Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kawaida, chama cha siasa kilichopo madarakani kwa kuchaguliwa ki-demokrasia, hakipaswi kuondolewa madarakani kwa nguvu. Uhalali wa kuiondoa serikali madarakani unapaswa uwe kupitia sanduku la kura katika uchaguzi wa kidemokrasia, na kama kuna ukiukwaji wa haki za uchaguzi, mfumo wa sheria wa nchi unapaswa kurekebisha hilo.
Lakini pale inapothibitika kwamba chama kilicho madarakani kinatumia udanganyifu kuendelea kuwa madarakani, na haiwezekani kupata haki ya uchaguzi kupitia mfumo wa sheria au mahakama, ndipo inapokuwa halali kuiondoa serikali ya chama kilichopo madarakani kwa kutumia nguvu.
Kauli ya aliekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido, Marko Henry Ng'umbi, na ile ya Nape, na muundo wa sasa wa Katiba ya Tanzania vina athari kubwa sana juu ya jambo hili. Na si mara ya kwanza CCM wanafanya hivi, kwa kiburi, kujigamba na kujiona wako juu ya sheria, kama video kwenye hii thread inavyoonesha, kwamba wao wameshauingilia mfumo wa sheria na mahakama. Utaona kwamba, kama hadi sasa kumetolewa kauli ambazo zinaonyesha serikali ya CCM imekuwa ikitumia nguvu na hila kushinda uchaguzi, na uchaguzi mmojawapo ni ule wa raisi ambao hauwezi kupingwa Mahakamani, basi ni wazi kunakuwa hakuna njia nyingine ya kupata haki ya uchaguzi nchini bali kwa kutumia nguvu, ili kurudisha mazingira ya demokrasia na haki katika uchaguzi, pamoja na mfumo wa sheria ulio huru.
Na hili linatiwa nguvu na na muundo wa Katiba ya Tanzania ambayo hairuhusu matokeo ya uchaguzi wa raisi kupingwa Mahakamani. Katika mazingira hayo, swali linakuwa, kama tuna Katiba ambayo hairuhusu kwenda Mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi wa Raisi, na hali zimethibitishwa kwamba kunakuwa na utumiaji nguvu na hila kwa chama kilichopo madarakani wakati wa uchaguzi, hali hiyo itarekebishwa vipi? Labda wale watakaoona bado hali hii haitoi uhalali wa kutumia nguvu, watuambie suluhisho hapo linakuwa nini.
Nakumbuka maneno ya Nyerere na Mandela, ambao hata walienda mbali zaidi, kwa kusema iwapo kunakuwa na ukosefu wa uchaguzi wa kidemokrasia, na wale waliopo madarakani hawaruhusu mfumo wa kisheria uruhusu upatikanaji wa uhalali na haki katika uchaguzi, basi inafikia mahali mapambano ya silaha kudai haki yanakuwa halali. Je, Tanzania bado hatujafikia hali hizi? Au je, huko ndiko tunakoelekea?
Mambo yanayofanywa na CCM ndio mambo ambayo yalihalalisha tuwasaidie Zanzibar kwenye mapinduzi yao, Msumbiji, Zimbabwe, Uganda, nk, na hata kuwaunga mkono Biafra wa Nigeria katika mapambano yao ya silaha kutafuta uchaguzi ulio huru na halali. Na sasa tunaona kila sababu ya kufanya hilo ndani ya nchi yetu wenyewe - kuwaondoa CCM kwa nguvu kwa sababu hawana tena legitimacy ya kuondolewa kidemokrasia kwa kura, kwa sababu wamekuwa wakiihujumu hiyo demokrasia wakijua watajilinda nyuma ya Katiba yetu isiyoruhusu kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Raisi Mahakamani, na kwamba wana uwezo wa ku-undermine judicial system ya nchi pale matokeo mengine ya uchaguzi yanapopelekwa mahakamani. Tukitaka kubadili Katiba wanazuia hili. Wanatuachia option gani?
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!
- Kuelekea 2025 - DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!