Kauli hii ya Pastor Tony Kapola inachochea ukatili dhidi ya wanawake walioko kwenye ndoa! Wanawake msifuate ushauri huu

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Inasikitisha sana huu uchochezi kufanywa na huyu mtumishi wa Mungu.

Sikutegemea kabisa kuona maneno kama haya yakitolewa na mtu kama huyu

Ningekuwa na mamlaka makanisa kama haya ningeyafutilia mbali.

Hiki ndicho alichokisema:

"Mama zetu walivumilia kwa sababu baba zao hawakuwa tayari kuwaona wanarudi nyumbani. Wakienda kusemelea kwa mama yake, mama mimi John ananifanyia hivi na hivi. Ananitesa, ananinyanyasa, ananipiga. Mama yake anamwambia hivi Mbona mimi baba ako ananipiga, ni kawaida, vumiia tu mwanangu"

"Siku hizi mama ako mwenyewe, kaachika. Anakwambia hivi "akikunyanyulia mkono chumba chako bado kipo. Kwa hiyo binti anaingia kwenye ndoa anajua kabisa chumba chake bado kipo. Kijana jichanganye"

Ni kauli kama hizi zinazofanya wanawake wabaki kwenye ndoa ambazo zimejaa manyanyaso na ukatili uliokithiri.

Ripoti ya World Bank iliyotoka mwaka 2022 ilisema kabisa kuwa asilimia 40 ya wanawake wenye umri kuanzia miaka 19 hadi 40 wameshawahi kupigwa au kufanyiwa vitendo vya ukatili.

Kwa takwimu kama hizi, mtu mashuhuri kama huyu anajitokezaje kwenye halaiki ya watu na kutetea ukatili kwa wanawake.

Kwanini Pastor asingetumia muda huu wa kutetea ukatili kwa wanawake, kuwasema wanaume wanaopiga wanawake zao?

Inasikitisha sana!

Hata mimi ningekuwa na mamlaka ninge wafutilia mbali nyinyi midume mlio jaa mawazo ya kifenist ndani ya nchi hii maana ndo chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika.

Ww feminist una ujinga mwingi eti wana ume mzima unajiita mama samia upuuzi tu.
 
Vunja chupa ya soda kisha kusanya vile vipande uvikalie ukiwa uchi.
 
Hili ni lipuuzi. Familia nyingi zinaharibika watoto wanabaki machokoraa
 
Aloo! Kupigana kupo.. kunaweza kusiwe kwa vitendo ila kupo, mwanamke akija physically atakutana na kitu fiziko ila kwa ajili ya self defense. Then nita retaliate as a Gentleman maana siwezi ruhusu upuuzi wake unipeleke Sentro.
Ila Kama akinikosea na bado akawa mkaidi naenda kutafta mtoto mbichi zaidi yake naanza upya ye namuacha na life lake..
Mnawaza Sana kuhusu clean shit ya “Kutokuvunjika kwa Ndoa” mnasahau mustakabali mzima wa Wanandoa..
in reality Ndoa ni fungamano tu la kidhahania ila halina practical evidence yoyote zaidi ya Cheti na Maandiko ya kiimani.
Zinatakiwa zivunjike hiviii mpaka itafika steji watakao kua wanaoana ni watu waliomaanisha haswa… sio saizi watu wanaoa kwa sababu za desturi za kimapokeo ambazo ukiangalia chimbuko lake ilikua ni mikataba ya kiutawala, biashara na njia kujirasimishia viburudisho enzi za Zama za mawe za kale…
 
Hata mimi ningekuwa na mamlaka ninge wafutilia mbali nyinyi midume mlio jaa mawazo ya kifenist ndani ya nchi hii maana ndo chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika.

Ww feminist una ujinga mwingi eti wana ume mzima unajiita mama samia upuuzi tu.
Nimecheka kwa nguvuuu sana Wewe jamaa phala sana,
Eti mwanaume anajiitaje
Mama samia!!

Hahahah jamaa hua hahudhurii vikao mbona wenzake
kina Maghayo The Mongolian Savage I'd zao zina majina ya Kibabe sana?

😂😂😂
 
Mbona ujumbe wa jamaa na malalamiko ya mtoa uzi ni vitu viwili tofauti. Tony hapo kaonesha namna wazazi wanamchango kwenye ndoa za mabinti zao.

Na kaangalia pande zote mama akiwa anamfanya binti kuwa mvumilivu na namna pia baba anaweza kumharibu binti yake kwa kumpa kila kitu na kukataa kumuachia awe chini ya mwanaume mwengine hasa hapo aliposema ''dad's daughter'' .
 
Back
Top Bottom