Kauli hii ya Kardinal Pengo,inatukumbusha "upande wa pili" wa Kanisa Katoliki

nitavipataje?
 

Hawa wasio kuwa na familia uchungu na ugumu wa maisha wataujulia wapi?
Hawa waliozoea kuishi kwa toa toa ndugu bwana atakuongezea maisha magumu watayajulia wapi?
 

Hakika Titicomb ,huo ndio ulikuwa msingi wa hoja yangu,na si vinginevyo
 
Nadhani ingekuwa vema ungeweka tu hiyo mifano ungekuwa umemaliza ubishi wala usingelazimika kutuita wajinga watu wote wangejua sisi ni wajinga kwa kutokujua taarifa hizo. Mwisho wa angalizo hili jukwaa sio lazima utukane.
 
Mimi mwenyewe sijaamini kama kusema hivyo alikuwa amedhamiria,, inawezekana maneno yalimtoka bahati mbaya.. ila hata kipindi fulani maaskofu walitoa waraka juu ya katiba mpya, ila yeye akaja kupingana nao.. Mungu atusaidie sana..
Msaada wa Mungu katika hili ni kutuondolea vikwazo. (kikwazo mnakijua)
 
Sikua na mpanngo wa ku comment chochote kwenye hu uzi na sio kwasababu ya kumpenda au kumchukia mtu yeyote bali ni kwasababu ya utafiti na mleta uzi alivyo connect dots so nimeridhika kabisa, niseme pia nimesoma michango ya watu wote hadi page ya 6 but nimelazimika kurudi nyuma tena ili nifatilie unacho kiandika (page 5). NIlipokusoma tu kule ukurasa 1 nilihisi kitu kuhusu wewe; ni kweli alioyasema Pengo yana ukakasi but hata wewe ingekua vizuri kama ungeleta DATA ili tujue unacho kisema ni kweli au UONGO. Watu wa dini Fulani hua hawaoni shida kumzushia mtu wa dini nyingine UONGO, sina hakika kama mungu wao kawaruhusu hivyo au LAA; Kuna sehemu umetaja miezi ambayo taasisi za serikali zilifanyia mikutano yake kwenye kumbi za TEC Kurasini na Msimbazi centre, mleta, huyo unaye bishana nae anaomba utaje mikutano hiyo, porojo za nini!? Wengine ambao hatupo Dar na ambao pia sio Wakatoriki tunakutafsiri kama wewe ni muongo na mchonanishi. Weka DATA uaminike, sio POROJO.
 
Jambo lolote lenye hoja mkingamo haliwezi kuwa kweli kwa upande wowote wa wanaobishana kwa kuishia tu kusema mimi najua ni kweli basi inakuwa kweli bila kuleta mifano ya kupinga hoja ya mwenzio na kutetea hoja yako. Tupe mifano mkuu wewe haitoshi tu kusema wewe unajua ni kweli tuletee hicho kithibitisho kilichokuamisha wewe nasi tuamini.
 
Ukiacha kufundisha YaliYomema na kukataza mabaYA kazi nYingine Ya hizi dini ni KUJENGA MATUMAINI miongoni mwa Waumin wake hapa sasa kusema ukweli panakuwaga mtihan Tumuelewe tu
 
Nahisi pia huyu jamaa alimwambia asihudhurie ibada ya xmass kitaifa wala kupeleka kiongozi wa juu kule BUKOBA.
Pengine alijua watu watakuwa na maswali mengi.
 
1 Kama clue niliyowapa hamuwezi kuifuatilia mpo kwenye wrong forum.

2. Mimi pia sipo DSM ila nilikuwa na kazi za taasisi za serikali. Ndipo nikajua wamepewa masharti hayo na maagizo wapi wafanyie mikutano yao hususan kumbi za katoliki bila kuhojiwa au kubughudhiwa. Na kweli ilifanyika.

3. Kuhusu chuki za kidini hususan kwa kanisa katoliki mwenye macho haambiwi ona.

4. Kuhusu kujadiriwa kwa hoja ya msingi niliyochangia nashukuru mmejitokeza na kukiri mchango wangu ni serious allegation. Mimi narudia siyo allegation ni personal experience na practice inayoshudiwa si na mimi tu bali na watu wengi

5. Mantiki ya mleta mada "barafu" ni kuwa awamu hii imesababisha ugumu wa maisha ni ajabu Pengo anazungumza tofauti na wengine tunavyoshuhudia ugumu wa maisha. Akaeleza ukaribu wa kanisa katoliki na utawala na hususan utawala wa awamu hii. Hilo hamtaki kulijadiri baadhi yenu kwa sababu hamna hoja mbadala.

6. Kama unataka kujiridhisha na ukweli au uongo wa mtu tafuta ushahidi wa uongo wake umwanike. Kumbe hata uwezo wa kutumia vidokezo hamna.

Anayehubiri udini anayetuamulia watawala na anayezuia demokrasia ya kweli hapa kwetu ni kanisa katoliki kwa kukumbatia watawala maimla. Na hawaishii hapo tu South America Far East na sasa USA. Someni mpate elimu mjikomboe.
 
Ndugu zangu, tukubali kuwa usemi wa hali ngumu tumeaminishwa tu na baadhi yetu. Manake kwa wengine, mie nami nimo! sijaona tofauti ya nilivyokuwa kabla ya Nov 2015 na baada. So hiyo homilia inatoa hali halisi ya maisha. Wengine hali ngumu wanayodai ni kwa ajili ya kuhalalisha kusitisha majumu yao kwa wanaowategemea. Ndivyo nionavyo!!
 
Lile lipete likubwa kwenye kidole cha pengo mkono wa kushoto huwa la nini lile lipete
 
tatizo kubwa sana every body is trying to be a puppet ..... hawa watu wa makanisa makubwa wanashindwa kukabiliana na matatizo yao binafsi ya waumini kupungua sadaka kupungua wanasaidia wengine ....kanisa linapoteza ushawishi siku hadi siku... itafika mahali watakosa sadaka za kutosha na sio muda mrefu siku izi kuna makanisa mapya yanafunguliwa daily na wanajua jinsi ya kuifanya kazi ya kiroho vizuri ...sasa huyu kadinali na maaskofu waendelee kuleta masihara tu kanila litaanguka muda sio mrefu miaka mingine 50
 
Mkuu maelezo marefu unazunguka tu. Fanya hivi kumaliza ubishi
(1) Tuwekee waraka au barua ya serikali yenye kuagiza au elekeza mikutano yote ya taasisi za serikali ifanyike ktk kumbi za kanisa katoliki. Au tuwekee hapa audio au video ya mtua akitoa maagizo hayo.
(2) Tuwekee hapa ushahidi wa hiyo mikutano na tarehe zake na jina la kumbi ili tujiridhishe kama utekelezaji wa hilo agizo au waraka ulifanyika.
Kama ukishindwa hayo mawili hapo juu inabakia kuwa ni tuhuma tu ambazo tunashindwa kuelewa nia ya mtoa tuhuma.
Natanguliza shukrani mkuu. Ukiona hauna ushahidi basi nyamaza au omba kurekebisha kauli zako kisha tuendelee na mjadala mkuu kuhusu kauli ya Kadinali Pengo ambayo wengi tumekubaliana imeleta tafrani, mixed feelings, na taharuki. Pamoja na matatizo yote yaliyotokana na kauli yake lakini nasi yatupasa tujadili kwa hekima tusilete tuhuma zinazoweza kuleta matatizo makubwa mbele ya safari hasa zikiwa zinajielekeza kuwajaza watu chuki dhidi ya watu au taasisi nyingine. Tanzania ni moja wajibu wetu kuitunza kwa ajili ya vizazi vyetu tusinge penda yatokee ya Yugoslavia na Bosnia, Rwanda na Burundi, Liberia na Sierra leone, Syria na Libya. Amani kwako mkuu.
 
Hivi mtuhumiwa anajipeleka polisi ajieleze makosa yake?

Kinawashinda nini kuainisha uongo wangu?

Barua za serikali hazinihusu.

Kama umetumwa kawaambie huu upuuzi wenu unafahamika na tupo wengi hatufurahii licha ya kwamba hamlisaidii taifa.
 
Hivi mtuhumiwa anajipeleka polisi ajieleze makosa yake?

Kinawashinda nini kuanisha uongo?

Barua za serikali hazinihusu.

Kama umetumwa kawaambie huu upuuzi wenu unafahamika na tupo wengi hatufurahii licha ya kwamba hamlisaidii taifa.
Mtuhumiwa ni serikali kwamba imetoa maagizo hayo ya upendeleo kama unavyotaka kutuaminisha.
Mtoa tuhuma dhidi ya serikali ni wewe ambae tunakuomba lete ushahidi kuthibitisha tuhuma zako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…