Msiyemfahamu Zungu, hilo toto la Kiarabu la kariakoo, limekiwa na manunda wa Gerezani na mchikichini, enzi alizokulia huyo mitaa yake yote ni ubabe tu, ukiwa bwege bwege unaonewa, kama haitoshi, kutoka hapo akachaguliwa kwenda jeshini kutokea shule. X soldier huyo, wengi tunaomfahamu huyo Kariakoo tukawa tuna uhakika huyo ni mtu wa system. Enzi za Nyerere ukichaguliwa kwenda jeshini ili uwe "system" juwa huyo ni kipanga "multi-talented".
Sikilizeni vizuri lugha yake bungeni, hataki wala hapendi longolongo na amri zake zimekaa kijeshi na kibabe, zimechanganyika pamoja. Mtajaza wenyewe.
Zamani niliwaambia watu, huyo ni 99% "chizi kapewa rungu" msije mkashanga siku akimwambia mbunge "we msenge kaa chini".
Huyu mimi naamini na uzee wake sasa hivi, ukimletea ujinga anakurukia kichwa.