Kabudi na Lukuvi walikuwa ni mawaziri wawili walioapishwa kabla ya wengine na JPM mara baada ya matokeo ya uchaguzi wa 2020. Kama sikosei waliapishwa siku moja na Waziri Mkuu.
Ila siku hiyo walipoapishwa JPM aliwapa angalizo kuwa baada ya yeye kumaliza awamu yake na hatimaye kuondoka madarakani, asingekubali Rais ambaye angemfuatia kuwa na umri zaidi yake yeye.
Inaonyesha hawa waheshimiwa eawili wana pilikapilika nyingi sana za chini kwa chini kuhusu nafasi hiyo nyeti. Kiuhalisia kuonyesha nia ya kuishika nafasi hiyo wala si dhambi, kwa kuwa hata katiba yetu hutoa sifa za mtu kuweza kuitwaa nafasi hiyo.
Mimi nashairi, kama kweli wana nia ya kuendelea kuitolea macho nafasi hiyo, basi hawana budi kujiunga na vuguvugu linafukuta hivi sasa nchini la kutaka kuwa na katiba mpya. Hapo ndipo watapata fursa nzuri sana ijapokuwa nao watapitia misukosuko mingi toka katika vyombo vya dola.
Ni ukweli usiopingika kuwa wao walikuwa ni mawaziri vipenzi wa JPM. Lakini kwa sasa nyakati za zamani zile za awamu ile zimekwishapita, hata kama zama hizo zilifupishwa. Hii sasa ni zamu ya watu wengine, ambao hata nao wana vipenzi vyao.
Tahadhari yangu kubwa kwa wasije kujikuta wanafukuzwa ndani ya chama. Na hatimaye baada ya muda wajikute wanalazimika kurudi tena katika zizi walilotokea huku wakiwa wamekatwa mikia.
Hapa nchini kuishi kama mpinzani wa CCM ama Rais ni kazi ngumu kweli kweli. Majibu yapo kwa akina Lowasa, Sumayi, Membe, Nyarandu, Mgeja, na wengine wengi.