Inasikitisha sana huu uchochezi kufanywa na huyu mtumishi wa Mungu.
Sikutegemea kabisa kuona maneno kama haya yakitolewa na mtu kama huyu
Ningekuwa na mamlaka makanisa kama haya ningeyafutilia mbali.
Hiki ndicho alichokisema:
"Mama zetu walivumilia kwa sababu baba zao hawakuwa tayari kuwaona wanarudi nyumbani. Wakienda kusemelea kwa mama yake, mama mimi John ananifanyia hivi na hivi. Ananitesa, ananinyanyasa, ananipiga. Mama yake anamwambia hivi Mbona mimi baba ako ananipiga, ni kawaida, vumiia tu mwanangu"
"Siku hizi mama ako mwenyewe, kaachika. Anakwambia hivi "akikunyanyulia mkono chumba chako bado kipo. Kwa hiyo binti anaingia kwenye ndoa anajua kabisa chumba chake bado kipo. Kijana jichanganye"
Ni kauli kama hizi zinazofanya wanawake wabaki kwenye ndoa ambazo zimejaa manyanyaso na ukatili uliokithiri.
Ripoti ya World Bank iliyotoka mwaka 2022 ilisema kabisa kuwa asilimia 40 ya wanawake wenye umri kuanzia miaka 19 hadi 40 wameshawahi kupigwa au kufanyiwa vitendo vya ukatili.
Kwa takwimu kama hizi, mtu mashuhuri kama huyu anajitokezaje kwenye halaiki ya watu na kutetea ukatili kwa wanawake.
Kwanini Pastor asingetumia muda huu wa kutetea ukatili kwa wanawake, kuwasema wanaume wanaopiga wanawake zao?
Inasikitisha sana!