Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,443
- 4,006
Mkuu,MKuu umeongea pointi nzuri sana! Nyerere angekuwapo Magufuli asingekuwa raisi, au angekuwa raisi wa awamu moja tu - anachapa kazi sana, lakini hana sifa za kuwa raisi
Ukishaapishwa kuwa Rais vyombo vya dola vinafungua milango kuvitumia, ukiogopa kuvitumia kutokana na mamlaka yako unakuwa ni kiongozi pambo. Nakuhakikishia laiti kama Mwalimu Julius Nyerere (Hayati) angekuwa bado yupo wakati jina la Dokta John Piombe Magufuli linapendekezwa kuwania na hatimaye kuwa Rais mwaka 2015, asingekuwa na uwezo wowote wa kumtoa kwa kuwa hekima ya namna ya kushughulika na wastaafu wote amejaaliwa kuwa nao, hivyo hoja kuwa angemng'oa kwa viisngizio vya demokrasia vinavyosemwa kwa sasa ni kujifariji tu.
Ukitaka kuthibitisha wale wote waliojasiri kuropoka matakwa yao waambia wafanye jaribio tu la kufanya mzaha usio jenga barafu itaganda kwa maji ya moto.
Wewe sikia tu usikutane na Mh Rais Magufuli maneno yote uliyopanga kumshambulia yatakuponyoka au kukuletea athari hata kabla yeye hajatamka chochote dhidi yako.
Nimeandika haya nikiwa naamini kabisa baadhi ya watu ambao mimi mwenyewe nimesoma nao ambao wana nyadhifa kadhaa serikalini pamoja na ujasiri wao na ujuaji mwingi wa enzi hzo ninazozikumbuka mie wanazimika ghafla wasielewe namana ya kutunisha misuli waliyokuwa wanajidai nayo huko nyuma.
Ukitaka kwenda na Rais Magufuli vizuri bila shida mkosoe kwa staha nahoja jenzi atakuheshimu na kutumia changamoto hizo kutatua upungufu uliouanisha kwa ustadi bila kinyongo chochote.
SIASA sio kuhoji kwanini wewe ni mfupi, kwanini wewe ni mweusi, kwanini wewe una ulimi mzito, kwanini wewe, hauamini ubatizo au kuslimu nk
SIASA ni kumulika mwanga wa tochi kwenye giza na kuonesha njia ambayo inakidhi matamanio ya watu wengi kufikia malengo ya mtu mmoja mmoja, jamii na taifa kwa ujumla katika mawanda ya usawa, uhuru, haki na maendeleo ya washika dau.
SIASA sio ugomvi kushusha hadhi ya itikadi ya mtu, kikundi, jamii au taasisi fulani ilimradi sheria za nchi zinazingatiwa ipasavyo.