Pre GE2025 Katoliki na KKKT yawakataa Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi, sasa inasubiriwa BAKWATA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Bakwata hii hii tawi la CCM?
 
Bakwata hawaangalii sana kilio cha wananchi! wao muda mwingi wanaunga mkono mambo ya watawala.
 
Sio jambo jema wakurugenzi ambao ni sehemu ya serikali kusimamia uchaguzi kati ya vyama vya upinzani na ccm- chama tawala(serikali), halafu msimamizi- mkurugenzi wa Halmashauri aliyeteuliwa na Rais wa Ccm- na anayelipwa na serikali ya Ccm-.

Hapo ni sawa sawa kwamba mko na mechi kati ya timu A na B, halafu refa na wasaidizi wake wote wateuliwe na kulipwa na uongozi wa timu A
 
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania kuhusu uongozi na utawala bora


SEMINA YA VIONGOZI BAKWATA MADA UONGOZI NA UTAWALA BORA


View: https://m.youtube.com/watch?v=Qt0qrpPU2Eo
Ustadh. Mwenda Said naibu katibu mkuu BAKWATA Taifa amwalika Bw. Joel Nanauka kutoa muhadhara wa uongozi na utawala bora

Viongozi wa BAKWATA kutoka mikoa mbalimbali walihudhuria semina hiyo iliyotayarishwa na BAKWATA kufahamu juu ya uongozi na utawala bora ili kutekeleza majukumu yao vizuri zaidi ...

BAKWATA siku zote imewaweka waumini mbele kupitia kuwa karibu na serikali mbalimbali za kilimwengu ili kuhakikisha mambo yanaenda sawa katika jamii pana ya Tanzania .




Balozi wa Marekani amtembelea mhe Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania.


Ziara ya mama Samia Suluhu Hassan
 
Mheshimiwa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dr. Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally apokea ujumbe mzito.

Balozi wa Marekani akiongozana na ujumbe wake , nchi inayoongoza katika kuchagiza demokrasia afika katika ofisi za makao makuu ya BAKWATA na kuonana na mufti wa Tanzania


Picha: Muft na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dr. Sheik Abubakar Zubeir bin Ally akiongea na wageni wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…