Kauli na matendo ya Rais Samia yameituliza nchi na kuwaunganisha Watanzania katika kuijenga Tanzania Yetu

Mifumo gani. Hebu tupe mfano hata mmojja
Sheria na katiba ndiyo viwe miongozo.

Angalia Japan, Uingereza, n.k nchi ambazo zinayojulikana kama constitutional sensitive countries. Kila mtu anaiogopa katiba. Na mambo yanakwenda vizuri mno. Hiyo ndiyo mifumo Sasa.


Jambo linalokiuka katiba na sheria likitokea kiongozi anajitathmini na kuachia ngazi.
 
Rais wetu naweza kusema anaendesha nchi kwa kufuata na kuzingatia kanuni na miongozo ya utawala Bora na utawala wa Sheria, Ndio maana unaona namna nchi ilivyoTulia na ilivyo na amani, Watu wapo huru na hawana hofu yoyote maana wanajuwa mama Ni kiongozi na siyo mtawala, wanaoona mama Ni mtumishi wao Ni siyo Mtukufu
 
Sijui kama unajua watu wa kanda ya ziwa wanawekwa pembeni siku hadi siku...sijui kama unajua kwamba hiyo inaweza kua sumu ya baadae? Tafakari kwa kina usikurupuke tu
 
Sijui kama unajua watu wa kanda ya ziwa wanawekwa pembeni siku hadi siku...sijui kama unajua kwamba hiyo inaweza kua sumu ya baadae? Tafakari kwa kina usikurupuke tu
Hakuna Anaye tengwa Wala kuwekwa pembeni na mama yetu, Ndio maana umeona hata ziara amefanya za kutosha katika ukanda huo, Kila mtanzania anapewa nafasi kulingana na uwezo wake bila kujari katokea wapi, Tuondoe mawazo ya kikabila,kidini na kikanda katika akili zetu, Mtu akiteuliwa tusianze kuulizana habari ya kabila lake au dini yake, Bali tuulizane juu ya uwezo wake katika nafasi aliyoteuliwa kuishika na anaweza na amekidhi vigezo na ataweza kuimudu
 
Naungana na wewe na hakuna anayebisha Hilo. Lkn hizo kanuni na miongozo ya utawala bora za Samia zilipaswa zifungwe kwenye sheria mama (katiba). Isiwe kwa utashi wake.

Katiba yetu inampa rais Uhuru wa kuwaumiza, kutesa na kuwanyima watu haki zao kama ilivyokuwa kwa awamu ya tano. Haya ndiyo tunasema yarekebishwe na mama.
 
Wenzake huwa wanafanya mageuzi makubwa ndani ya siku 100 tu. Huyu nishamstukia . UTANIKUMBUKA!
😁😁..Taratibu tutaelewana tu!
CCM huwa inabadilisha rangi tu.
 
😁😁..Taratibu tutaelewana tu!
CCM huwa inabadilisha rangi tu.
Mzizi wa tatizo ni mm, wewe na yule. Kwa pamoja tunastahili lawama. CCM hawawezi kujikaanga kwa kuweka mazingira mazuri ya siasa ili waondoke madarakani. Ilipaswa tuwashinikize. Lkn ndiyo tuko bize kuomba connection
 
Tutafika huko kwenye katiba muda ukifika, Hakuna jiwe litakalobaki bila kugeuzwa katik uongozi wa mama yetu kipenzi mama Samia suluhu Hassani, Amedhamilia kuijenga nchi hii na kuinua maisha ya watanzania, Tumuunge mkono na kumwombea ili mungu azidi kumlinda wakati wote
 
Mama hana noma akisema "Na hayo mukayangalie" ana maana hiyo ni sauti ya Rais si sawa na sauti za mitaani msichukulie poa
 
Dikteta aliligawa Taifa kwa udini na ukabila wake, na amezalisha mazezeta wengi wasiojitambua
 
Sijui kama unajua watu wa kanda ya ziwa wanawekwa pembeni siku hadi siku...sijui kama unajua kwamba hiyo inaweza kua sumu ya baadae? Tafakari kwa kina usikurupuke tu
Iwe sumu baadae kwani hao watu wa kanda ya ziwa ndio wenye Nchi? Magufuli aliwalisha ujinga
 
Kazi iendelee πŸ’ͺπŸ’ͺπŸ’ͺ
 
Kodi Ya Dhulma Ndiyo Inayokusanywa Sasa Hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…