Kauli tata kutoka Kwa Katibu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi

Kauli tata kutoka Kwa Katibu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Miongoni mwa masuala yanayowafanya wafanyakazi kushindwa kuuelewa umuhimu wa vyama vya wafanyakazi ni pamoja na kauli tata za viongozi wa vyama vya wafanyakazi hususani wanapouulizwa maswali yanayowasumbua wafanyakazi wengi.

Katibu alipoulizwa kuhusu kikokotoo jibu alilolitoa kwa kweli ni swali jingine, kumpa mfanyakazi jibu kuwa viongozi walijadiliana kutoka asilimia 25% hadi 33% ambayo inaonekana kero hakumfanyi mfanyakazi kuelewa ukizingatia hali haikuwa hivyo hapo mwanzo. Ipo haja ya kuonesha historia fupi ya mabadiliko hayo na misukumo yake.

Kuna mahali alisema......." We still have a room to bargain". Hapa tunajiuliza je hawa wawakilishi wetu kupitia vyama vya wafanyakazi wanawakilisha sauti za wafanyakazi kwa kuangalia nafasi ya majadiliano iliyopo au mahitaji ya wafanyakazi na hali iliyopo.

Viongozi wengi katika vyama vya wafanyakazi hawana ujuzi wa mjadiliano rafiki "social dialogue skills. Hata kama nafasi ya majadiliano ikiwepo bado lobbying effects ya viongozi wetu ni ndogo sana sidhani kama majadiliano yatakuwa yenye tija.

Nikiangalia mahusiano uwili au utatu" bi-partite/tripartite" yanavyofanyika bado viongozi wetu wanahitaji kujinoa zaidi kwenye stadi za majadiliano na mikataba ya majadiliano kuliko kukimbilia tu kujadiliana kwa sababu nafasi ipo. Vipi kuhusu " power relations " kwenye majadiliano. Je madlahi mapana ya umma " public interest" yanaangaliwa kwa haki pasi na matumizi yake kama silaha ya upande mmoja?

Bado tuna safari ndefu sana.
 
Back
Top Bottom