Kauli ya CDF mstaafu kuhusu waliotaka kupindisha katiba ili Rais Samia asiapishwe inanipa picha halisi ya kwanini Bashiru na wenzake walitenguliwa

Nadhani upo sahihi mkuu
Hata hii clip ukijuliza Why? na kutafakari kwa makini utaona kuna ujumbe na pengine majuto pia. Sikilizeni kwa makini na mjiulize kwa nini yamesemwa yaliyosemwa na aliyesema
Sure mkuu Mabeyo alitumika bila kujua na alipojua ndipo alipoamua akae pembeni kwahiyo bila shaka atakuwa na Majuto tu
 
Hiyo sheria unayotaja hapa uliitunga wewe peke yako? Alitakiwa astaafu lini na kwa sababu ipi

CDF anastaafu akiwa na miaka mingapi, na Mabeyo alistaafu akiwa na mingapi. Hujui Mabeyo alikuwa na umri mkubwa kustaafu kabla hata hajawa CDF? Yani mtu alipitiliza umri wa utumishi, anastaafu unalalamika.
 
Dah
Sikupingi mkuu! Ila dah
Anyway wewe tu uamue uendelee au usiendelee
 
Mkuu naomba karudie interview ya ex mkuu wa majeshi,ina maana hakuna hata mmoja aliyekuwa karibu Naye siku za mwisho za umauti wake??? Hata makamu?? Hata pm majaliwa???

Kwanini magufuli alimtumia mabeyo??? Angali viongozi wake wa juu wapo??? Magu alimuamini Sana mabeyo, alijiona yupo salama akiwa Naye kuliko kiongozi yoyote.

Kwanini pm majaliwa aliydanganya Uma kuwa yupo anachapa kazi, angali alikua yupo mahututi akipigania maisha yake??
 
Kwa hiyo Magufuli ndio aliandika sheria ya utumishi jeshini. Kwamba kabla ya Magufuli kuja, Majenerali walikuwa hawastaafu?

Na kama alikuwa ameishapanga Mabeyo astaafu lini, ni lazima iwe hivyo hata kwa Rais aliyefuatia. Hujui kwamba katiba inampa mamlaka Rais kuteua CDF, kwamba ni lazima Samia aishi katika kivuli cha Magufuli?
 
umeiweka vizuri sana mkuu.....
huyu mtu ilitakiwa jpm amtoe kabla hajakata moto, (maana inaonekana alijua haponi)
 
Kundi lipi lililofata katiba au lililotaka kuipuuza katiba?
 
Hivi mkuu wewe bado haujawajua tu hao wanaolazimisha siasa, katika mambo yasiohitaji siasa!
 
Mkuu naomba karudie interview ya ex mkuu wa majeshi,ina maana hakuna hata mmoja aliyekuwa karibu Naye siku za mwisho za umauti wake??? Hata makamu?? Hata pm majaliwa???

Kwanini magufuli alimtumia mabeyo??? Angali viongozi wake wa juu wapo???
Mkuu nimekwambia kwamba Mabeyo ndio alikuwa karibu na mgonjwa muda wote, hivyo ni lazima maelezo yote muhimu apewe yeye. Hata mzazi anapoona muda wake wa kubaki dunia umekwisha, basi hutoa usia wake kwa mtoto aliepo karibu yake ili afikishe ujumbe kwa wenzake waliopo mbali.

Haiwezekani kwa hali ya umauti aliyokuwa nayo eti angekaa tu asubiri mpaka makamu atoke Tanga aje ampe maagizo ya nini kifanyike na wakati mtu wa kumpa maagizo hayo yupo nae karibu.
Magu alimuamini Sana mabeyo, alijiona yupo salama akiwa Naye kuliko kiongozi yoyote.
Angekuwa amuamini makamu basi asingeendelea kuwa makamu wake katika uchaguzi mkuu wa 2020. Kumbuka yeye ndie alikuwa raisi na mwenyekiti wa chama, so angeweza kumchagua yoyote anaemtaka yeye pasipo kupingwa na yoyote. Na kwa vile uchaguzi alikuwa ashajiandaa kushinda basi angeshinda tu hata kama makamu angekuwa fatuma Karume.
Kwanini pm majaliwa aliydanganya Uma kuwa yupo anachapa kazi, angali alikua yupo mahututi akipigania maisha yake??
Hakutaka kuleta taharuki katika jamii, kumbuka kipindi kile kuna kiongozi mmoja wa chama aliekuwa amehifadhiwa na mabeberu huko Ulaya, kila siku ilikuwa kazi yake ni kubwabwaja na kubwata katika mitandao ya kijamii kuhusu afya ya raisi Magufuli. Hivyo Majaliwa hakupenda na yeye kuwa miongoni mwa waliokuwa wanagombania kuleta taharuki katika taifa kutokana na hali ya raisi.
 
Mkuu kama ukisoma katikati ya mistari ya kauli zake utaona mjadala ulikuwa unafanywa kwingine, yeye Mabeyo anafanya maamuzi kwa manufaa ya Taifa!
 

Sasa aliyeongelea habari za mujibu wa sheria ni nani kati ya mimi na huyo niliyemquote, na umeona wapi kwenye Comment yangu kuna mahali nimelalamika kuhusu CDF kustaafu, kina David Musuguri na Ernest Kyaro walistaafu wakiwa na miaka mingapi mkuu


Mkuu sisi tunaandika kulingana hali halisi iliyopo siyo kwamba hatuzijui sheria ila swali ni je unadhani kila Kiongozi anafuata hizo sheria, huwa namshangaa mtu anayeongelea habari za "mujibu wa sheria" kwenye nchi ambayo sheria huwa zinapindishwa mara nyingi na hakuna anayefanywa lolote, Magufuli mwenyewe kuna protocol kadhaa ndani ya jeshi alizivunja kiasi kwamba wanajeshi wenyewe wakabaki wanamshangaa
 
Gen Mabeyo alikuwa anajua nani anapaswa atangaze kifo cha magufuri ila nadhani aliwashirikisha baadhi ya viongozi wa kisiasa kwa kuwapima uelewa wao na ndo maana akatoa amri ya atakayetangaza kifo cha magufuri ni Bibi tozo na mjadara ukaishia hapo
 
Haya mambo yalijulikana na tuliyajadili hapa.

Mabeyo kaja kuweka rekodi wazi tu na hata hiyo kaweka kwa summary tu. Kuna mengi sana hajasema.

Kitabu kizima kikitoka mtastuka sana.
 
Jiulize kama alijua makamu ndie second kwa nn wamuite waziri mkuu kwanza? Je na yy alikua anaingiwa na kile kishawishi cha kina bashiru?

Ningekua Mobeyo ningekaa kimya tu, nikala benefit of the doubt
Mi nadhani hapa ilotumika ile mfumo dume kwamba wazri kwakuwa ni mwanaume pamoja na katibu mkuu pia ni mwanaume basi tuwaite kwanza wao maana wanawake na hisia wako karibu sana hawachelewi kupiga mayowe wakati kunahitajika utulivu kwanza ili ijulikane nini kinafanyika maana jambo lenyewe nila kustua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…