Kwa hiyo FF unamaanosha apuuziwe sababu ya "uchizi" wake?
Huyo huwezi kumpuuza, hana ujinga wa kuweza kupuuzwa na hauna ujanja wa kumsema kuwa ana makosa. Ni mtu anaeelewa anafanya nini.
Mimi nimejaribu kuifafanuwa lugha yake, ni ya kikariakoo na nikaeleea kidogo alikotokea. Ana sifa hizi:
1) kazaliwa mjini, kakulia mjini, enzi za utemi wa mjini.
2) kaanzia kazi jeshini na kaishi huko.
3) Kaishi nje ya nchi kwa miaka mingi (kwa hiyo ana exposure).
4) Kwenye siasa kaanzia mitaani mpaka sasa Naibu Spika, anazijuwa corridor za kisiasa vilivyo.
5) Shule kaenda na Madrassa kaenda. Humwambii kitu.
6) Mbunge wa wilaya ambayo ni kitovu cha utajiri wa Tanzania.
7) Mbunge wa wilaya ambayo ni kitovu cha siasa za Tanzania.
8) Dar ni maarufu, tena maarufu kweli kweli, circle zote anazijuwa, za kisiasa, za kibisashara, za kisomi, za kidini.
9)( wengi hawalijuwi hili, huyo kishakuwa mchezaji mpira mzuri sana. Kilichomrudisha nyuma kwenye mpira ni kwenda jeshini tu, nadhani kitengo chake kule kilikuwa kinahusika na mambo nyeti sana, hakuwa na muda mrefu wa kujiendeleza kimpira.
Mtu kama huyo utamueleza nini wakuja kama wewe?
Elimu humpati, madrassa humpati, utoto wa mjini humpati, umaarufu humpati, exposure humpati, siasa humpati. Umaarufu humpati. Inabidi umuombee mema na azidi kuwa mwema.
Sasa nikueleze alivyo "down to earth". Hivi na uspika wake, kuna siku nimemkuta ghafla kakaa kwenye mabenchi na mkewe (nafahamiana na mkewe) pale Regency wanangoja namba wamuone Doctor, basi kaja kijana kujpendekeza pale, mzee njoo huku, Azzan akanyanyuka akamsikiliza akaja kukaa, nikajuwa kamkatalia kwenda kabla ya aliowakuta hawajaenda mwanzo. Ingawa alitaka kkupewa "priority", akagoma, mkewe ananinong'oneza, huyu mzee mie naumwa, yeye anataka nisote tu hapa, hakubali tuingie mpaka tuliowakuta mbele wamalizike.
Huyo ndiyo Zungu, "a man down to earth".
Allah ampe umri mrefu na amzidishie hekima. Amiin.