Kauli hizi Mbili za Injinia Hersi na Mhamasishaji Nugaz zitakusaidia vyema kujua Yanga SC ni Klabu ya aina gani

Kauli hizi Mbili za Injinia Hersi na Mhamasishaji Nugaz zitakusaidia vyema kujua Yanga SC ni Klabu ya aina gani

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Kauli ya Injinia Hersi Ligi ikianza

"Kwa jinsi Yanga SC kupitia Sisi GSM tulivyofanya Usajili huu mkubwa naomba kila mwana Yanga SC ajigambe na tusipokuwa Mabingwa Msimu huu wanihoji Mimi na wakiweza wanifanye lolote. GSM tumedhamiria na hatubahatishi na tumeisajilia Yanga SC Wachezaji wakubwa na mahiri ambao hata kwa Wapinzani wetu hawapo na walikuwa wakiwatamani mno tu "

Kauli ya Mhamasishaji Nugaz leo

"Tusidanganyane Yanga SC yetu bado inajengwa na kama ni kuanza kuwa Mabingwa labda kwa baadae ambapo huku Kocha mpya Nasreddine Nabi akiwa ameshaisuka vyema Timu yetu. Tukiwa Mabingwa msimu huu ni bahati tu ila sidhani sitaki niwe Mnafiki na niseme Uwongo katika Mwezi Mtukufu huu tulionao "

Generalist akiwakosoeni hapa mnanuna.
 
Kwa kauli hizi mbili tofauti yaonyesha pale Jangwani kila mmoja na lengo lake na kauli yake.

Ndo sasa nimemulewa Kocha Mwambusi alipoulizwa baada ya game ya Jana kuwa, Ujio wa Kocha mpya unaweza kuwa chachu ya njia nyepesi kuchukua ubingwa?

Mwambusi alimjibu mwandishi wa Azam Sports " Asante sana".
 
Simba atachukua ubingwa miaka mitano mbele mfululizo, na huo mwaka wa sita ni maamuzi tu tukiamua tunabeba tena na tena, hao GSM watakimbia wenyewe.
 
Back
Top Bottom