Kauli ya Fiston Mayele kuhusu Tuzo ya Mfungaji Bora 2021/22, mbio za Yanga ubingwa wa Ligi Kuu

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Mara baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabo 3-0 ambao wameupata dhidi ya Kagera Sugar, straika wa Yanga, Fiston Mayele amezungumza kwa ufupi kuhusu ushindi huo, mbio za ubingwa na kasi yake katika kuwania Tuzo ya Mfungaji Bora Msimu wa 2021/22:

“Namshukuru Mungu kwa matokeo haya, Kagera Sugar ni timu nzuri, walikuwa wakitafuta pointi tatu.

“Mungu ametusaidia tumepata ushindi, Yanga malengo yetu ni ubingwa, tumeshaanza mzunguko wa pili, bado mechi kumi na nne, tutapambana ili kushinda.

“Kuhusu ufungaji bora nitaendelea kupambana na Mungu atasaidia ili niweze kuchukua, mashabiki waendelee kutuunga mkono na wasali kwa ajili ya timu yao.”

Mayele.jpg
 
Mbona wachezaji na makocha wa ligi za Ulaya hua hawasemi hizi za 'Namshukuru Mungu' wao huongelea maandalizi, focus na mbinu.

Akishinda husikii 'Kwanza namshukuru Mungu' utasikia 'Namshukuru kocha kwa maandalizi aliyotupa na mbinu zake zimetufikisha hapa na timu nzima kwa ushirikia wake katika kupambania ushindi'
 
Ila kwa Tanzania hii, kwa sasa Mayele ndiye fowadi na hii baada ya Simba kutosajiri mshambuliaji kwa kuwaamini walewale waliotisha miaka ya nyuma. Pamoja na usimba wangu huu,namkubali Mayele na kama vipi Simba imvunjie tu kimkataba chake na Yanga.

Simba ingeachana na Kagere,Boko na Mugalu tuwe na Mayele tu au Adebayor basi tusingeona gharama zozote za kuwa na wachezaji hawa kwa sasa. Shida ipo kwa watu wanakula hela nyingi na hawana msaada kwa timu na hii hali iliwatafuna sana Azam japo kwa sasa wanaanza kubadilika. Simba bado ina mambo ya namjua namjua na uswahiba mwingi sana kwenye klabu.

Mfano Matola anachotaka yeye kuona mtu fulani anacheza kwenye mechi kwakuwa wote ni watoto wa mjini. Ili kuwa na ubora Simba inahitaji makocha wote wa nje na Matola anajua Simba inamtaka sana sio kwa sababu ni kocha mzuri bali kwakuwa ni Matola mtoto wa nyumbani.
 
Mbona wachezaji na makocha wa ligi za Ulaya hua hawasemi hizi za 'Namshukuru Mungu' wao huongelea maandalizi, focus na mbinu.

Akishinda husikii 'Kwanza namshukuru Mungu' utasikia 'Namshukuru kocha kwa maandalizi aliyotupa na mbinu zake zimetufikisha hapa na timu nzima kwa ushirikia wake katika kupambania ushindi'
Usiwapangie watu maisha Kila mtu na notion zake
 
Mbona wachezaji na makocha wa ligi za Ulaya hua hawasemi hizi za 'Namshukuru Mungu' wao huongelea maandalizi, focus na mbinu.

Akishinda husikii 'Kwanza namshukuru Mungu' utasikia 'Namshukuru kocha kwa maandalizi aliyotupa na mbinu zake zimetufikisha hapa na timu nzima kwa ushirikia wake katika kupambania ushindi'
Kuna namna nyingi za kumtanguliza Mungu, hata huko Ulaya kuna wachezaji wengi huwa wanafanya ishara za msalaba au kunyoosha mikono juu katika kuomba au kutambua uwezo wa Mungu.
 
Mbona wachezaji na makocha wa ligi za Ulaya hua hawasemi hizi za 'Namshukuru Mungu' wao huongelea maandalizi, focus na mbinu.

Akishinda husikii 'Kwanza namshukuru Mungu' utasikia 'Namshukuru kocha kwa maandalizi aliyotupa na mbinu zake zimetufikisha hapa na timu nzima kwa ushirikia wake katika kupambania ushindi'
Pole san a ulaya wanaum wanaolewa vipi na wewe
 
Mbona wachezaji na makocha wa ligi za Ulaya hua hawasemi hizi za 'Namshukuru Mungu' wao huongelea maandalizi, focus na mbinu.

Akishinda husikii 'Kwanza namshukuru Mungu' utasikia 'Namshukuru kocha kwa maandalizi aliyotupa na mbinu zake zimetufikisha hapa na timu nzima kwa ushirikia wake katika kupambania ushindi'

Kwa hiyo ungekuwa wewe ndiye Fiston Mayele, ungesema "namshukuru kicha wangu Nabi kwa maandalizi aliyotupa na mbinu zake zimetufikisha hapa na timu nzima kwa ushirikia wake katika kupambania ushindi" 😁

Wewe jamaa acha kupangia watu maisha bhana! Siyo vizuri hata kidogo.
 
Mbona wachezaji na makocha wa ligi za Ulaya hua hawasemi hizi za 'Namshukuru Mungu' wao huongelea maandalizi, focus na mbinu.

Akishinda husikii 'Kwanza namshukuru Mungu' utasikia 'Namshukuru kocha kwa maandalizi aliyotupa na mbinu zake zimetufikisha hapa na timu nzima kwa ushirikia wake katika kupambania ushindi'
Labda lugha inakupiga chenga
 
Back
Top Bottom