Bess
JF-Expert Member
- Oct 4, 2016
- 547
- 656
Ninashangaa chama kinachojiita cha ki-demokrasia, kiongozi wao mkuu anatishia wenzake kwamba wasionje sumu kwa ulimi linapokuja suala la kugusa maslahi yake ndani ya chama.
Ghafla maswali machache yanaibuka:
Kuukubali upinzani Tanzania kwa sasa ni janga ambalo sio tu litapelekea kwenye siasa za kikanda na kikabila, bali zitaua kabisa spirit ya umoja na maendeleo kwa Taifa letu.
Heri tubaki na CCM sababu licha ya mapungufu, wana msamiati wa maendeleo, umoja na amani kwenye kutamka na kutekeleza wanayoamini.
Ghafla maswali machache yanaibuka:
- Hicho kikao kilikuwa cha maadui ama ndugu zake katika chama? Kama ni wanachama wenzake, lugha yake kwa adui inakuaje?
- Kama anafikia kusema hayo wakati hana dola vipi akipata usukani wa vyombo vyote vya dola?
- Kama anatishia yeyote anayesogelea nafasi yake ambayo ni ndogo tu ya uongozi wa chama, vipi akipewa UAMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YOTE NCHINI?
- hawa sio wale wanaopiga kelele kila siku kwamba chama tawala hakina demokrasia, wao wanaonesha asubuhi ipi kama mfano wa kuigwa? mbona kwao ni usiku linapokuja suala la uhuru wa kuomba nafasi yoyote ndani ya chama?
- Hawa sio wale tunaosema ni mbadala wa chama tawala, sasa mbona ni dead-brain katika tabia asili za kidemokrasia?