu mwamba anajua kupiga ma cross hatar sana halafu ana upepo wa kutosha. Hii wingi sio ya kuicha,

3. ANUARY JABIR wa Dodoma jiji
Tuongeze idadi ya washambuliaji kwenye kikosi chetu. Huyu kijana ana mwili wa kutosha ana kimbia sana tudimuache huyu kijana kwenye msimu huu wa dirisha dogo la usajiri.
Najua viongozi wangu mnaenda kufanya usajiri msije mkafanya tena makosa ya kutuletea watoto wa shule kama BANDA, kumbukeni tunaitaji kutetea ubingwa wetu.
Wachezaji mnaoweza kuachana nao kwenye dirisha hili ni JOHN BOCO, BANDA, KOPE KISHIMBA, PASCAL WAWA.
ASANTENI
 
Back
Top Bottom