Idea ya Jiwe ya vitambulisho vya machinga ni bomu lililokuwa linasubiri kulipuka.Sio kwa utararibu huo,watu wanaacha kazi za maana kama kilimo,uvuvi,ufugaji n.k huko vijijini kwao,wanakuja kuwa machinga ,kuuza bidhaa toka China.Huko vijijini wameachwa wazee ndio wanaendeleza kilimo.Nguvu kazi yote inazurura mjini.Ilikuwa ni suala la muda uchumi unaotegemea kilimo kwa asilimia zaidi ya 70 ,ungeanguka!
Jiwe alitakiwa kutoa ruzuku kwa wakulima vijijini ,hata kwa kupunguza bei ya mbolea,mbegu na pembjeo kwa ujumla wake.ili kuwavuta kufanya kazi zenye tija huko vijijini badala ya kuzurura kutwa-kuchwa na biashara ambazo hazieleweki!