Kauli ya 'Kata simu kwanza kuna mtu ananipigia' huwa unaichukuliaje?

Kauli ya 'Kata simu kwanza kuna mtu ananipigia' huwa unaichukuliaje?

Inategemea na situation.

Me hii kauli naichukulia fresh tu kama ambavyo me hufanya kwa wengine.

Mimi ikiwa ninazungumza na rafiki na nikapigiwa simu ya kazini, huwa kawaida nitamwambia rafiki yangu. "samahani, naona kazini wanapiga simu, ngoja niwasikilize kisha nakurudia". ama "oya kuna simu hapa naona ya office, ngoja nipokee maramoja then nakurudia"...hapo kwenye polite language inategemea, tumezoeana vip, how comfortable are we for each other.

Ikiwa ninazungumza na simu kazini lakini kuhusu jambo lisilo muhimu sana na ninapata call kutoka kwa rafiki yangu. Namwambia mfanyakazi wangu ama mwenzangu ama boss wangu au ama yoyote hapo kazini. "Samahani, kuna simu inaingia, inaweza kuwa muhimu/emergency ngoja nipokee kisha nakurudia". kisha napokea ya rafiki yangu yule yule ambaye pia nasubilishaga.

So inategemea kulingana na simu ambayo ina uharaka zaidi, ama umuhimu zaidi, lakin siangalii mtu Mimi...unajua kuna zile emergency call lazima nipokee na kumjulisha mwingine nitampigia tena haijarishi ni nani. sasa wewe kisa boss au mtu mwenye hadhi yako lakin ukute tunaongea jambo lisilo muhimu basi niache simu za wengine!, Hapana!,..labda kama anaepiga nae nijue huwa hana jambo la muhimu hapo sawa. lakin sio kwamba eti Hana umuhimu kwangu
 
Je kwa yule anaeku hold bila taarifa nayo ipo kwenye kundi lipi?
 
Nipo naongea na manzi...gafla simu ya baba au mama hii Hapa, wahala subir nichonge na mzee au maza
 
Ukishajua kwamba simu ni communication na communication ni relay of information kwahio ukiwa unaongea na mtu hata kama ni mzazi wako current information ni known (unajua mnaongelea nini) na nyingine ikiita hata kama ni unknown number unaweza kumwambia unayeongea nae sasa kwamba ngoja upokee hii simu takupigia (sababu unknown information huenda ni urgent) na current information unajua hata ikisimama baadae itaendelea bila shida
 
Sababu mlikuwa mnaongea ujinga na sasa kapigiwa simu ya muhimu labda pesa .

Kwahiyo wewe mjinga usubiri
 
Kwa mwenye inferiority complex anaona kadharaulika, ila kwangu hapana. Ukiniambia hivyo nakuelewa sana tu kutegemea na jambo. Mf, napiga na wewe soga tu pengine muda wa kazi bosi amepiga inakuwaje hapo? Au imagine nipo mahali namsubiri mtu anifikie, kapiga wakati napiga soga na wewe, asubiri mpaka tumalize soga au nimpokelee? Wabongo ni watu wa kujishtukia sana
Nakubaliana na wewe muhasibu CPA. Najioneaga kawaida sana
 
Hiyo ni moja ya vitu vidogo vidogo sana vya kupima ustaarabu wa mtu. Ni common kwa watu wenye stress na maisha.
 
Hivi hii kauli na agizo uwa unalichukuliaje na uwa unajisikiaje!? Unapoongea na mtu kwenye simu kisha anakupa hilo agizo

Inaeleweka kuna mtu anapiga ambaye ni muhimu kuliko wewe
 
Nitachukulia kawaida kama naongea na wengine lakini siyo mwanamke wangu niwe naongea naye halafu aniambie kata kuna mtu ananipigia 😒
 
Ha ha Ndio maana vijana wanaanguka Sana kwa Pressure siku hizi.

Mbona kawaida sana hiyo.
 
Hivi hii kauli na agizo uwa unalichukuliaje na uwa unajisikiaje!? Unapoongea na mtu kwenye simu kisha anakupa hilo agizo

Kwamba simu inayoingia ina umuhimu zaidi ya iliyo hewani kwa muda huko...

Hili nalo ni gumu kueleweka?
 
Mimi ukinifanyia hivyo na mimi pia siku nyingine nakufanyia kulipiza alafu ukijiongeresha ndo ntakujibu
 
Mnakasirika vitu vidogo sana.nakata vizuri na akipiga napokea
 
Mimi naona ni sawa tuu yawezekn ni simu MUHIM ukija iache hadi huyo mtu aje kushik simu mukaongea inawezekan ikachukua siku kadhaa na either mimi ndio mwenye shida

Mimi sio shida kbsa atakama mkewang aniambie hvyo it's oky
 
Back
Top Bottom