Kauli ya Kinana iliwaondoa polisi barabarani, kauli ya nani itakuja kuondoa Tozo?

Kauli ya Kinana iliwaondoa polisi barabarani, kauli ya nani itakuja kuondoa Tozo?

Jerlamarel

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2021
Posts
843
Reaction score
2,525
Ingawaje wanasiasa wanaleta siasa kwenye mambo ya msingi, kwenye maisha ya wananchi wao, lakini siyo wote wanaowadanganya kwa hizo siasa zao.

Others can see directly their deceptions and read their minds.

Iko wazi makusanyo ya mapato ya adhabu ya makosa ya barabarani kulikuwa kuna watu flani flani wanafaidi? Kulikuwa kuna target limits kabisa kwamba mwezi huu lazima zipatikane kiasi kadhaa. Na kuna kipindi ilisemekana kila askari alikuwa anapewa target yake kila anapoenda barabarani.

Na ndiyo maana kauli ndogo tuu ya makamu mwenyekiti wa chama fulani ilitosha kumfanya IGP a-make a move. Na inavyoonekana waliokuwa wanafaidi walikuwa hawamo tena kwenye system.

Lakini huyu huyu makamu mwenyekiti amekalia kimya suala la tozo za miamala ambalo linawaumiza sana wananchi wote kwa ujumla kushinda hata hizo tozo za barabarani ambazo zilikuwa zinawaumiza wachache tuu.

Je, ukifanya compare and contrast hapo unaona ina make sense? Haimake sense kabisa.

Je ni nani atakujaga kutoa kauli itakayosikilizwa? Maana hata wakitetea oooh tozo zimetungiwa sheria bungeni ni just bluffing tuu maana hata hao askari wa barabarani walikuwepo pale kwa sheria halali na wameondoka bila hiyo sheria kwenda kubadilishwa bungeni!

FY0b2gnWQAEYgYN.jpg
 
Back
Top Bottom