Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Juzi Ally Hapi alivitaka vyombo vya dola kuwachukulia hatua CHADEMA wanaotaka uchaguzi usifanyike bila ya mabadiliko kufanyika, akisema ni kisingizio kwa kuwa hawajajiandaa.
Kauli hii inazidi kukandamiza wapinzani na wananchi kwa ujumla kwenye uhuru wa kutoa maoni yao pale wanapoona mambo hayaendi vizuri.
Pia soma: Pre GE2025 - Ally Hapi: Vyombo vya dola shughulikieni wanaotaka kuzuia uchaguzi
Na hili litachochea umwagaji damu zaidi kipindi hiki cha uchaguzi kwa kufanya vyombo vya dola kutumia nguvu ya ziada sehemu ambayo haisatahili sababu tu CCM inaogopa kuwa challenged na CHADEMA. Kama hawaoni shida kwenye sheria za uchaguzi wapingane kwa hoja, sio kujificha nyuma ya polisi.
Kauli hii inatakiwa kukemewa mara moja na vyombo vya dola hasa jeshi la polisi. Viongozi wasiwatumie ovyo kuua demokrasia nchini na kufanya watu makasuku. Likiachwa hili itakuwa kawaida kwa jeshi la polisi kuchukuliwa kama vikundi vya wahuni wanaoweza kutumika kwa maslahi binafsi.