Buyaka
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 1,705
- 1,953
Baada ya kuahidi kushughulikia changamoto za soko la Kariakoo, Mhe. Rais S.S. Hassan amewaambia wananchi "na nyinyi wakati serikali inawabeba, wanasema abebwae hujikaza, na nyinyi jitahidini kufuata sheria zinazowekwa katika maeneo mlipo maanake nimeona njia zote zimezingiwa, vibanda kila pahali..."
My take:
Tafadhali sana viongozi wetu, tunaomba muondoe huo mtazamo kwamba mnatufanyia hisani!
Serikali na Rais wa nchi hawambebi mtu. Wanatimiza wajibu wao. Rais aliomba kura anatimiza ahadi za kutatua matatizo. Watumishi wa umma wa kawaida wameajiriwa, wanalipwa mshahara, wanatimiza wajibu wao. Hakuna anaebebwa.
Isitoshe, utaratibu (au kutokuwepo na utaratibu) wa kuuza bidhaa njiani na kujenga vibanda ovyo ovyo ni serikali yenu imekuwa ikihubiri kwa nguvu kwamba hakuna sheria nchi hii inayosema Mmachinga haruhusiwi kufanya biashara popote.
Kama mmebadilisha mwelekeo msituambie mnatubeba! Please!
Clip hii hapa ya Rais na Makamu wake wa Rais wakidadavua kinaga ubaga policy za umachinga na haki zao kwa mtazamo wao, sio wa kwetu sisi Wamachinga.