Kauli ya Membe kwamba "Wakati wao hawakuteua vijana sana"

Kauli ya Membe kwamba "Wakati wao hawakuteua vijana sana"

August

Platinum Member
Joined
Jun 18, 2007
Posts
10,983
Reaction score
7,157
Nilikuwa kusikiliza BBC Swahili asubuhi hii, ambapo imenukuliwa kwamba Membe anaipongeza awamu ya tano kuhusiana na infrasture kama barabara flyover, SGR na uteuzi wa vijana ingawa bado anawatumbua tumbua, tofauti na "wakati wao"

Sasa nimetafakari wakati wao yeye Membe na nani au alishakuwa "Rais" wetu hapo kabla moja kwa moja au kwa kupitia mtu mwingine au kikundi hivyo angependa kuongezea hapo kwa kuwa Rais moja kwa moja bila kutumia kikundi, au Mtu mwingine.

Kingine alicho ongelea ni kushukia kwa demokrasia katika awamu hii. Bila kuchanganua mzigo alioachiwa Rais wa sasa wa my reform nidhamu ya kazi, matumizi, efficiency, na quality ya mazao yetu au miradi yetu yenye kuweka uchumi kuwa endelevu.

Hivyo kusababisha Kiongozi aliyepo kuwekeza zaidi ktk mambo hayo ya msingi kuliko kuimarisha demokrasia ktk lundo la takataka, hili lingeleteleza Matatizo na manunguniko kwa wale ambao wasingeweza kushiriki hiyo domokrasia kwa kukosa fedha za Rushwa na kujibinafsishia "mali za serikali" iwe hunting blocks, kwenye gas, kwenye umeme, n.k
 
Umeandika nini sasa? Nawe ni hao hao wa Lumumba takataka! Ben Saanane, Azory, Mawazo, maiti kwenye sandarus coc beach, we can not condone maendeleo at the loss of life! Rubbish!
 
Huyu Mzee asipopata muda wa kukaa akatulia, tunahatari ya Kumpoteza Sisi kama Taifa! Huu ni Wakati wa yeye kutumika katika sehemu ya Ushauri ktk Taifa,

Kitakachokuja kumfanya atuache, ni pale upinzani wanaposhindwa kumhurumia kumwambia ukweli kwamba, anaingia kugombea nafasi ya Uraisi ambayo hawezi kushinda, ili ajitafakari zaidi, matokeo siku yanatangazwa, hapo ndo kwenye mashaka yangu, asije Tu akajikuta amedodoka kama kuku wa mdondo.

Tunamhitaji huyu mzee kama mtu mhimu katika Taifa letu, amelifanyia mengi Taifa letu kwa kujituma ingawa pia anahusishwa na uporaji wa pesa za Gadafi.
 
Umeandika nini sasa? Nawe ni hao hao wa Lumumba takataka! Ben Saanane, Azory, Mawazo, maiti kwenye sandarus coc beach, we can not condone maendeleo at the loss of life! Rubbish!
Unatakiwa kuelewa siasa, haiendi hovyo hovyo, mwishowe tutakuwa kama central africa republic au nchi zingine zenye internal problem.
Angalia Iraq , Libya ,Afghanistan , hivyo unatakiwa kuelewa ingredients za democracy.

Angalia Russia walianza na Glasnost, China wakaanza. Na economic reformation, mwishowe russia ikapangaranyika, china leo hii ni giants in the world economically na military.

Sasa wa Russi wamejitambua unaona Putin anapiga Raisi 10 yrs anakuja kuwa PM ana rudi kuwa Raisi.

Wewe njaa yako ni ya democrasia au uchumi kwanza?

Hizo western countries au developed countries walianza na Democracy au maendeleo ya "vitu" ya uchumi?
Usiwe bwege mtozeni, hao western countries wana release kitu kwa watu wengine baada ya wao kuwa wame move kwenye kitu kingine ili wawe a step ahead yako.

Sasa wewe unataka kuwafuata wao, huwezi
 
Membe "mbobezi" katika mambo Mengi kuliko watanzania wengi anatakiwa kuelewa au kujikumbusha kwamba demokrasia haijawahi kumletea maendeleo mtu bali kumrudisha mtu nyuma ambaye bado hajajiwekea msingi ya uchumi ambayo ni uzalishaji na huduma zinazoendana na suala hilo, na mfano halisi ipo kwenye jamii zetu, wanao practice hiyo democracy utaona mtoto au watoto wataleta wajukuu , maboy friend na ma girl friend kwa Wazazi wao badala ya kufikiria kujitegemea, wakati wale waliochukulia maisha ni mapambano utaona watoto nao hujiongeza.
 
Back
Top Bottom