Kauli ya Rais Samia inaashiria kuwa CHADEMA hawako salama ndani ya chama hicho wapo vijana wake wa "Kitengo"

Kauli ya Rais Samia inaashiria kuwa CHADEMA hawako salama ndani ya chama hicho wapo vijana wake wa "Kitengo"

Akihutubia kwenye maazimisho ya miaka 20 ya jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro Septamba 17, 2024 rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa uovu wote uliopangwa kwenye mkutano wa chama kimoja cha upinzani (CHADEMA) anazo taarifa zote

Rais amesema kuwa interenjesia ya vijana wake ina uwezo mkubwa imepata taarifa za kikao chao chote kilichofanyika Septemba 11 mwaka huu na kwamba uovu wao wote waliopanga juu ya Serikali yake ameufahamu

Hivi karibuni baada ya kifo cha kada wake aliyetekwa na kuuwawa na watu wanaodaiwa wasiojulikana viongozi wa CHADEMA walikutana Arusha na kufanya kikao cha dharura cha kamati kuu

Kikao hicho kilitoka na maazimio kuwa ifikapo septamba 23 mwaka huu vijana wote wa chama hicho nchi nzima wakutane jijini Dar na kufanya maandamano ya amani

Lengo la maandamano hayo ni kushinikiza watu waliomteka na kumuua kada wao Ally Kibao wanafahamika na kuchukulia hatua za kisheria na makada wake watatu Soka na wenzake waliotekwa na watu hao hao wasiojulikana waachiwe huru au kama wameuwawa miili yao ikabidhiwe kwa ndugu zao ili izikwe

Kauli ya Rais Samia kuwa interejensia ya vijana wake iko vizuri na ndio maana kilichojadiliwa kwenye kikao hicho cha CHADEMA hotuba nzima anayo na kujua uovu wao mwingine waliopanga inamaanisha kuwa vijana wake wa kitengo ni miongoni mwa baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho

Pia kauli hiyo ya Rais inaashiria kuwa kama sio baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho kuwa watu wa kitengo basi vijana wake wa TISS au Polisi wameweka vifaa vya kunasa sauti kwenye ukumbi uliofanyika kikao hicho cha dharura cha CHADEMA cha kamati kuu ambacho ni cha viongozi wa juu tupu (Vingunge)

Kama ni kweli kiongozi mmoja wapo wa juu wa CHADEMA ni mtu wa TISS basi yamkini chama hicho hakiko salama na siri zake nyingi zitaendelea kutoka na kufika Serikalini bila yao kujua nani anazipeleka

Hivyo CHADEMA wanahitaji nao kufanya intelejensi yao iliyotukuka ya kumbaini kiongozi au viongozi hao wa kamati kuu ya chama hicho ambao ni watu wa kitengo

Comasa

PIA SOMA
- Rais Dkt. Samia: Nina taarifa ya kikao chao cha Arusha, wanapanga uhalifu, Serikali ya Tanzania haiondoshwi hivyo
Alidondoka Idi Amin, Adolf Hitler, Jiwe,Pinochet, na kenge wengine, sembuse huyu kilaza
 
CHADEMA wamekomaa hawataki mazungumzo wao wanasema wamechoka turaona kama tutavuka salama salimini baada ya keshi sptemba 23
 
Kwa nini hukufikiria maongezi ya hicho kikao yalinaswa kwa vyombo vya udukuzi(bugging)??
 
Wazeni nje ya box, vikao vya chadema viwe live kwenye mitandao yote, YouTube, TikTok, Facebook, Instagram


Pia watu watoe maoni live kwenye comments mitandaoni,hapo intelijensia inakuwa haina kazi
Kuna vikao vya siri hivyo ndio serikali wanaviogopa
 
Kwa nini hukufikiria maongezi ya hicho kikao yalinaswa kwa vyombo vya udukuzi(bugging)??
Yote hayo yanawezekana serikali ina mbinu nyingi wanaweza hata kutumia wadukizi kunasa habari za wapinzani wao
 
Pale msibani alipozomewa masauni hakuna aliyepanga iwe hivyo, ni watu tu wana hasira na serikali ya ssh. ajikite kwenye utawala bora, adui yake sio chadema.
Kweli kabisa yeye angejika huko kama awali alipoingia madaraka na 4R alifanya vizuri mpaka nchi za magharibi na jumuiya za kimataifa zikampongeza nchi ya Tanzania ikaanza kurudi kwenye diplomasia yake ya zamani
 
Kwenye hili la kupanga Uhalifu ni uongo, Ama Rais Kadanganywa ama kaamua kuzusha mwenyewe ili atimize lengo lake la kuwaumiza Chadema

Maazimio yote ya Chadema huwekwa hadharani, hawajawahi kuficha

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Rais kuongea yasiyokuwepo, Wakati wanamkamata Mbowe alisrma Mbowe ni gaidi na kwamba Wenzake walikwisha Hukumiwa, lakini ni akina nani waliohukumiwa kabla ya Mbowe kukamatwa?
Wanasiasa wa pinzani Nchi zetu hizi za dunia ya 3 wanapitia magumu sana time will tell
 
Back
Top Bottom