Hamjambo wote!
1. Ebana eeeh! Lazima tuseme ule ukweli ili utuweke huru. Tukisema tunamung'unya maneno na kujiumauma tutaishi kwenye kiza na shimo miaka na miaka.
2. Tumefundishwa tangu tukiwa wadogo kuwa duniani hakuna kinachoshinda nguvu ya umma.
3. Tulikaririshwa hivyo kuanzia kwenye uraia, civics, General studies n.k.
4. Wapo watu wanaamini hivyo pia. Mimi nilitaka kuwa mmojawapo lakini hesabu zangu zinakataa.
5. Nikasema, acha nifikiri kinyume na akili na hesabu zangu. Kwamba Hakuna nguvu kama Nguvu ya umma.
6. Historia inaonyesha waliokuja kucchukua watumwa afrika walikuwa wachache Sana. Kwamba watu kumi wangeweza kuwaswaga watu elfu moja.
7. Nikakumbuka kuwa People Power ni kanuni za kidemokrasia na wala kwenye uhalisia haina maana yoyote. Haina ukweli wowote. Ukweli upo kwenye Ukubwa we Pua sio wingi wa makamasi. Kumaanisha nini?
8. Nilikuwepo kwenye maandamano. Watu walikuwepo maelfu kwa maelfu. Tulikuwa wengi Sana
9. Lakini gari yenye Askari watatu mpaka watano tuu wenye silaha walitosha kabisa kutufanya tukimbia kama mizimu iliyotoroka kuzimu. Tulikuwa wengi lakini hatukuwa na nguvu yoyote. Hakukuwa na nguvu ya umma mbele ya chuma.
10. Tumeona Iran na maeneo mengine. Iran wamejitokeza watu wengi sana. Lakini walipotokea watu wenye silaha(Askari) people powers haikuonekana. Waliyeyuka kama mshumaa kwenye moto.
11. Sipendi uongo. Sipendi faraja hasa ya uongo. Sipendi ushindi wa kutegemea huruma au uzembe wa opponents.
12. People power kauli ya kitapeli kabisa. Haina ukweli wowote ule. Kauli ya kisiasa ya watu walioamua kujifariji.
13. Ukweli ni kuwa Mwenye silaha na teknolojia ndiye mwenye nguvu. Anaweza kuwa mmoja tuu na kutiishia mamilioni ya watu.
14. Usiseme walikuwa wanaua au wanapiga risasi.
15. Wewe ulitakaje? Mwenye nguvu ni Yule mwenye options nyingi. Mwenye uwezo WA kuamua atumie option ipi ili ashinde. Bila kujali options atakazotumia ni halali au haramu. Dhulma au Haki.
16. Sisemi kuua watu ni halali au Jambo zuri. Ila nazungumzia NGUVU.
Iwe ni NGUVU za GIZA au NGUVU za Nuru.
17. People power haina tofauti na MajiMaji War. Ni Imani isiyo na ukweli. Mwishowe ni kilio, maumivu, na kusaga meno.
18. Nimejifunza kuwa, watu hawana nguvu. Hasa ukisema Watu wengi. Kushabikiwa au kupendwa na watu wengi sio chochote labda kwenye ulimwengu wa Demokrasia na Uhuru.
19. Lakini kwenye ulimwengu wa matokeo ambao haujali kanuni moja. Unaoweza kutumia Demokrasia au Mabavu. Watu sio chochote kile.
20. Chochote ni Teknolojia, silaha, Pesa na roho ngumu isiyojali na isiyosita kufanya maamuzi magumu yasiyotoshana na akili ya kawaida.
21. Kama Jeshi, na wenye pesa hawatakuwa upande wa maandamano au kutetea HAKI, sioni namna People power ikifanya KAZI.
22. Sikatishi watu tamaa. Nazungumzia uhalisia.
. Bado Najifunza.
TaikonMASTER
Kwa sasa Golden Tulip, Masaki. Dar es salaam