Katika utawala wa Raisi Samia mawakili wanasheria wamekuwa na kazi nyingi sana; sababu ni haki na usawa kuongezeka au kuzidi kuporomoka?

Katika utawala wa Raisi Samia mawakili wanasheria wamekuwa na kazi nyingi sana; sababu ni haki na usawa kuongezeka au kuzidi kuporomoka?

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Ni jambo ambalo nimelishuhudia na sijui kama watu wengine wanaliona, kwamba katika awamu hii ya utawala wa Raisi Samia kumekuwa na masuala mengi sana yanayohusu wanasheria hawa mawakili wetu. Labda niseme wazi kwamba haijawahi kutokea katika jistria ya Tanzania mawakili wakawa busy kama hivi sasa chini ya utawala wa Raisi Samia.

Wakati wa Nyerere watu wengi hata hawakujua kuna kitu kinaitwa advocates, na kidogo wakati wa Mwinyi pia. Wakati wa Mkapa walianza kujitokeza, na wakati wa Kikwete walizidi kujitokeza lakini hawakuwa na kazi nyingi za mahakamani. Wakati wa Magufuli uwakili wa kwenda mahakamani ukaanza kuwa dili sana, na tasnia ya uwakili ikakua kwa kasi, kasi ambayo tuseme imekuwa mara mbili zaidi katika kipindi cha utawala wa Samia.

Kuna sababu zozote za msingi kwa nini utawala wa Raisi Samia unahitaji shughuli nyingi sana za mawakili wa sheria?
 
1724397789519.png
 
Mahakama ni ofisini kwa wakili. Je kuna tatizo mtu kwenda ofisini kwake?
 
Ishu hapa ni utandawazi yaani sio kwamba matukio yalikuwa hayapo no
sasa hivi kila mwenye simu janja ni muandishi
naamani umbea umetamalaki.
 
Back
Top Bottom