Kauli ya Magufuli kuwa Kabudi na Lukuvi hawatagombea Urais haikuwa ya ghafla, ilipangwa siku nyingi na ndio mwanzo wa mgogoro ndani ya CCM

Magufuli kawekwa na Mkapa, usiwe mbishi.

 
Hao wote kabudi wala lukuvi hawafai kuwa maraisi wa tz kulingana pia na dunia inapoelekea
 
Magufuli kawekwa na Mkapa, usiwe mbishi.
Mkapa alimwekaje Magufuli kwenye uraisi wakati unajua kila kilichotokea? Kumwambia akachukue form za uraisi? Magufuli kuwa raisi ni juhudi yake na Kikwete wala hakuwa na mpango nae kwenye list yake ya mfukoni. Bila mgongane kati ya Membe mtu wa Kikwete na Lowassa Magufuli asingekuwa raisi
 
Ngoja Dotto wa Wizara ya Fedha mtoto wa dada yake Magufuli aje awe raisi ajae ndio tutaelewa maana ya kunyooshwa!
 
Ina maana hao wajanja waliomwondoa Sokoine kimaajabu April 1984 walishajua mapema kwamba Nyerere alikuwa na mpango wa kung'atuka Novemba 1985?
Yes, Nyerere alifanya liwe wazi sana kwamba alitarajia Sokoine awe mrithi wake. Tatizo Sokoine alikuwa mkali saa, na ni kweli kuna wakati altaka kuwaweka ndani mawaziri kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Sokoine hata alikuwa na wazo kwamba ikiwa serikali iligharamia elimu hadi chuo kikuu, basi ukimaliza chuo kikuu usipewe vyeti bali upangiwe kazi na serikali, kwa kuwa watu wakipewa vyeti wengine walikuwa wanaenda nje au private sector kfanya kazi, na Sokoine alichukizwa sana na hilo na kuona ni kuiibia serikali. Wakati huo kuanzia form four hadi chuo kikuu, ukimaliza ulipangiwa kazi na serikali.
 
Kama ingefanyika hivyo wale ambao wangefanya kazi kwenye sekta binafsi wangetoka nchi gani?
 
Msingi wa kukuza uchumi huwezi kuepuka private sector.

Private sector inatoa ajira kwa Watanzania kama wana sifa.

10% ya michango ya NSSF inatoka waajiri (Private sector) 10% kwa waajiriwa wa (Private sector kupitia mishahara) ndio msingi wa michango ya NSSF.

18% ya manunuzi ya bidhaa na huduma yanayofanywa na private sector yanaingia serikalini kama VAT. Hayo ni makato ya Opex (operating cost)

30% ya net profit ya kampuni binafsi inakatwa kama corporate tax.

Usoshalist hauna maana ya kila kitu kufanywa na public sector au kila mtu aliesomeshwa kwa mkopo wa elimu ambao ataurudisha baada ya kuajiriwa.

Sidhani kama Sokoine alikuwa short sighted kiasi hicho.

Ila kwa sasa; kama JPM anataka kukuza tax base; TIC na TIB Bank zifanye kazi kimkakati ili kukuza private sector inayozalisha bidhaa na huduma ambazo kwa asilimia kubwa tuna import.

Na uzalishaji uwe na excess ili tuki-export tuwe na surplus ya balance of trade and balance of payment.

Imetosha ku-operate kwenye deficit on balance of trade and balance of payment.

Time is now
 
Mmelewa madaraka mpaka mnasahau kifo.

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
Kila mtu atakufa muda wake ukifika, na hakuna ajuaye siku wala saa.
Wewe mwenzetu unajua siku ya kifo chako? Unajuaje hao wenzio siku yao ya kufa, na nini chakufanya udhani kuwa hawatakuwa hai wapate madaraka hayo?
 
Mnaongea nini nyie mnazungumzia mende!! Lukuvi na Kabudi?ni akina nani nchi hawa ni kama Ndanda na Majimaji acheni dharau kwa nchi hii, ongea kuhusu, Jaffo, Mbarawa, Hussein Mwinyi (uhakika kbsa), Majaliwa kwa mbali na Mama Samia, Bashiru acheni Utopolo
 
Kabudi yuko pompous sana, ana kariri kwingi kuliko kuelewa.
 
nionavyo mimi hao watu wawili ndio wagombea wao wanaowaandaa,mwenyekiti aliongea vile hadharani ili kuwaepusha na mashilawadu (wasifuatwefuatwe)

naona ile kauli kama mkakati kabambe kabisa[emoji16][emoji16][emoji16]

time will tell[emoji188][emoji188][emoji188]
 
Wewe lazima unatoka Zanzibar
 
Kauli hii ya Magufuli imeweza, kwa makusudi au kwa bahati tu, kuwapumbaza Watanzania wengi kutoka kwenye hoja ya kuangalia taasisi ya urais na mabadiliko ya kimfumo inayoyahitaji, kama vile mabadiliko ya katiba kupunguza nguvu za urais, kwa rais yeyote ajaye, na kuwapeleka kwenye viroja vya kujadili nani atakuwa rais.

Mwalimu JK Nyerere, katika mkutano wa waandishi wa habari kujadili sifa za rais atakayetufaa, mwaka 1995, Kilimanjaro Hotel, aliulizwa na muandishi wa habari maoni yake kuhusu Augustine Mrema. Mgombea wa NCCR Mageuzi aliyekuwa akiwika sana wakati huo.

Mwalimu Nyerere, kwa busara zake, alikataa kuongelea watu. Alisema hajaja pale kwenye mkutano kuongelea mtu. Na kama waandishi walifikiri kaja kuongelea mtu, angefungasha virago na kuondoka zake.

Mwalimu alisema alienda pale kuzungumzia sifa za mgombea safi.

Alielewa tofauti ya kujadili mtu na kuujadili urais kimfumo. Alielewa tofauti ya kumjadili mtu na kujadili sifa za rais anayefaa.

Siasa za Afrika zinajikita kwenye kuangalia watu, badala ya kuangalia mifumo.

Mpaka leo wengi hatujajifunza somo alilofundisha Mwalimu Nyerere Kilimanjaro Hotel mwaka 1995.

 
MKuu umeongea pointi nzuri sana! Nyerere angekuwapo Magufuli asingekuwa raisi, au angekuwa raisi wa awamu moja tu - anachapa kazi sana, lakini hana sifa za kuwa raisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…